Wednesday, March 27, 2013

ADVANC BANK WAZINDUA TAWI JIPYA TEMEKE DAR




 Mwakilishi wa Mbunge wa Temeke, Thabit Mussa akikata utepe wakati wa uzinduzi wa jengo la benki ya Advanc, Temeke jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Peter Moelders na kulia ni Kaimu Meneja wa benki hiyo, Boniface Mhali na diwani wa Temeke, Hamisi Msombo. (Picha na Habari Mseto Blog)
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Advanc, Peter Moelders akisakata muziki wa asili na msanii wa kundi la Wanne Star, wakati wa uzinduzi wa benki hiyo, Temeke jijini Dar es Salaam.
Wasanii wa kundi la  Wanne Star na kundi lake akitumbuiza wakati wa uzinduzi wa tawi la benki mpya ya Advanc, Temeke jijini Dar es Salam jana

DAR ES SALAAM, Tanzania 

BENKI ya Advanc imetakiwa kuonyesha tofauti yao na benki zingine kwa kutoa riba nafuu na masharti yanayowezekana kwa wakopaji ili kulisaidia Taifa kiuchumi kupitia wajasiriamali wadogo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi la benki hiyo wilayani Temeke jana, mwakilishi wa mbunge wa Temeke, Thabit Massa alisema ingawa kuna benki nyingi nchini lakini riba na masharti magumu yanafisha ari ya watu kukopa.

Mwakilishi huyo wa mbunge alisema kufunguliwa kwa tawi hilo kunafanya Temeke kuwa na matawi saba sasa ya benki lakini bado hakujawa na mafanikio tarajiwa na mbaya zaidi baadhi ya benki hizo hazina huduma nzuri kwa wateja.

“Lugha nzuri hakuna na hata mikopo imekuwa ikitolewa kwa kujuana baina ya wakopaji na watendaji wa baadhi ya benki jambo ambalo sio jema na linashusha imani ya wateja kwa benki” alisema na kuongeza kuwa anatarajia mabadiliko.

Alisema beni hiyo inatakiwa ije na mambo tofauti ili kuleta tija kwa wakazi wa eneo hilo tofauti na ilivyo sasa na awali Mtendaji mkuu wa benki hiyo, Moelders alisema wamekuja ulata mapinduzi makubwa katika uduma za kibenki nchini.

“Benki yetu walengwa wake na wananchi wa kawaida na wale waliopo vijijini na kabla ya mwisho wa mwaka huu itafungua matawi mawili Jijini Mwanza na mwakani watazindua matawi mengine ya idadi hiyo Jiji la Mbeya.
Alisema

No comments:

Post a Comment