Meneja wa Bia
ya Safari Lager, Oscar Shelukindo(wapili kushoto),Mtaalamu wa
kutengeneza Bia wa Kiwanda cha Bia Dar es Salaam, Calvin Nkya
(kushoto),Mtaalamu wa Kutengeneza Bia Afrika Mashariki,
Machiel Bosch na Meneja wa Kiwanda cha Bia cha TBL Dar es Salaam,Calvin
Martin wakionyesha tuzo ilizozitwaa Bia ya Safari Lager Afrika
Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akielezea namna zilivyopatikana tuzo hizo
Oscar Shelukindo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)
Bia
ya Safari Lager inayotengenezwa na kampuni ya bia Tanzania (TBL) imenyakua
zawadi ya jumla katika mashindano ya kwanza ya ubora wa bia yaliyoandaliwa na
taasisi ya IBD (The Institute of
Brewing and Distilling). Mashindano haya ya kusisimua yaliyofanyika mapema
mwezi huu kuanzia tarehe 3 hadi 8 katika jiji la Accra Ghana yalishuhudia
kampuni ya kutengeneza bia ya SABMiller Afrika ikipokea tuzo 10 kati ya 13
zilizotolewa, ikiwemo tuzo hii ya ubingwa wa jumla wa mashindano haya
iliyonyakuliwa na bia ya Safari Lager ya hapa Tanzania.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini leo, Bwana Oscar Shelukindo, Meneja wa bia ya
Safari Lager alisema kwamba, “Nchini Tanzania, bia yetu ya Safari Lager
inafahamika vizuri kwa ladha yake yenye ubora wa hali ya juu usiobadilika, hili
si jambo geni miongoni mwa watanzania. Lakini kutunukiwa tuzo ya ubingwa wa
jumla katika mashindano yanayoshirikisha bia nyingi nyingine za bara letu la
Afrika ni jambo la kutia fora sana!. Ukweli kwamba Safari Lager imenyakua pia
tuzo ya ubora wa bia za Afrika zenye kiwango cha kilevi cha zaidi ya asilimia 5
inadhihirisha kwamba tumejizatiti katika umakini wa utengenezaji bia. Tuzo hii
ya ubingwa wa jumla inawapa wateja wetu uhakika kwamba kweli wanakunywa bia
Bingwa”. Alimaliza Bwana Shelukindo.
Zaidi
ya bia aina 50 tofauti kutoka katika makampuni maarufu yanayotengeneza bia Afrika
yalishiriki mashindano haya, yakiwemo makampuni kama SABMiller-Africa na SAB
ltd. Taasisi ya IBD ilikusanya wataalamu huru kutoka katika mabara matatu
tofauti ili kuonja bia na kutoa maamuzi yasiyo na upendeleo wowote. Wataalamu
hawa kwa pamoja wana uzoefu wa jumla ya zaidi ya miaka 500 katika kazi hii.
Katika mashindano haya bia hizi zilipimwa katika makundi tofauti kama vile, bia
zinazotengenezwa kwa kutumia malighafi zinazopatikana sehemu inapotengenezwa
bia yenyewe, bia zenye kiwango cha kilevi cha chini ya asilimia 5, na pia kundi
la bia zenye kiwango cha kilevi cha zaidi ya silimia 5. Tuzo ya juu kabisa ya
tuzo za bia za Afrika ni tuzo ya ubingwa wa jumla wa bia zote zilizoshiriki,
tuzo hii imenyakuliwa na bia yetu ya Safari Lager.
Kwa
kupewa tuzo hii ya ubingwa wa jumla, Safari Lager imedhihirisha kwamba kweli ni
Bia Bingwa, sio tu kwa hapa Tanzania na ulimwenguni kote, lakini hasa hasa kwa
bia nyingine za aina yake za hapa Afrika.
Safari Lager imenyakua pia mara tano tuzo za ubora wa bia zijulikanazo
kama Gold Monde Selection, hii ni kwa sababu ya ladha yake bora isiyobadilika.
No comments:
Post a Comment