KIkosi cha Juve kilichopenya robo fainali Ligi ya Ulaya |
MABINGWA wa Italia Juventus jana walifanikiwa kuingia robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuilaza Celtic mabao 2-0 na kufuzu kwa jumla ya mabao 5-0, huku PSG ya Ufaransa nayo ikipenya hatua hiyo kwa sare ya 1-1.
Juventus iliyokuwa uwanja wake wa
nyumbani mjini Turin, ilipata mabao yake katika kila kipindi bao la
kwanza likifungwa dakika ya 24 na Alessandro Matri na kufanya hadi
mapumziko matokeo yawe 1-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote
kushambuliana, lakini ni Juventus walioendelea kutamba kwa kujipatia
bao la pili lilitumbukizwa kimiani na Fabio Quagiarella.
Katika mechi nyingine iliyochezwa jana
usiku, PSG ilifanikiwa kuungana na timu za Real Madrid, Borrusia Dotmund
na Juventus hatua ya robo fainali baada ya kulazimishwa sare kwenye
uwanja wake wa nyumbani na Valencia ya Hispania.
Hadi mapumziko timu hizo mbili zilikuwa nguvu sawa kwa kutofungana licha ya kushambiuliana na kufaya kosa kosa kadhaa.
Kipindi cha pili kilianza kwa Jonas wa
Valencia kuipatia wageni bao la kuungoza katika dakika ya 55 na
kuwafanya wenyeji kucharuka wakisaka bao.
Juhudi zao zilikuja kufanilkiwa katika
dakika ya 66 kupitia nyota wake, Ezequiel Lavezzi na kuifanya timu hiyo
iliyomchezesha nyota wa zamani wa England, David Beckham kusonga mbele
kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya mechi ya awali kumalizika kwa PSG
kushinda mabao 2-1 ugenini.
No comments:
Post a Comment