Monday, March 25, 2013

KILIMANJARO VAISAKHI RALLY 2013, JAMIL KHAN AIBUKA MSHINDI



DEREVA Jamil Khan wa timu ya Dar es salaam, akisaidiana na Rahim Suleiman amefanikiwa kuibuka mshindi wa mashindano ya magari ya Kilimanjaro Vaisakhi 2013. 
Kwa ushindi alioupata Jamil katika mashindano ya kilometa mia moja, zilizoanzia katika uwanja wa Sikh mjini Moshi hadi Kia kupitia Bomang'ombe, Sanya juu na kurudi Moshi kunampa fursa ya kujiwekakatika nafasi ya kuchuana kutafuta mshindi mwaka wa taifa.
 
Wengine waliofuzu ni dereva mkongwe wa timu ya Pandya, Mzee Kirit Pandya aliyeshika nafasi ya pili, akisaidiwa na Awadh Bafadhil, Gurjit Singh Dhani wa timu ya Shameer Yusuf, Shafin Khan wa timu  ya Evolution, akisaidiwa na Moses Matovu na Dereva Salvatory Mcharo akisaidiwa na Akram Hafidh.
 
ERIC CORMACK AONGOZA MZUNGUKO WA KWANZA

Dereva Eric Cormack na akisaidiwa na Daudi Charles kutoka timu ya kula vumbi kutoka Arusha juzi alifanikiwa kuongoza raundi ya kwanza ya mbio za magari za Kilimanjaro Varsakhi 2013, yenye umbali wa kilometa 20, kwenda hadi TPC kupitia mabogini na kurudi uwanjani Sikh Club Moshi mjini. 
Cormack alikuwa wa kwanza kuondoka uwanjani hapo na kufanikiwa kuongoza mzunguko huo wa dakika kumi na tano, akifuatiwa kwa karibu katika nafasi ya pili na Dereva Gerrard Miller akisaidiwa na Peter Fox
wa timu ya Abu kutoka Arusha, nafasi ya Tatu ikishikiliwa na Dereva mkongwe katika historia ya mashindano hayo, Mzee Kirit Pandya akisaidiana na Awadh Bafadhil wa timu ya Pandya kutoka Kilimanjaro, huku Marco Ferreira wa kula vumbi ya Arusha akisaidiwa na  Ratnaveer Darbar na Jayant Shah wa timu ya Jayant kutoka Dar es salaam akisaidiwa Ravi Chana wakimaliza katika nafasi za nne na tano kwa mfatano huo.
 
Awali akizungumzia lengo la mashindano hayo, Mwenyekiti wa klabu ya magari ya mashindano ya Kilimanjaro (KMSC), Bonzon Louis ambaye pia ni dereva kutoka timu ya Kiduku alisema, lengo ni kukusanya pointi kwa mshindi wa jumla atakayetawazwa kuwa bingwa wa taifa mwisho wa mwaka.
 
Louis alisema mashindano kama hayo hufanyika kila mwaka katika mikoa ya Arusha, Dar es salaam, Tanga, Morogoro na Kilimanjaro na hatimae kutokana majumuisho ya pointi anapatikana bingwa wa taifa.
 
Alisema changamoto ni kukosa wadhamini pamoja na elimu ndogo miongoni mwa wananchi kuhusu mashindano hayo na kuongeza kuwa hata ajali aliyoipata katika eneo la mabogini lilitokana na wananchi kupanga mawe barabarani kuzuia magari.
 
Mashindano hayo yaliendelea jana kwa mzunguko wa mwisho wa umbali wa kilometa mia moja, yaliyoanzia katika uwanja wa Sikh Moshi saa mbili asubuhi kwenda KIA kupitia Sadala, Bomang'ombe, Sanya juu hadi KIA na kurudi Boma katika hoteli ya Snow view kabla ya msafara kurejea Sikh Club kwa zoezi la utoaji wa zawadi.
 

MADEREVA 28 WATHIBITISHA KUSHIRIKI....

 
MBIO za magari ya Vaisakhi Rally, zinazotarajiwa kufanyika kuanzia Machi 23 hadi 24 mkoani Kilimanjaro, zimevutia madereva wa mbio hizo wapatao 28 kutoka katika mikoa ya Dar es salaam, Arusha Tanga na mwenyeji Kilimanjaro. 
Mbio hizo zinazofanyika kila mwaka na kuandaliwa Klabu ya magari ya mashindano, Kilimanjaro Motor Sports Club (KMSC), zitaanzia katika uwanja wa Sikh Club mjini Moshi na kuzinduliwa na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro ACP-Robert Boaz.
 
Kwa mujibu wa waandaaji hao wa mbio hizo, uwanja wa Sikh Union Club unatarajiwa kutumika kuanzishia mbio na kama kituo cha kumalizia mbio hizo. 

Madereva waliothibitisha kushiriki mbio hizo zilizoanza leo, Jumamosi ni pamoja na mshindi wa mwaka jana, Shafin Khan, bingwa wa taifa katika mbio za Rally kitaifa za mwaka jana, Dharam Panday, Shafin Khan / Moses Matovu (Evo 9) , Lali / TBA (N 12B), Gurjit Singh Dhani / TBA (N10 Pro drive) , Rajpal Singh Dhani / TBA (N10 Pro drive), Salvatory / Akram Hafidh (S/Impreza GC8), Victor Rogart / Sharook Aloo (S/legacy) na Kirit Pandya / Awadh bafadhil (S/Impreza GC8).

Wengine ni Binesh Haria / Viren Shah(S/Impreza GC8), Amarjit Dilon/TBA (N12), Tufail Amin / TBA (VW beetle), Fayaz chandu / TBA , Eric Cormack / Daudi Charles(Evo 4), Marco Fereira / Ratnaveer Darbar (S/Legacy), Gurpal Singh Sandhu / Manmeet singh Birdi (Evo10) , Gerrard Miller / Peter Fox (Evo 9), Louis Bonzon / Ahmed Hussein ( R/Rover V8), Shiraz Shabay / Ashraphe Ashraph (R/Rover V8), Jamil Khan / TBA (T/Land cruiser) , Harshil bhatt/Victor (S/Impreza GC8), Twalib / TBA (S/Impreza GC8), Manmohan Agarwal / TBA (S/Impreza GC8), Rizwan Haji / Shabir bandali
 

Wadhamini wake wakuu mbio za mwaka huu, ni kampuni ya Hari Singh & Sons Ltd na washirika wake, wadhamini wengine ni, Sunvic Express, Keys Hotels Travel & Tours, Maji Poa, Charan Singh & Sons, Yes Automotive Parts, Panone and Company Ltd, Tanzania Volunteers, Authentic Emergency Services Ltd, Snow View Hotel and Nanak Hauliers Ltd.

No comments:

Post a Comment