Sunday, March 24, 2013

MASANJA MKANDAMIZAJI, STARA THOMAS NA BAHATI BUKUKU KUPAMBAPA TAMASHA MAALU LA INJILI MJINI MOROGORO SIKUKUU YA PASAKA



KAMPUNI ya QS Mhonda J Entertainment imeandaa tamasha la muziki wa Injili liitwalo, Tumaini Jipya Gospel Concert, ambalo litafanyika katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro, Machi 31 mwaka 2013 ambayo itakuwa Siku Kuu ya Pasaka.
Dhumini kubwa la kuandaa tamasha hili ni kutaka kuwasaidia watu wenye mahitaji maalum kwenye jamii ikiwemo watoto yatima pamoja na wale wanaishi katika mazingira magumu, kutoa misaada kwenye hospitali pamoja na Makanisa yaliyopo mjini Morogoro.
Tumaini Jipya Gospel Concert limeanzia Morogoro lakini litaendelea kwenye mikoa mingine ya Tanzania Bara, kwa kipindi chote cha mwaka huu wa 2013 likiwa na lengo lile lile la kutoa tumaini kwa jamii.
Katika tamasha hilo  ambalo ni la aina yake kufanyika Tanzania litapambwa na Waimbaji wakubwa wa muziki wa Injili Afrika Mashariki ambao ni Bahati Bukuku, Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’, Joseph Nyuki, Stara Thomas, Matha Mwaipaja, Sifa John, Chamwenyewe na Revina Steven.
Mbali na waimbaji hao lakini zitakuwepo kwaya na vikundi mbalimbali vya muziki wa Injili Tanzania ikiwemo, Rafiki Gospel Singers, Haleluya Kwaya, Victoria Kwaya na MTC huku Masanja Makandamizaji akipewa jukumu la kuongoza shughuli hiyo (MC).
Sambamba na kutoa burudani ya mziki kupitia waimbaji tuliowataja lakini tutakuwa na muda maalum wa kutoa elimu ya Ujasiriamali kwa watu wote, pamoja na mbinu za kufaulu mtihani kwa wanafunzi.
Aidha katika tamasha la Tumaini Jipya tunatarajia kuwaweka pamoja watu zaidi ya elfu 30 kutoka katika viunga vyote vya mji wa Morogoro kwa lengo la kuwapa tumaini jipya.
Tunaamini kuwa hii ni fursa pekee kwa wakazi wa Morogoro kuweza kujumuika na watu wengine duniani katika kusherehekea siku kuu ya Pasaka kwa kufika kwao katika tamasha la Tumaini jipya ili kupata tumaini jipya.
Imeandaliwa na:-
QS Joseph Mhonda-Mkurugenzi Mtendaji wa QS Mhonda J Entertainment.

No comments:

Post a Comment