Tuesday, April 23, 2013

Benki ya Exim kusaidia vita ya kutokomeza malaria nchini



 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim Anthony Grant (kulia) akisalimiana na Laila Adam mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jangwani wakati wa warsha kuhusu ugonjwa wa malaria kwa Wanafunzi wenye Ulemavu iliyodhaminiwa na benki hiyo mwishoni mwa wiki. Picha na Mpiga Picha Wetu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim Anthony Grant (kulia) akisalimiana na Happy Tadeo mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jangwani wakati wa warsha kuhusu ugonjwa wa malaria kwa Wanafunzi wenye Ulemavu iliyodhaminiwa na benki hiyo mwishoni mwa wiki. 


Na Mwandishi Wetu

BENKI ya EXIM imeahidi kuendelea kusaidia kampeni mbali mbali zinazolenga kutokomeza ugonjwa wa malaria nchini ili kupunguza vifo vinavyotokana na ugonjwa huo nchini.


Akizungumza katika warsha kuhusu ugonjwa wa Malaria iliyoandaliwa kwa wanafunzi wenye  ulemavu mkoani Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim Anthony Grant alisema kuwa japokuwa dunia imepata mafanikio makubwa katika kutokomeza ugonjwa huo, bado ugonjwa huo ni tishio hasa kwa akina mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano huku akibainisha kuwa watu 660,000 upoteza maisha kila mwaka kutokana na ugonjwa huo.

Semina hiyo imefanyika siku chache kabla ya maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani itakaefanyika tarehe 25, April, 2013 na kaulimbiu ya Wekeza katika vizazi vijavyo, Shinda Malaria.

Grant aliwaasa watanzania kujenga utamaduni wa kufanya usafi katika makazi yao ilikupunguza uwezekano wa mbu kuzaliana na kuongezeka huku akiwasisitizia kutumia vyandarua kabla ya kulala.

“Ugonjwa wa malaria bado ni tishio hapa Tanzania na duniani kwa ujumla. Mpaka leo, watu 660 000 duniani upoteza maisha duniani wengi wao wakiwa akina mama wajawazito pamoja na watoto chini ya miaka mitano,” alisema Grant.

Grant alisema kuwa benki yake itaendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya kujikinga dhidi ya ugonjwa huo na kuzisihi taasisi mbali mbali kusaidia jitihada za kutokomeza ugonjwa huo.

Naye Laila Adams kutoka Shule ya Sekondari ya Jangwani wakati akisoma risala ya wanafunzi wenye ulemavu alisema kuwa watu wenye ulemavu bado wanachangamoto mbali mbali zakimaisha.

“Kwa mfano, licha ya Serikali kuandaa na kutekeleza mipango ya maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) na elimu ya sekondari (MMES) inayolenga kutoa fursa zaidi za elimu, idadi ya watoto wenye mahitaji maalum wanaopata fursa hizo bado ni ndogo ukilinganisha na vikundi vingine.

“ Kwa mfano wakati kiwango cha wanafunzi wanaoandikishwa katika elimu ya msingi kikiongezeka hadi asilimia 94 mwaka 2011 kutoka asilimia 78 mwaka 2000, watoto walemavu walieandikishwa kuanza elimu ya msingi ni chini ya asilimia moja,” alisema.

No comments:

Post a Comment