Friday, April 26, 2013

COASTAL UNION YAIPA UBIGWA YANGA BAADA YA KUTOKA SARE YA BAO 1-1 NA AZAM FC


 


Yanga imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu, kufuatia sare ya 1-1 katika mchezo wa ligi hiyo baina ya wenyeji Coastal Union na Azam FC ya Dar es Salaam, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga leo.

Matokeo hayo yanamaanisha, Azam FC waliokuwa washindani wakuu wa Yanga SC yenye pointi 56, hawawezi tena kufikisha pointi hizo ambazo wanazo mabingwa hao wapya, kwani hata wakishinda mechi zao nyingine  mbili zilizobaki, watamaliza na pointi 54.
Mchezaji aliyepeleka shangwe na vigelegele Jangwani leo ni Danny Lyanga, ambaye aliifungia Coastal bao la kusawazisha dakika ya 72.

Azam ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao katika mchezo wa leo, lililofungwa na beki Aggrey Morris kwa penalti dakika ya 60, baada ya mshambuliaji wa zamani wa Yanga SC, Gaudence Mwaikimba kuchezewa rafu kwenye eneo la hatari  na beki Yussuf Chuma- na refa Andrew Shamba wa Pwani akaamuru pigo hilo.

No comments:

Post a Comment