Wednesday, April 17, 2013

GRAND MALT YAZINDUA TUZO ZA “EXCEL WITH GRAND MALT 2013”.


Meneja wa Kinywaji cha Grandmalt Bi Consolata Adam kulia akiwa na afisa mahusianao wa TBL Bi Doris malulu wakizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar Es Salaam juu ya uzinduzi wa tuzo za wanafunzi wa vyuo vikuu nchini ambapo Tamasha la Kwanza litafanyika jumamosi  hii kwenye viwanja vya chuo kikuu Arthi na jumapili kwenye chuo kikuu cha Mkwawa mkoani Iringa.

Dar es Salaam, April 16, 2012
Kinywaji maarufu cha Grand Malt leo kimezindua tuzo kwa wanafunzi wa elimu ya juu zijulikanazo kama “Excel with Grand Malt”, huu ukiwa ni mwaka wa tatu kwa tuzo hizi kutolewa.
 
Akizungumzia tuzo hizo, meneja wa kinywaji cha Grand Malt Bi. Consolata Adam alisema; Excel with Grand Malt ni tuzo za aina yake ambazo zimelenga kutambua na kuthamini mchango wanaoonesha wanafunzi katika fani mbalimbali nje ya masomo ya darasani. Tunatambua kuwa kazi kubwa ya mwanafunzi anapokuwa chuoni ni kuhudhuria vipindi vya darasani na kupata elimu, bali tunapenda pia kuwatambua wale wachache ambao wanakwenda mbali zaidi na kufanya mambo ya maendeleo katika mazingira yao ya chuo.
 
Tuzo hizi zilianzishwa mwaka juzi ambapo tuliweza kufika katika mikoa sita na kufikia vyuo vipatavyo ishirini.  Kwa mwaka huu mchakato utaanza mwezi Aprili hadi June, na Mikoa itakayohusika ni pamoja na Dar es salaam, Morogoro, Iringa, Dodoma, Kilimanjaro na Mwanza ambapo vyuo vipatavyo 20 vitashiriki. Kama ilivyokuwa miaka iliyopita, fani zitakazoshindanishwa ni Ubunifu (Innovation), Michezo (sports), Utamaduni na burudani (Culture & Entertainment) na Mazingira na Huduma za jamii (Environment & social responsibilities). Kama ilivyo ada, washindi katika fani hizi watajipatia zawadi mbalimbali toka Grand Malt ikiwa ni pamoja na pesa za kununulia vitabu na vyeti vya ushindi.
 
Kwa sasa natangaza rasmi kuwa tunzo hizi zimezinduliwa rasmi na mkoa wa kwanza utakuwa ni hapa Dar Es Salaa ambapo tunatarajia kufanya tamasha kubwa kwenye viwanja vya chuo kikuu cha Chuo kikuu Artdhi siku ya jumamosi kisha jumapili tutafanya tamasha la ufunguzi kwenye Viwanja vya chuo cha Mkwawa mkoani Iringa na kutakuwa na burudani na zawadi nyingi na zaidi kutakuwa na GrandMalt baridi na hakutakuwa na kiingilio chochote. Alisema Bi. Consolata.
 
Akielezea umuhimu wa Tuzo hizo, meneja masoko wa TBL Bw. Fimbo Butallah alisema; Alisema tunafurahi sana kuona vyuo vyote vilipokea tuzo hizi kwa furaha kubwa, hii ni kwa sababu wanatambua umuhimu wake. 
Kupitia tuzo hizi ambazo zitakuwa zikitolewa kila mwaka, Grand Malt inatoa changamoto kwa vijana walio vyuoni kuona umuhimu wa kujituma na kufanya mambo mengi na makubwa zaidi ya kufaulu mitihani ya darasani tu. 
Tunaomba viongozi wa serikali za wanafunzi na viongozi wa vyuo kuendelea kutoa ushirikiano kama walivyofanya mwaka jana ili kuleta ufanisi zaidi katika tuzo za mwaka huu. Kama ilivyo kawaida, utaratibu utakuwa ule ule ambapo wanchuo watapendekeza majina ya vijana wanaoamini kuwa wamefanya mambo makubwa ndani ya vyuo vyao katika tasnia zilizotajwa hapo awali, kisha kufuatiwa na kipindi cha kupiga kura ambapo washindi watapatikana. Alimaliza Bw. Butallah.
 
Kwa upande wake Afisa uhusiano wa Tbl bi Doris Malulu Alisema GrandMalt kwa kuzingatia umuhimu wa juhudi za serikali katika kuhamasisha jamii kutunza mazingira kwa kupanda miti mwaka huu Grand Malt itafanya zoezi maalum kwenye kila chuo kwa kupanda miti imara itakayosaidia kutunza na kuboresha mazingira ya vyuo hivyo ili kuandaa mazingira bora ya kusomea ya wanafunzi wa sasa na wa vizazi vijavyo ambapo mkoani Iringa  zoezi hilo litafanyika jumatatu April 22,2013 katika vyuo vya Mkwawa,Ruaha na Tumain na Mkoani Dodoma zoezi hilo litafanyika kwenye vyuo vya UDOM na St Johns  siku ya jumatatu April 29,2013 asubuhi , kisho zoezi hilo litaendelea katika mikoa ya Morogoro,kilimanjaro,Mwanza na Dar Es Salaam.

No comments:

Post a Comment