Monday, April 8, 2013

MBUNGE WA CUF AHAMAMASISHA MIRADI MAENDELEO YA TANGA


Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Tanga Amina Mwidau (CUF), kiakabidhi mifuko ya saruji kwa viongozi wa Kata ya Kiomoni.

Na Mwandishi Wetu, Tanga

MBUNGE wa Viti maalum Mkoa wa Tanga, Amina Mwidau (CUF), awametaka wananchi wa mkoa wake kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo katika maeneo yao.

Kauli hiyo aliitoa kwa nyakati tofauti alipokuwa akizungumza katika ziara yake hiyo katika kata za halmashauri ya jiji la Tanga na Wilaya ya Pangani, ambapo alisema ni muhimu kwa kila mwanajamii kutambua wajibu wake.

“Suala la amaendeleo halina itikadi na sasa sio wakati wa kampeni za uchaguzi, ni jukumu letu kwa viongozi wa Mkoa wa Tanga, kuhakikisha tunashiriki katika miradi ya maendeleo kwa dhati.

“Ni wazi Mkoa wa Tanga tuna kila sababu ya kuhakikisha tunaimarisha uchumi wetu hasa baada ya miaka kadhaa viwanda vyake kufa kutokana na kutokuwepo na usimamizi mzuri. Ikiwa kila mtu atatambua wajibu wake ni wazi tutafanikiwa kufikia lengo letu,” alisema Mwidau.

 Alisema kutokana na hali hiyo kila mara amekuwa akishiriki katika kuhamasisha maendeleo katika maeneo yote ya mkoa huo bila kujali uongozi wa kaa upo chini ya chama cha CUF au CCM.

 “Tanga tuna ardhi nzuri na tuna kila sababu ya kujivunia jambo  hili ingawa kukosekana kwa usimamizi madhubuti kwetu imekuwa ni kilio kikubwa kwa wananchi wetu tunaowaongoza, wabunge wote wa mkoa huu tuna wajibu wa kuliangalia hili,” alisema Mbunge Mwidau.

Katika ziara hiyo akiwa wilayani Pangani Mwidau, alisema kuwa amefurahishwa kuona wananchi na viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Mwera kuamua kuchimba kisima kikubwa zaidi ya kilichopo sasa na katika hilo amefurahishwa kuona mchango wa awali wa mashine aliyoitoa imewezesha kujengwa kwa kisima kisima kingine kikubwa cha futi 45 na kipenyo cha nchi sita.

No comments:

Post a Comment