Monday, April 22, 2013

MCHEZO WA MASUMBWI ULIPO HAMASISHWA CHALINZE MKOA WA PWANI


Bondia Amos Thomas  kushoto akioneshana ufundi wa kutupiana makonde na Edrew Joseph wakati wa mpambano wa kuamasisha mchezo wa masumbwi Chalinze Mkoa wa pwani  Juzi mchezo huo ulitoka droo picha na www.superdboximgcoach.blogspot.com
Baazi ya mashabiki wakiwa na Diwani wao
Bondia Said Minyusi wa Chalinze kushoto akirusha konde ambalo alina madhala kwa Zumbe Kukwe wa Dar wakati wa mpambano wa kuamasisha masumbwi Chalinze mkoa wa Pwani juzi  Kukwe alishinda kwa TKO ya raundi ya kwanza picha na www.superdboximgcoach.blogspot.com
Baazi ya mashabiki waliojitokeza kuhamasisha mchezo wa masumbwi wakiangalia burudani hiyo
Mabondia walio itimisha mpambano huo wakati wa kuhamasisha masumbwi Chalinze
Diwani wa Kata ya Bwilingi Chalinze Ahmed Kalama Nassar akizungumza kabla ya mpambano wa mwisho kwa ajili ya kuhamasisha ngumi katika kata hiyo
Mwaite Juma wa Chalinze kushoto akimwangalia bondia Mussa Ali baada ya kupiga konde zito na kwenda chini
Na Mwandishi Wetu

ZAIDI ya mashabiki 300 wamejitokeza kuangalia mpambano wa Masumbwi kwa ajili ya kuhamasisha mchezo wa ngumi Chalinze  Mkoa wa Pwani pamoja na vitongoji vyake mashindano hayo ya masumbwi yaliyoandaliwa maalumu kuhamasisha mchezo uho katika vitongoji maarufu.

Uliwakutanisha mabondia wa Dar es salaam na Chalinze na mabondia wanaotamba katika kitongoji hicho mpambano huo wa masumbwi ulioanza saa tatu ya usiku na kumalizika saa nne na nusu uliwakutanisha bondia Amos Thomas aliye toka sare na Edrew Joseph uku mpambano mwingine ukiwakutanisha Zumbe Kukwe wa Dar es salaam aliye mgalagaza bila huruma Said Minyusi wa chalinze

Mpambano mwingine ni Alex Kado wa chalinze alishindwa kuhimili mikiki mikiki ya Nassoro Khatibu na kupigwa kwa ponti

Pambano lililokuwa likisubiliwa na watu wengi zaidi ni mpambano uliowakutanisha Mwaite Juma wa Chalinze na Mussa Ali ambapo mwaite aliweza kumsambalatisha ali kwa TKO ya raundi ya kwanza na kupeleka shwangwe kwa wapenzi waliojitokeza katika mpambano huo

Baada ya kumalizika kwa mpambano huo Diwani wa Kata ya Bwilingi Chalinze Ahmed Kalama Nassar ambaye alikuwa mgeni rasmi wa mpambano huo alisema yupo tayali kuwanunulia vifaa vya mchezo huo ili kuendeleza masumbwi katika kata hiyo

Ambapo ame haidi kuongeza ushirikiano wa wataalamu wa masumbwi kwa kushilikiana na viongozi ili chalinzi kiwe kitovu cha masumbwi nchini

No comments:

Post a Comment