Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) kuwaonesha wasanii Aprili 24. Star Light Hotel bule
Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA)
|
Peter Mwenda
|
PRESS RELEASE
SHIWATA imeandaa maonesho maalum kila mwezi ili kutoa nafasi
kwa wasanii wa fani ya mbalimbali pamoja na wanamichezo kuonesha vipaji vyao.
Wasanii wengi chipukizi wanakosa mahali pa kuonesha kazi
zao, mara nyingi kazi za wasanii wakubwa ndizo ambazo hurushwa katika redio na
luninga (TV).
SHIWATA imeamua kuandaa maonesho haya kwa malengo makuu
yafuatayo
(1) Kukuza
vipaji
(2) Kuwapatia
soko (underground) mahali ambapo wanaweza kuonesha vipaji vyao na kuwashawishi
mapromota mbalimbali kuwaajiri.
(3) Kuelimisha
jamii kuhusu matatizo mbalimbali kama maadili na magonjwa kama
UKIMWI,malaria.
(4) Kuimarisha
umoja kati ya wasanii na wanamichezo
SHIWATA inawataarifu viongozi
mbalimbali na makundi ya sanaa na Michezo pamoja na wasanii binafsi kutakua na
mkutano Siku ya Jumatano Aprili 17 mwaka huu saa 8 mchana katika ukumbi wa
Splendid,Bungoni Ilala kupanga ratiba na kupata taarifa zaidi.
Onyesho la Kwanza
litaoneshwa katika ukumbi wa Star Light Hotel, Mnazi Mmoja Dar es Salaam siku
ya Jumamosi Aprili 24.
Michezo itakayoneshwa ni pamoja
na maigizo, sarakasi, ngoma, kwaya, karate, Taekwondo, Taarab, Dansi, Bongo
Flava, Mavazi, Gospal na Kasida, mada kuu katika maonesho hayo ni Amani na Utulivu.
Hii ni nafasi ya pekee kwa
wasanii chipukizi (underground) kuonesha vipaji vyao.Watengenezaji wa
filamu, mapromota, wamiliki wa bendi, MaDj na wanunuzi wa mbalimbali wa kazi za
sanaa wanaalikwa ili waweze kuona vipaji na kununua kazi za wasanii hao
chipukizi.
Wanafunzi wenye vipaji kutoka
shule za msingi, Sekondari na vyuo mbalimbali wanaalikwa kuja kuonesha vipaji
vyao.
Mipango iliyofanywa ili maonesho
haya yarushwe live kituo kimojawapo cha televisheni.
Kutokuwa na chakula kwa wasanii
na zawadi mbalimbali zinazotolewa kwa wasanii watakaofanya vizuri katika kila
onesho.
Hii itakuwa nafasi nzuri kwa
wapenzi wa burudani ya sanaa kwani kwa muda mrefu walikuwa hawajui wapi
wanaweza kupata burudani kama hiyo kiingilio
kitakuwa bure.
Wote mnakaribishwa
Peter Mwenda 0715/0752- 222677
Ofisa Habari wa SHIWATA
No comments:
Post a Comment