Monday, April 29, 2013

NMB YAENDELEA KUBORESHA HUDUMA ZA KIBENKI KARIBU YAKO


 Wateja waBenkiya NMB wakipatamaelekezoyahudumaza JISEVIE kutokakwaOfisawa NMB tawi la NMB House  Edith Mavura.Hudumazitolewazokwawatejawa NMB waliojisajilikutumia NMB Mobile .Hudumainayomuwezeshamtejakupatahudumazakibenkimahalapopotebilakufikakwenyetawi la NMB
 Wateja wa Benkiya NMB wakipata maelekezo yanayohusu maboresho ya huduma ijulikanayo kama JISEVIE kutoka kwa Ofisa wa NMB tawi la Bank House, Salvatory Mushi .Jisevie inamsaidia mteja wa NMB kupata huduma za kibenki sehemu yoyote atakapokua bila kufika kwenye tawi la NMB.Mteja ataweza kutumia simu yake ya kiganjani na kutembelea Mashine za kutoa fedha ili Kujisevia.
 Ofisawa NMB tawi la Bank House, Salvatory Mushi akimwelekeza mteja wa NMB jinsi ya kujiungana NMB Mobile ili KUJISEVIA huduma zitolewazo kwa wateja wa NMB waliojisajili kutumia NMB Mobile .Huduma inayomuwezesha mteja kupata huduma za kibenki mahala popote bila kufika kwenye tawi la NMB

Ofisa wa  NMB tawi la Loliondo, Lembris Lesion akimwelekeza Mchungaji mstaafu, Ambelikile Mwaisapile jinsi ya kujiungana NMB Mobile ili KUJISEVIA huduma zitolewazo kwa wateja wa NMB waliojisajili kutumia NMB Mobile .Huduma inayomuwezesha mteja kupata huduma za kibenki mahala popote bila kufika kwenye tawi la NMB.

Na Mwandishi Wetu

NMB imeendelea kuboresha huduma zake kwa kuzindua bidhaa na huduma mbali mbali ili kuwawezesha wateja kupata huduma za kibenki kwa urahisi na unafuu zaidi.

Ili kukuwezesha kupata huduma za kibenki haraka na kwa wakati wowote, Benki ya NMB imeendelea kuelemisha wateja wake aina mbalimbali ya huduma za kibenki wanazoweza kuzipata bila ya kwenda katika tawi la NMB kupitia kampeni yake maalum iitwayo JISEVIE.

Huduma zilizojumuishwa katika mpango huu maalum wa Jisevie ni pamoja na Huduma ya NMB mobile, Huduma ya NMB PesaFasta, Huduma ya NMB ATM na huduma ya kuweka na kutoa fedha kupitia Vodacom Mpesa.

“ Mpango huu wa kuelemisha wateja juu ya huduma mbali mbali wanazoweza kuzipata bila ya kupitia benki, yaani Jisevie unalenga katika kuendelea kutoa huduma bora zaidi , kuvutia na za haraka zaidi wakati wowote mteja anapohitaji huduma za kibenki”, alisema bwana Arjan Molenkamp, Afisa Mkuu wa Biashara ya Wateja Binafsi.
Wateja ambao wataweza kutumia moja ya huduma hizi zilizoainishwa katika mpango huu wa Jisevie watapata faida mbalimbali ikiwemo; kutokutumia fedha taslimu kulipia huduma mbali mbali, kuweka au kutoa fedha mahali popote kwa kutumia huduma ya Vodacom Mpesa, Kutuma fedha kwa mtu yeyote asiye na akaunti wala kadi ya ATM ya NMB kwa kutumia NMB PesaFasta na kutohitaji kutembelea tawi lolote la benki ya NMB ili kuweka fedha kwenye akaunti yako.

Wateja wa NMB sasa wanaweza kupata huduma za kibenki popote walipo bila kutembelea tawi la NMB. Haya yote yametokana  NMB Jisavie ambayo itamwezesha mteja wa NMB  kuwa na  NMB Mobile,NMB Pesa Fasta ,POS,NMB ATM,Huduma ya kuweka na kutoa fedha  kutoka kwenye akaunti ya NMB kwenda M-Pesa na M-Pesa kwenda Akaunti ya NMB,Zaidi ya hayo yote NMB inalenga kumuwezesha Mteja wake aweze kujihudumia mwenyewe bila kufika kwenye tawi la NMB.

Faida nyingine anazoweza kupata Mteja wa NMB kwa kupitia mpango huu wa Jisevie ni pamoja na kuangalia salio la akaunti yako, kupata taarifa fupi ya matumizi ya akaunti yako, kununua Luku,Kulipa ankra ya Maji-DAWASCO, kulipia bili ya King’amuzi ya DStv, Kulipia kodi za Mapato na kununua muda wa hewani.

No comments:

Post a Comment