Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, April 8, 2013

Profesa Lipumba, alia na uchumi wa Tanga


Profesa Lipumba, akiangalia ukuta uliojengwa na wananchi wa Kijiji cha Kigombe mkoani Tanga, mara baada ya kuuzindiwa, kushoto ni Mwenyekiti wa Kijiji hicho Mzee Said.
Mwandishi Wetu, Tanga
MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amesema Mkoa wa Tanga ni moja kati ya mikoa maarufu kwa viwanda nchini lakini hivi saa hali ya kimaendeleo katika mkoa huo imekuwa mbaya.

Kauli hiyo ameitoa leo mjini hapa alipokuwa akiwasilisha mada inayohusu maendeleo ya uchumi kwa Mkoa wa Tanga katika kongamano lililoandaliwa na Chama cha Wananchi (CUF) kwa kushirikiana Taasisi ya Maendeleo ya demokrasi kwa vyama vya siasa ya nchini Denmark (DIPD).

Profesa Lipumba alisema kuwa  hakuna haki bila kuwa na maendeleo yanamgusa mwananchi wa kawaida.

Alisema Mkoa wa Tanga imefanikiwa kuwa na rasimali nyingi ikiwemo zao la Mkonge ambalo kwa sasa limekosa msukomo hali inayochangia umaskini kwa wananchi wa mkoa huo.

"Pamoja na Tanga kuwa na fursa nyingi za kiuchumi lakini bado kadri siku zinavyokwenda umaskini umekuwa ukiwatesa wananchi. Viwanda vilikuwa zaidi ya 70 lakini sasa hakuna hata kimoja kinachofanya kazi huku zao la mkonge lilikosa msukumo wa makusudi kwa wananchi wake.

"Katika soko la dunia inaonyesha kuwa Tanga ilikuwa ikizalisha tani 234,000 kwa mwaka lakini sasa mkonge umeporomoka na kufikia tani 25,000 tu hali ambayo imekuwa ikiongeza umaskini kila kukicha. Kama kungekuwa na msukumo wa makusudi wa kufufu zao hili ni wazi Tanga ingekuwa imepaa kimaendelo kwa wananchi wake kutokana na kuwa na kila aina ya rasilimali zikiwemo za matunda na mbogamboga," alisema Profesa Lipumba.
Profesa Lipumba, ambaye ni mtaalamu wa masuala ya uchumi duniani, alisema ili kuweza kufikia malengo ya mkoa huo kuweza kupambana na umaskini ni lazima serikali ikubali kwa kufanya uwekezaji hasa katika kufungua bandari ya Tanga ambayo ni lango kuu la kiuchumi.

Alisema Bandari ya Tanga imekuwa haitumiki ipasavyo hali inawechangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa umaskini na hazorotesha harakati za mkoa na wananchi kwa ujumla.

"Bandari ya Tanga, zao la mkonge pamoja na kukosekana kwa msukumo wa kuimarisha sekta ya elimu ni moja ya masuala yanayoufanya mkoa huu kuzidi kurudi nyuma kiuchumi pamoja na wananchi wake,” alisema Profesa Lipumba

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...