Mkuu wa Jeshi la Magereza
nchini, Kamishna Jenerali John Minja (kushoto) akisalimiana na Jaji Mfawidhi wa
Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Aisha Nyerere baada ya kutoa hotuba ya
uzinduzi wa mabasi manne na gari ndogo moja (pick-up) kwa ajili ya kuwasafirishia
mahabusu toka gerezani kwenda mahakamani na kurudi gerezani kwa mkoa
wa Arusha. Uzinduzi huo ulifanyika katika Gereza Kuu Arusha.
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali
John Minja, akikata utepe kuzindua rasmi jukumu la kuwasafirisha Mahabusu
kutoka Gerezani kwenda Mahakamani na kurudi Gerezani kwa Mkoa wa Arusha.
Katikati ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Aisha Nyerere
akipongeza uzinduzi huo. Uzinduzi huo ulifanyika katika Gereza Kuu Arusha.
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali
John Minja akitoa hotuba yake kabla ya kuzindua mabasi manne na gari
ndogo moja (pick-up) kwa ajili ya kuwasafirishia mahabusu toka gerezani
kwenda mahakamani na kurudi gerezani kwa Mkoa wa Arusha. Katika hotuba
yake mkuu wa jeshi hilo aliwataka maofisa magereza wa mkoa huo wawe
makini kuyatunza magari hayo. Uzinduzi huo ulifanyika katika Gereza
Kuu Arusha.
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali
John Minja, akiwa ndani ya moja ya mabasi yaliyozinduliwa kuashiria
uzinduzi wa kuwasafirishia Mahabusu kutoka Gerezani kwenda Mahakamani
na kurudi Gerezani kwa Mkoa wa Arusha. Uzinduzi huo ulifanyika katika
Gereza Kuu Arusha.
Sehemu ya magari matano ya kuwasafirisha Mahabusu
yaliyozinduliwa na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali
John Minja, katika hafla iliyofanyika Gereza Kuu la Arusha.
PICHA ZOTE
NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA
YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.
No comments:
Post a Comment