Floyd Mayweather Jr. (44-0, 26 KO’s) VS Saul “Canelo” Alvarez (42-0-1, 30 KO’s) step foot inside the ring on September 14th at the MGM Grand in Las Vegas, Nevada |
Thursday, May 30, 2013
Fainali ya Pool kufanyika Leaders Club, 'Safari Lager Higher Learning Competition 2013'
Meneja wa Bia ya Safari, Oscar Shelukindo akifafanua jambo kuhusu fainali za Pool
Lwiza Mbutu akizungumza na waandishi wa habari.
Mchezaji wa Single wa Chuo cha CBE, Liliani Meori
Katibu wa Chama cha Pool Taifa (TAPA), Amos Kafwinga akizungumza wakati wa mkutano huo.
Kiongozi
wa bendi ya Twanga Pepeta, Lwiza Mbutu akionesha manjonjo yake wakati
wa mkutano na waandishi wa habari leo. Kushoto ni Rapa wa bendi hiyo,
Jumainn Said.
Na Mwandishi Wetu
BENDI
ya Muziki wa Dansi ya Twanga Pepeta, inatarajia kupamba fainali za Michuano ya
mchezo wa Pool ngazi ya Taifa yajulikanayo kama
'Safari Lager Higher Learning Competition 2013'.
Fainali
hizo zinatarajiwa kupigwa katika viwanja vya Leders kuanzia kesho mpaka
Jumapili ambapo anatarajiwa kupatikana bingwa wa michuano hiyo iliyoanza
kutimua vumbi Mei 5 mwaka huu.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Meneja wa Bia ya Safari Lager
ambao ni wadhamini wakuu wa shindano hilo, Oscar Shelukindo alisema, wameamua
kuichukua bendi ya Twanga ili kutoa burudani wakati wa fainali hiyo ambayo pia
itapabwa na nyama choma kutoka katika bar tano zilizoshinda katika shindano la
nyama choma mwaka huu.
Shelukindo
alisema, bingwa katika shindano hilo
atajinyakulia kitita cha sh mil 2.5 pamoja na kombe huku zawadi nyingine
zikitolewa kwa mshindi wa pili na mchezaji mmoja mmoja na kudai kuwa, timu nane
zitachuano ambao ni mabingwa wa kila Mkoa.
Nae
Kiongozi wa bendi ya Twanga Luiza Mbutu alisema, wamejipanga kufanya burudani
kali ikiwa ni pamoja na kuwatambulisha wapenzi na mashabiki wao nyimbo mpya na
kuwataka kuja kwa wingi kwani hakuna kiingilio.
Katika
fainali hizo bingwa mtetezi ni chuo cha Sauti Mwanza ambacho pia kimefanikiwa
kuingia katika kinyanyang’anyiro hicho mwaka huu.
Ashanti United haina mpango na 'Mafaza
'
Kikosi cha Ashanti kilichopanda Ligi Kuu |
KLABU ya soka ya Ashanti United iliyorejea tena kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, imeweka bayana kuwa itafanya usajili wake kwa wachezaji vijana wenye uwezo kisoka badala ya kuwakimbilia 'mafaza' wakiwa na lengo la kutaka kuendelea kuzionyesha mfano klabu nyingine umuhimu wa kuzalisha 'jeshi' lao wenyewe.
Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mbaraka Hassani aliiambia MICHARAZO kwenye mazoezi ya timu hiyo uwanja wa Msimbazi, kwamba hawatawapapatikia mafaza kwa kuhofia kuja kujichanganya mbele ya safari ilihali wamejiwekea mikakati ya kutotaka kurudi walipotoka ambapo walisota kabla ya kurudia Ligi Kuu.
Mbaraka ambaye ndiye aliyeipandisha mwaka 2004 kabla ya kuzama msimu wa 2007-2008, alisema kutoa nafasi kwa vijana kutasaidia kuwatangaza wachezaji hao kama walivyofanya miaka ya nyuma na kuwaibua mastaa kadhaa wanaotamba hivi sasa katika soka la Tanzania.
Baadhi ya nyotga hao ni pamoja na kipa wa kutumainiwa wa Yanga, Ally Mustafa Barthez, Jabir Aziz, Juma Jabu, Mohammed Kijuso, Juma Nyosso, Deo Ngassa na wengineo.
"Hatujaanza rasmi kufanya usajili, lakini tukianza tutajikita kwa vijana zaidi kwa lengo la kuwapa nao nafasi ya kuonwa, si unajua Ashanti ni kama chuo kazi yetu kuzalisha wengine wachukue ndivyo tutakavyofanya hata safari hii kwa vile tumepania kuonyesha mfano kwa klabu nyingine," alisema Mbaraka.
Mbaraka, alisema anaamini kuwapa nafasi vijana kunasaidia kukuza soka la Tanzania kuliko kuendelea sera ya kung'ang'ania wachezajki wenye majina ambao mara nyinbgi usumbua hasa kwenye suala la masilahi ikizingatiwa klabu yao haina wafadhili zaidi ya wanachama na wadau wake kuchangishana fedha kuiendesha.
Ashanti imerejea ligi kuu msimu ujao pamoja na klabu za Rhino Rangers ya Tabora na Mbeya City na wanaendelea kupima wachezaji kwa ajili ya kupata itakaowasajili.
KASEBA APANIA KUMKALISHA MMALAWI
BONDIA wa ngumi za
mateke ‘Kick Boxer’ Japhet Kaseba amesema amejipanga kuweka rekodi nzuri katika
tasnia hiyo kwa kumchapa Mmalawi, Rasco Chimwanza katika pambano lao la kuwania
ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati linalotarajiwa kuchezwa Juni 8, mwaka huu.
Akizngumza na Habari Mseto jijini Dar
es Salaam, Kaseba alisema anajua kama bondia huyo ni nyota katika tasnia
hiyo, lakini kutokana na maandalizi aliyoyapata atahakikisha anaweka heshima
katika ngumi za mateke.
“Namshukuru mungu nina afya nzuri hadi
sasa na naendelea na mazoezi kwajili ya pambano hilo naomba Watanzania
wajitokeze kwa wingi katika ukumbi huo wa DDC Magomeni,” alisema Kaseba.
Naye Katibu Mkuu wa Oganizasheni ya
ngumi ya za kulipwa Tanzania (TPBO), Ibrahim Kamwe alisema maandalizi ya
pambano hilo yamekamilika, na tayari wamemtumia nauli Mmalawi huyo na kwamba
anategemea kuingia nchini Juni 5.
Nae kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila ‘Super D’ ametoa DVD mpya 3 kwa ajili ya mafunzo ya mchezo wa ngumi ndani yake kukiwa na clips za mabondia wanaofanya vizuri Tanzania kama Thomas Mashali vs Fransic Cheka na mambondia wengine mbalimbali
CD hizo zilizotengenezwa kwa umakini wa
ali ya juu ambazo zitakuwa chachu kwa ajili ya kuvutia wapenzi na
mashabiki mbalimbali kujua mchezo wa masumbi wakiwa wanangalia live mana
DVD hizo zina maelekezo ya sheria mbalimbali ambazo zinatumika katika
masumbwi
DVD hizo kwa sasa zinapatikana katika
makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi au unaweza kuzipata jengo la
Azam lililopo mtaa wa Msimbazi karibu na kituo cha Polisi Post Gelezani
kwingine ni GYM ya Amana iliyopo Ilala au unaweza kuwasiliana na kocha
kwa simu 0713406938 ili uweze kupata DVD hizo kwa ajili ya kujifunza
zaidi mchezo huo
Mbali ya kupatikana katika maeneo hayo pia
katika mchezo mbalimbali ya masumbwi kutakuwa na CD na DVD za mafunzo wa mchezo
huo zenye mapambano makubwa ya mabondia wa ndani na nje ya nchi.
Aliongeza kuwa baadhi ya mapambano yaliyomo katika CD na DVD
hizo ni ya Kalama Nyilawila
,Japhert Kaseba,Rashidi Matumla, Hassani Matumla,Thomas Mashali Dhidi ya
Francis Cheka, Mbwana Matumla na
Francis Miyeyusho,Japhert Kaseba na Maneno Oswald, Said Mundi na King Class Mawe.
mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywether,
Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali
na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya
juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super
D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa
ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
“Ninatarajia kuwepo kwa ajili ya kuwauzia DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika Mpambano ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi”, alisema Super D .
--
Super D Boxing Coach
Email.superdboxingcoach@gmail.com
www.burudan.blogspot.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mob;+255787 406938
+255774406938
Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania
MTOTO RAMLA ADAM ASHEREKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA
MTOTO RAMLA ADAM |
MTOTO RAMLA ADAM kushoto akilishana keke na Zainabu Mhamila 'Ikota' wakati wa siku yake ya kuzaliwa kwake iliyofanyika nyumban kwao Buguruni ramla alitimiza miaka sita katika siku yake hiyo |
Mtoto Ramla Adam kulia akiwa katika picha ya pamoja na mama yake mzazi na Zainabu Mhamila 'Ikota' |
Wednesday, May 29, 2013
BEN PAUL KUWASINDIKIZA MISS UN-COLLEGE TEMEKE
MSANII wa muziki wa kizazi
kipya, Bernard Paul ‘Ben Paul’, anatarajiwa kuwasindikiza warembo wa
kinyang’anyiro cha Redd’s Miss Uni-college Temeke kitakachofanyika kesho katika
ukumbi wa Club Bilicanas, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa
habari Dar es Salaam jana, mratibu wa shindano hilo, Florence Josephat,
alisema kuwa maandalizi yote yamekamilika na kwamba kilichobaki ni shoo yenyewe
ambayo alitamba itakuwa katika ubora wa hali ya juu.
Alisema kuwa jumla ya warembo
13 wanatarajia kupanda jukwaani siku hiyo, ikiwa ni baada ya kunolewa vilivyo
kwa takribani wiki tatu na kwamba wameiva kuwapagawisha watakaofika kushuhudia
uhondo huo.
“Maandalizi yote yamekamilika
hivyo tunawaomba wapenzi wa burudani na urembo kwa ujumla kujitokeza kwa wingi
siku hiyo kwani kipenzi cha warembo, Ben Paul, atatoa burudani ya hali ya juu
itakayoambatana na shoo kutoka kwa warembo wetu kutoka vyuo vitano vilivyopo Temeke,”
alisema.
Alivitaja baadhi ya vyuo
hivyo kuwa ni Chuo Kikuu cha Uganda, TIA, Chuo cha Bandari, DUCE na Chuo cha
Utalii, huku akitamba kuwa kutokana na ubora wa warembo walionao, wana imani
mwaka huu Redd’s Miss Tanzania atatoka katika kitongoji chao hicho.
Florence ambaye alikuwa mshiriki wa fainali za Miss Tanzania
2008, aliwataka wapenzi wa urembo na burudani, hasa wanafunzi wa sekondari na
vyuo, kujitokeza kwa wingi siku ya shoo yao
ili kujionea warembo bomba, huku wakipata burudani ya aina yake.
Alitaja kiingilio cha shoo yao kuwa ni Sh 10,000 na
kwamba mbali ya kinywaji cha Redd’s ambao ndio wadhamini wakuu wa mashindano
hayo, wadhamini wengine ni Shome Decoration & Catering,
djfetty.blogspot.com na Lamada Hotel.
Odama aisambaza ‘Whitch Doctor’
Na Elizabeth John
MWANADADA ambaye anafanya vizuri
katika tasnia ya filamu nchini, Odama amesambaza filamu yake mpya inayokwenda
kwa jina la ‘Whitch Doctor’.
Akizungumza Dar es Salaam,
nyota huyo alisema filamu hiyo ameisambaza hivi karibuni anaomba wadau wa kazio
zake wakae mkao wa kula kwaajili ya kupokea vitu vizuri kutoka kwake.
“Namshuku mungu asilimia kubwa ya
kazi zangu zinapokelewa vizuri na mashabiki wangu hivyo ninaimani hata kazi hii
itapokelewa vizuri kutokana na ubora uliopo ndani yake,” alisema Odama.
MISS SINZA/ MISS TANZANIA 2012-2013 BRIGIT ALFRED AWAFUNDA WAREMBO WA REDD'S MISS SINZA 2013
Miss
Sinza na Miss Tanzania 2012-2013, Brigit Alfred (kulia) akizungumza na
Warembo wanaotarajia kuwania Taji la Redd's Miss Sinza 2013, wakati
alipowatembelea katika Kambi yao ya mazoezi jana katika Ukumbi wa Meeda
Sinza na kuwafunda kuhusu mashindano hayo kuelekea shindano hilo
linalotarajia kufanyika Juni 7 mwaka huu kwenye Ukumbi huo. Katika
shindano hilo Viingilio vitakuwa ni Sh. 20,000 kwa VIP na viti vya
kawaida ni Sh. 10,000. Shindano hilo limedhaminiwa na Mtandao wa
www.sufianimafoto.com, kinywaji cha Dodoma Wine, Chilly Willy Energy
Drink, Clouds Media Group, CXC Africa, Saluti5 na Fredito Entertainment.
Miss
Sinza na Miss Tanzania 2012-2013, Brigit Alfred (katikati) akipozi na
warembo wanaowania Taji la Redd's Miss Sinza 2013, wakati
alipowatembelea kwenye Kambi yao ya mazoezi katika Ukumbi wa Meeda
Sinza.
Miss
Sinza na Miss Tanzania 2012-2013, Brigit Alfred (katikati) akipozi na
warembo wanaowania Taji la Redd's Miss Sinza 2013, wakati
alipowatembelea kwenye Kambi yao ya mazoezi katika Ukumbi wa Meeda
Sinza. Picha zote na www.sufianimafoto.com
The Finest’ ya Mwana FA yapisha msiba wa Ngwea
Na Elizabeth John
MKALI wa muziki wa bongo fleva
nchini, Mwana FA amesema ameahirisha kufanya shoo yake ambayo inajulikana kwa
jina la ‘The finest’ ambayo ilitakiwa kufanyika leo, ili kuupisha msiba wa
msanii wa hip hop nchini, Albert Mangwea uliotokea Mei 28 mwaka huu.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mwana FA alisema ameamua kufanya hivyo kutokana na umuhimu wa msanii huyo
katika tasnia ya muziki wa hip hop nchini.
Mbali na Mwana FA, wasanii wengine
ambao wamesogeza mbele na kuhairisha kufanya shoo zao ni pamoja na Lady Jay
Dee, Izzo Business, Joeh Makini na Kalapina.
SUPER NYAMWELA AKAMILISHANYIMBO YAKE MPYA YA DUVELLEE DUVELLEE LA POP BONGO
MNENGUAJI
Mahiri wa muziki wa dansi nchini, anayeshambulia na bendi ya Extra
Bongo, Super Nyamwela, amekamilisha Song lake jipya linalokwenda kwa
jina la Dullee Duvellee, linalopigwa katika mtindo wa Bongo Pop.
Akizungumza
na mtandao huu wa www.sufianimafoto.com, Nyamwela, amesema kuwa Wimbo
huo aliourekodia katika Studio za C91, zilizopo Kinondoni,
amemshirikisha Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Muki kutoka katika
Kundi la Makomandoo lililo chini ya THT.
Aidha
alisema kuwa Msanii huyo aliyemshiriki ni yule anayetamba na Song lake
kali ya Staili ya Kibega, ambao kwa pamoja katika wimbo huo wemefanya
kazi ya kueleweka na inayomvutia kila mmoja atakayepata bahati ya
kuusikiliza wimbo huo.
''Hivi
sasa najipanga kuzindua staili yangu mpya ya Bongo Pop, inayokwenda na
'Swaga za Duvellee Duvellee' ambyo kwa maana halisi ya kiswahili cha
Kitaa ni Shwari Shwari, na tayari wimbo huu nimeshausambaza katika Vituo
mbalimbali vya Redio nchini na baadhi wameshaanza kuutendea haki kwa
kuupiga na kuwapa raha wasikilizaji''. alisema Nyamwela
Pia Nyamwela amesema kuwa yupa katika maandalizi ya kurekodi Video ya Wimbo huo mwishoni mwa wiki hii katika Studio mpya za THT.http://www.sufianimafoto.com/
MASHINDANO YA CHESS KUTIMUA VUMBI JUNI 14-6
Mkurugenzi wa Spicenet Tanzania, Viney Choundary akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu mashindano
ya wazi ya kimataifa yajulikanayo kama ‘Spicenet Tanzania Open Chess
Championship 2013’ yanayotarajiwa kutimua vumbi juni 14-16 katika ukumbi wa Meru uliopo katika jengo la Golden Jubilee Tower mtaa wa Ohio jijini Dar es Salaam. Kulia ni Emmanuel Mwaisumbe na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha mchezo wa Chess, Joe Anea.
Emmanuel Mwaisumbe akifafanua jambo.
Na Elizabeth John
CHAMA cha Mchezo wa Chess nchini, kimeandaa
mashindano ya wazi ya kimataifa yajulikanayo kama ‘Spicenet Tanzania Open Chess
Championship 2013’ ambayo yanatarajia kuanza kutimua vumbi Juni 14 hadi 16
katika ukumbi wa Meru uliopo katika jengo la Golden Jubilee Tower mtaa wa Ohio
jijini Dar es Salaam
Katika kunogesha mashindano hayo ambayo yataweka
rekodi Afrika Mashariki, yatashirikishwa na bingwa ambaye alikua ni mchezaji
namba tatu duniani mwaka 1990, Nigel Short.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Chess, Joe Anea alisema mashindano hayo
yatahusisha wachezaji kutoka Tanzania, Zambia, Uganda na Kenya na kwamba
yanatarajiwa kuhudhulia na jumla ya wachezaji 80, huku wachezaji 50 wakitoka
Tanzania na 30 kutoka nchi za jirani.
Alisema kuwa mshindi wa kwanza atajinyakulia sh.
1,000,000, sh.500,000 kwa mshindi wa pili, sh. 300,000 kwa mshindi wa tatu, sh.
100,000 kwa mshindi wa nne na tano.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa kampuni ya
Spicenet, ambayo ndio wadhamini wa mchezo huo, Vinay Choudary alisema wameamua
kuungabnisha nguvu na chama cha Chess kuufufua mchezo huo Tanzania katika
jitihada za kuhakikisha nchi yetu inang’ara katika medani ya michezo katika
mashindano ya kimataifa.
“Nia yetu ni kukisaidia chama hiki kuhakikisha
mchezo huo unatangazwa na hatimaye kutambulishwa kwa watu wengi kupitia shule,
taasisi, vyuo vikuu na njia nyingine,” alisema.
Naye Ofisa Michezo wa Baraza la Michezo la Taifa
(BMT), Benson Chacha aliupongeza uongozi wa Chess pamoja na wadhamini wake kwa
kuamua kuurudisha mchezo huo ambao ulisajiliwa na BMT mwaka 1984.
“Sisi kama Baraza tutausaidia mchezo huu kupata
vitambulisho mbalimbali vya kushiriki mashindano ya mchezo huu, pia tunaomba
wadau wajitokeze kudhamini kwa lengo la kukuza michezo nchini,” alisema.
Familia ya Ngwair watoa taarifa ya mazishi na jinsi mwili utakavyoletwa Bongo
Ngwair enzi za uhai wake |
BABA
Mdogo wa 'Membaz' wa kundi la Chember Squad, Albert Mangwea 'Ngwair', Mzee Mangweha ambaye yuko Mbinga Songea kikazi,
amesema kuwa wamekubaliana na kaka yake mkubwa yaani baba mkubwa wa
Ngwair, David Mangweha ambaye naye yuko Songea kuwa watu watakutanika
Mbezi kwa msiba na pia mapokezi yatafanyika hapa Dar es salaam Mbezi
Beach.
Baba
huyo mdogo alisema kuwa kesho ndo watarudi Dar es Salaam pamoja na
kaka yake yaani baba mkubwa wa marehemu.
Kuhusu mwili kuletwa hapa
Tanzania kutoka Afrika Kusini baba mdogo amesema kuwa mpaka sasa
hawajajua jinsi gani mwili huo utafika hapa lakini kuna ndugu zao ambao
tayari washaanza kufanya taratibu za kuwasiliana na ubalozi wa Afrika
Kusini ili kujua ni jinsi gani mwili huo utafika hapa.
Kama kutakuwa na mabadiliko yeyote watakapowasili kesho baba mdogo na baba mkubwa baada ya kikao cha familia watatoa taarifa.
Lakini asuibuhi mmoja wa ndugu wa marehemu kutoka mkoa wa Mara alisema kuwa mwili wa msanii huyo aliyekuwa mkali wa Hip hop utakapowasili nchini utazikwa mjini Morogoro ambapo tayari kuna msiba umewekwa na mama yake.
Ndugu huyo alikuwa akihojiwa moja kwa moja na kituo kimoja cha redio na kusema wana ndugu wamekubaliana Ngwair akazikwe Morogoro alipohifadhiwa baba yake.
Lakini asuibuhi mmoja wa ndugu wa marehemu kutoka mkoa wa Mara alisema kuwa mwili wa msanii huyo aliyekuwa mkali wa Hip hop utakapowasili nchini utazikwa mjini Morogoro ambapo tayari kuna msiba umewekwa na mama yake.
Ndugu huyo alikuwa akihojiwa moja kwa moja na kituo kimoja cha redio na kusema wana ndugu wamekubaliana Ngwair akazikwe Morogoro alipohifadhiwa baba yake.
Ngwair, aliyefahamika baada ya kutoa
kibao cha Ghetto Langu mwaka 2003 kabla ya kupakua albamu ya Mimi na
kisha kufuatiwa na Nge, alifariki jana nchini Afrika Kusini kwa kile
kilichoelezwa kujidunga dawa za kulevya, ingawa bado haijathibitishwa
kidaktari alipoenda kufanya shoo na msanii mwenzake M2P.
WASIFU WA MAREHEMU NGWAIR
MAREHEMU Albert Kenneth Mangwea alizaliwa Novemba 16, 1982 mjini Mbeya akiwa ni mtoto wa mwisho kati ya watoto 10 wa baba yake na wa sita kwa mama.
Kiasili Ngwair alikuwa mwenyeji wa mkoa wa Ruvuma kabila la Kingoni, ingawa amekuwa mjini Morogoro na mkoa wa Dodoma.
Shule ya Msingi aliisoma Shule ya Bungo mjini Morogoro alikohamia akiwa na miaka mitano kabla ya kuhamia Dodoma kulamizia darasa la saba toka la tano alilohama nalo Shule ya Mlimwa.
Sekondari aliisoma Mazengo Sec kabla ya kuendelea Chuo cha Ufundi cha Mazengo pia mjini Dodoma alipoanza kujihusisha na muziki kabla ya kutua kundi la Chamber Squad lililoundwa na Jafarah, Jay Mo, Noorah, Mez B, Mchizi Mox na Dark Master.
Amewahi kunyakua tuzo ya Kili Music Award kupitia kipengele cha muziki bora wa Hiphop, huku nyimbo kadhaa zilimtambulisha vyema kwa mashabiki baadhi ikiwa ni Ghetto Langu, Mikasi na nyingine za kushirikishwa na wasanii mbalimbali.
Katika maisha yake ya muziki aliwahi kutoa albamu mbili za Mimi ya mwaka 2005 na Nge ya mwaka juzi ambayo hata hivyo haikufanya vyema sokoni kama ile ya awali.
WASIFU WA MAREHEMU NGWAIR
MAREHEMU Albert Kenneth Mangwea alizaliwa Novemba 16, 1982 mjini Mbeya akiwa ni mtoto wa mwisho kati ya watoto 10 wa baba yake na wa sita kwa mama.
Kiasili Ngwair alikuwa mwenyeji wa mkoa wa Ruvuma kabila la Kingoni, ingawa amekuwa mjini Morogoro na mkoa wa Dodoma.
Shule ya Msingi aliisoma Shule ya Bungo mjini Morogoro alikohamia akiwa na miaka mitano kabla ya kuhamia Dodoma kulamizia darasa la saba toka la tano alilohama nalo Shule ya Mlimwa.
Sekondari aliisoma Mazengo Sec kabla ya kuendelea Chuo cha Ufundi cha Mazengo pia mjini Dodoma alipoanza kujihusisha na muziki kabla ya kutua kundi la Chamber Squad lililoundwa na Jafarah, Jay Mo, Noorah, Mez B, Mchizi Mox na Dark Master.
Amewahi kunyakua tuzo ya Kili Music Award kupitia kipengele cha muziki bora wa Hiphop, huku nyimbo kadhaa zilimtambulisha vyema kwa mashabiki baadhi ikiwa ni Ghetto Langu, Mikasi na nyingine za kushirikishwa na wasanii mbalimbali.
Katika maisha yake ya muziki aliwahi kutoa albamu mbili za Mimi ya mwaka 2005 na Nge ya mwaka juzi ambayo hata hivyo haikufanya vyema sokoni kama ile ya awali.
Monday, May 27, 2013
KING CLASS MAWE KUPAMBANA NA BAUNSA JUNI 16 PANANDI PANANDI ILALA
KING CLASS MAWE |
Patrick Kavako'Baunsa' |
Mpambano
huo ulioratibiwa na Kinyogoli Fondition kwa kushlikiana na PST itakuwa
chachu kwa vijana kuendelea kuupenda na kuucheza mchezo huo unaopendwa
na wengi nchini
mbali
ya mpambano uho kutakuwa na mapambano mengine ya kukata na shoka bondia
Abuu Mtambwe ataoneshana umwamba na Kassim Gamboo na Bondia mkongwe
kabisa Yohana Robart atamenyana na Mussa Sunga
Kocha huyo wa kimataifa wa mchezo wa ngumi nchini,Rajabu
Mhamila ‘Super
D’ ametoa DVD mpya 3 kwa ajili ya mafunzo ya mchezo wa ngumi ndani yake
kukiwa na clips za mabondia wanaofanya vizuri Tanzania kama Thomas
Mashali vs Fransic Cheka na mambondia wengine mbalimbali
CD hizo zilizotengenezwa kwa umakini wa
ali ya juu ambazo zitakuwa chachu kwa ajili ya kuvutia wapenzi na
mashabiki mbalimbali kujua mchezo wa masumbi wakiwa wanangalia live mana
DVD hizo zina maelekezo ya sheria mbalimbali ambazo zinatumika katika
masumbwi
DVD hizo kwa sasa zinapatikana katika
makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi au unaweza kuzipata jengo la
Azam lililopo mtaa wa Msimbazi karibu na kituo cha Polisi Post Gelezani
kwingine ni GYM ya Amana iliyopo Ilala au unaweza kuwasiliana na kocha
kwa simu 0713406938 ili uweze kupata DVD hizo kwa ajili ya kujifunza
zaidi mchezo huo
Mbali ya kupatikana katika maeneo hayo pia
katika mchezo mbalimbali ya masumbwi kutakuwa na CD na DVD za mafunzo wa mchezo
huo zenye mapambano makubwa ya mabondia wa ndani na nje ya nchi.
Aliongeza kuwa baadhi ya mapambano yaliyomo katika CD na DVD
hizo ni ya Kalama Nyilawila
,Japhert Kaseba,Rashidi Matumla, Hassani Matumla,Thomas Mashali Dhidi ya
Francis Cheka, Mbwana Matumla na
Francis Miyeyusho,Japhert Kaseba na Maneno Oswald, Said Mundi na King Class Mawe.
mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywether,
Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali
na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya
juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super
D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa
ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
“Ninatarajia kuwepo kwa ajili ya kuwauzia DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika Mpambano ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi”, alisema Super D .
--
Super D Boxing Coach
Email.superdboxingcoach@gmail.com
www.burudan.blogspot.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mob;+255787 406938
+255774406938
Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania
Zantel yazindua Epiq Open Mic
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya Diamond na Ney wa Mitego wakitumbuiza jukwaani kwenye uzinduzi wa tamasha la Epiq Open Mic
======= ====== ========
Katika kuelekea msimu wa sita wa
shindano la kuimba la Epiq Bongo Star Search, kampuni ya simu za
mikononi ya Zantel leo imezindua Epiq Open Mic ikiwa ni nafasi nyingine
kwa vijana wenye vipaji vya muziki kuonyesha vipaji vyao kabla usaili
wa Epiq Bongo Star Serach haujaanza.
Epiq Open Mic inatarajiwa
kuwapa nafasi vijana kujifunza misingi ya muziki kutoka kwa mmoja
wa watayarishaji wa muziki maarufu zaidi nchini, Marco Chali. Marco
Chali ambaye pia ni mtunzi na mwimbaji, ametayarisha nyimbo
nyngi ambazo zimeshinda tuzo ndani na nje ya nchi za wasanii kama Ms.
Trinity kutokea Jamaica, A.Y
wa Tanzania, Prezzo wa Kenya, J Martins kutoka Nigeria na
wengine wengi. Tamasha hilo la Epiq Open Mic, ambalo ni la bure
litazinduliwa rasmi kwenye viwanja vya Mwembe Yanga Temeke
tarehe 26 ya mwezi huu ikisindikizwa na wakali kibao wa Bongo
flavor kama Diamond Platnumz, Madee, Godzila, Ney wa Mitego,
Mabeste na Mrap.
Akizungumza wakati wa kuzindua
matamasha hayo, Afsa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan alisema
kampuni ya Zantel inaaminini katika kuwawezesha vijana kufikia ndoto
zao. ‘Muziki ni ajira kwa vijana wengi, na kuamini hilo ndio maana
kampuni ya Zantel imeamua kuwafikia vijana wote wenye vipaji na
kuwapa nafasi ya kuonekana’ alisema Khan.
Baada ya uzinduzi wa tamasha
la Epiq Open Mic Mwembe Yanga tamasha hilo litaendelea kila
jumamosi kwenye makao makuu ya Zantel likiwapa nafasi vijana
kujisajili na kurekod sauti zao. Vijana watakaorekodi sauti zao
watapigiwa simu na timu ya watayarishaji wa muziki chini ya Marco Chali
pamoja na wanamuziki ili kuwapa ushauri wa namna ya kuboresha muziki
wao zaidi.
‘Zantel imejipanga kutumia fursa
hii kuwahamasisha vijana kushiriki katika kukuza vipaji vyao,
kuongeza uelewa wa mambo ya muziki pamoja na kuchangamkia fursa
zilizopo katika muziki’ alisisitiza Khan. Epiq Open Mic pia
inatarajia kuwapa fursa ya kurekodi baadhi ya vijana watakaokua
na vipaji.
GARI LAGONGA TRENI DAR MKE ALIYEKUWA AKINDESHA YUPO TAABANI MUME WAKE AFA PAPO HAPO
Wakazi wa Dar es Salaam wakingalia eneo ajali hiyo ilipotokea majira ya asubuhi leo.
|
Baadhi ya wakazi wa eneo la Moshi
Bar karibu na Mombasa nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam wakiangalia
kioo cha gari aina ya Honda CRV eneo ajali ilipotokea.
|
Agnes Msoka aliyekuwa akiendesha gari lililogonga treni na kusababisha kifo akisubiri kufanyiwa upasuaji hospitalini.
|
Dereva wa gari liligonga Treni akiwa amelazwa ICU kwa matibabu.
|
Gari iliyogonga treni likiwa limeegeshwa Kituo cha Polisi Kikuu cha TAZARA Dar es Salaam.
|
Huyo ndo marehemu aliyefariki katika ajali hiyo.
|
HAMADUU MWALIMU ALIVYO MWONESHA UBABE COSMAS KIBUGA
Bondia Cosmas Kibuga kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Hamaduu Mwalim wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki mwalimu alishinda kwa pointi picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Bondia Cosmas Kibuga kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Hamaduu Mwalim wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki mwalimu alishinda kwa pointi picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Bondia Cosmas Kibuga akimsubili kwa hamu hamaduu mwalim baada ya kudondoka chini wakati wa mchezo wao jana |
Bondia Hamaduu Mwalimu kushoto akioneshana umairi wa kurushiana makonde na Cosmas Kibuga wakati wa mpambano wao uliofanyika Dar es salaam jana Mwalimu alishinda kwa point picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Mpambano wa utangulizi kwa ajili ya kusafisha uwanja |
WASANII WAKABIDHI PICHA YA KUCHORA YA RAIS JAKAYA KIKWETE
Msanii
Salum Hamisi wa Kikundi cha Safi Culture Group akicheza kusimama na
mkono mmoja katika tamasha la wasanii chipukizi jana Dar es Salaam.
Kichanga cha siku nne chaokotwa shimoni alikokaa kwa siku 6
UKISHANGAA ya Mussa basi utayaona ya
Firauni, usemi huu umethibitika Songea baada ya Mtoto Bahati Upendo
mwenye siku 3 toka
azaliwe aliyekuwa amewekwa kwenye mfuko wa mbolea kisha kutupwa kwenye
shimo kuokolea akiwa hai licha ya kuishi shimoni humo kwa sita sita.
Ndani ya shimo hilo amekaa siku 6 bila kula wala kunywa
hadi alipo okotwa na wasamaria wema...
Hivi sasa yuko Hospitali ya Mkoa wa
Ruvuma akiwa Salama Salimini .
Yeyote Mwenye nafasi ya kumsaidia mtoto
huyu anaweza kwenda moja kwa moja Hospitali au wasiliana na namba
zifuatayo, mchango utafuatwa 0755061588 au 0755 731 234.
Dawati
la Police Wanawake Mkoa wa Ruvuma wakiwa na Wauguzi kuangalia usalama
wa Mtoto huyo aliye Tupwa. Kutoka kulia ni Muguzi Rukia Twahili anaye
fuata Devota Umbela na aliye mshika mtoto Mwenyekiti wa Mtandao wa
Police Wanawake Fadhila Chacha na wa mwisho kushoto ni A nna Chaima
USAHIRI WA SHINDANO LA BIBI BOMBA WAFANYIKA KWENYE VIWANJA VYA LEADERS CLUB, TAMASHA LA NYIMBO ZA MAKABILA LINAENDELEA
Mshiriki wa shindano la
Bibi Bomba, Bi. Veronica Kayombo (katikati) akionesha umahiri wa kuimba nyimbo
wakati wa mchujo wa kuwatafuta washiriki 10 watakaoingia katika nyumba kwa
ajili ya shindano hilo lililoandaliwa na Clouds Tv na kudhaminiwa na Airtel.
Kushoto ni Anna Nicolous na Rozalia Marko
Majaji
wa Shindano la 'Bibi Bomba' kutoka (kushoto) Zamaradi Mketema, Babuu wa
Kitaa, Regina Mwalekwa na Benny Kinyaiya, wakifuatilia washiriki wakati
wakijieleza kuhusu ufahamu wa shindano hilo, lililoanza leo katika
Viwanja vya Leaders Club Kinondoni, wakati wa Tamasha la Nyimbo za
Makabila 'Tamadunika' linaloendelea hivi sasa viwanjani hapa.
Mmoja kati wa washiriki 32, akijieleza wakati wa mahojiano rasmi viwanjani hapo....
Mmoja kati wa washiriki 32, akijieleza wakati wa mahojiano rasmi viwanjani hapo....
Baadhi ya wanacrew wasimamizi wa shoo hiyo, wakiwa eneo la tukio.....
Babu wa Kitaa, (kushoto) akiburudika kwa miondoko ya sebene na mmoja wa washiriki wa shindano hilo.
Mshiriki akijieleza......
Watazamaji wakifuatilia shindano hilo......
Waongozaji
wa Tamasha hilo, wasema lolote, Mbwiga Mbwiguke na Suzzy Bartazar,
wakijiandaa kusherehesha Tamasha hilo la Nyimbo za Makabila.
Benny Kinyaiya, akitoa maelezo mafupi kwa washiriki wa shindano la Bibi Bomba.......
Gea Habib, akifafanua jambo kwa washiriki wa shindano hilo....
Sehemu ya watazamaji......
Sehemu ya watazamaji waliojitokeza kushuhudia Tamasha hilo.....
Picha na www.sufianimafoto.com