Wednesday, May 29, 2013

BEN PAUL KUWASINDIKIZA MISS UN-COLLEGE TEMEKE


 Florence Josephat, mratibu Redd's Miss Uni-college. Kulia ni mmoja wa waratibu Francisca Mansilo.


MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Bernard Paul ‘Ben Paul’, anatarajiwa kuwasindikiza warembo wa kinyang’anyiro cha Redd’s Miss Uni-college Temeke kitakachofanyika kesho katika ukumbi wa Club Bilicanas, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, mratibu wa shindano hilo, Florence Josephat, alisema kuwa maandalizi yote yamekamilika na kwamba kilichobaki ni shoo yenyewe ambayo alitamba itakuwa katika ubora wa hali ya juu.
Alisema kuwa jumla ya warembo 13 wanatarajia kupanda jukwaani siku hiyo, ikiwa ni baada ya kunolewa vilivyo kwa takribani wiki tatu na kwamba wameiva kuwapagawisha watakaofika kushuhudia uhondo huo.
“Maandalizi yote yamekamilika hivyo tunawaomba wapenzi wa burudani na urembo kwa ujumla kujitokeza kwa wingi siku hiyo kwani kipenzi cha warembo, Ben Paul, atatoa burudani ya hali ya juu itakayoambatana na shoo kutoka kwa warembo wetu kutoka vyuo vitano vilivyopo Temeke,” alisema.
Alivitaja baadhi ya vyuo hivyo kuwa ni Chuo Kikuu cha Uganda, TIA, Chuo cha Bandari, DUCE na Chuo cha Utalii, huku akitamba kuwa kutokana na ubora wa warembo walionao, wana imani mwaka huu Redd’s Miss Tanzania atatoka katika kitongoji chao hicho.
Florence ambaye alikuwa mshiriki wa fainali za Miss Tanzania 2008, aliwataka wapenzi wa urembo na burudani, hasa wanafunzi wa sekondari na vyuo, kujitokeza kwa wingi siku ya shoo yao ili kujionea warembo bomba, huku wakipata burudani ya aina yake.
Alitaja kiingilio cha shoo yao kuwa ni Sh 10,000 na kwamba mbali ya kinywaji cha Redd’s ambao ndio wadhamini wakuu wa mashindano hayo, wadhamini wengine ni Shome Decoration & Catering, djfetty.blogspot.com na Lamada Hotel.

No comments:

Post a Comment