Friday, May 24, 2013

BFT YAOMBA WADHAMINI


Na Elizabeth John


KOCHA wa timu ya taifa ya ngumi, Remmy Ngabo, ameitaka serikali na wadau wa ngumi nchini, kujitolea kudhamini kambi ya mabondia 16 ambao wanajiandaa na mashindano ya Majiji yanayotarajia kufanyika Julai 1 hadi 7 mwaka huu, jijini Mwanza.
Awali mashindano hayo yalipangwa kufanyika Juni 20 hadi 25, kutokana na kutokuwa na maandalizi ya kutosha, wamelazimika kusogeza mbele tarehe ya kufanyika kwa mashindano hayo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, alisema mabondia hao kwasasa wanaendelea na mazoezi ya kujifua katika uwanja wa Taifa wa Ndani jijini Dar es Salaam kwaajili ya maandalizi ya michuano hiyo.
“Mabondia wapo katika hali ngumu ya maandalizi hivyo wadau wa mchezo huu tunawaomba wajitokeza kudhamini maandalizi haya,” alisema.
Alisema mashindano hayo ya Majiji ni maandaliazi ya kuwaweka sawa mabondia kwaajili ya mashindano ya Afrika na Olimpiki ambayo yanatarajia kufanyika hivi karibuni yakishirikisha mataifa mbalimbali.
“Maandalizi mazuri ya mashindano makubwa ni haya mashindano madogo, mabondia wanatakiwa kufanya mazoezi ya kutosha ili kushiriki mashindano hayo,” alisema Kocha huyo ambaye anatambulika na Shirikisho la Ngumi Duniani (AIBA).

No comments:

Post a Comment