Tuesday, May 14, 2013

CLOUDS MEDIA GROUP YAZINDUA MSIMU MPYA WA VIPINDI MJINI DODOMA, YAFANYA SEMINA DHIDI YA UHARAMIA WA KAZI ZA WASANII





Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh Zitto Kabwe ambae pia ni mdau kubwa wa Muziki hapa chnini,pia alikuwa ni mmoja wa wazungumzaji kwenye semini hiyo iliyohusu na  harakati rasmi za vita dhidi ya uharamia wa kazi za wasanii,iliyofanyika mapema leo kwenye ukumbi wa hoteli ya African Dreams,nje kidogo ya mji wa Dodoma.kutakuwepo na kampeni ya matembezi ya hisani ya harakati rasmi za vita dhidi ya uharamia wa kazi za wasanii yatakayofanyika kesho,wabunifu na wavumbuzi mbalimbali, mseto wa shuguli mbalimbali zitahusishwa.  Aidha pia mchana huu kutakuwepo na burudani hadhara ya sanaa za kisasa na za kitamaduni,mpira, chakula na bidhaa mbalimbali za kitanzania katika uwanja wa jamhuri .
 Mmoja wa wasemaji kwenye semina hiyo aliyejitambulisha kwa jina la   Patrick Ngowi  kutoka kampuni ya Helvetic Solar Contractors, akizungumzia fursa mbalimbali kuhusiana na mambo ya ujasiliamali na pia alielezea ni namna gani amefanikiwa mpaka kufikia kumilimiki lampuni yake binafsi kupitia fursa alizokuwa akikumna na nazo na kuzifanyia kazi vilivyo. 

 Mmoja wa washiriki wa semina hiyo akiuliza swali kwa Mh Zitto Kabwa kuhusiana na mambo mbalimbali ya ujasiliamali na namna ya kuzitumia fursa hizo katika kujikwamua kimaisha.
 Mh Zitto kabwe akimsikiliza mmoja wa washiriki wa semina hiyo alipokuwa akiulizwa kuhusiana na suala la fursa zinazopatikana kwa vijana na namna ya kuzitumia katika ujumla wa kujikwamua na ugumu maisha,ambapo watanzania wengi wamekuwa wakizilalamikia.

No comments:

Post a Comment