Pambalo
 la watani wa jadi Simba na Yanga la Ligi Kuu ya Vodacom lililochezwa 
jana (Mei 18 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na 
kumalizika kwa mabingwa wapya Yanga kushinda mabao 2-0 limeingiza sh. 
500,390,000.
Mechi
 hiyo namba 180 ambayo ilikuwa kati ya saba la kuhitimisha ligi hiyo 
msimu wa 2012/2013 ilishuhudiwa na watazamaji 57,406 waliokata tiketi 
kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 
20,000 na sh. 30,000.
Kila klabu imepata mgawo wa sh. 123,970,927.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 76,330,677.97.
Kiingilio
 cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata 
tiketi hizo walikuwa 19,039 na kuingiza sh. 95,195,000 wakati kile cha 
sh. 7,000 kiliingiza watazamaji 17,647 na kupatikana sh. 123,515,000.
Mgawo
 mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 63,036,064.81, 
tiketi sh. 3,818,890, gharama za mechi sh. 37,821,638.88, Kamati ya Ligi
 sh. 37,821,638.88, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 
18,910,819.44 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) 
sh. 14,708,415.12.
No comments:
Post a Comment