Tuesday, May 14, 2013

Vodacom yaungana na UN wiki ya nenda kwa usalama



    Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani Tanzania,Mohamed Mpinga akiongea na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Mapambano kuhusiana na masuala ya Usalama Barabarani katika kuadhimisha wiki ya Umoja wa Mataifa ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo huadhimishwa Mei 6 hadi 12 ,ambapo wafanyakazi wa vodacom waliambatana na mkuu huyo katika kutoa elimu  kwa watoto wa shule hiyo na Uzuri zote za Sinza jijini Dares Salaam na kutoa msaada wa madafutari na vitabu mbalimbali vya kujisomea,anaeshuhudia kulia ni Meneja uhusiano wa nje wa Vodacom Tanzania,Bw.Salum Mwalim.
 Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania,Bi.Ena Mwangama,akimkabidhi kitabu  cha sayansi mmoja wa wanafunzi wa shule ya  Mapambano iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam, wakati wafanyakazi wa vodacom Tanzania,walipofika shuleni hapo kutoa elimu ya Usalama Barabarani ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya  wiki ya Umoja wa Mataifa ya Nenda kwa Usalama Barabarani yaliyoanza  Mei 6 hadi 12.kila mwaka.
   Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania , wakiwafundisha wanafunzi wa shule ya msingi  ya Mapambano ya jijini Dar es Salaam, baada ya kuwapa msaada wa vitambu vya sayansi ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya  Umoja wa Mataifa ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo huadhimishwa Mei 6 hadi 12 ,ambapo wafanyakazi wa vodacom waliambatana na mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani Tanzania,Mohamed Mpinga  (hayupo pichanini) kutoa elimu  kwa watoto wa shule za Uzuri na Mapambano zote za Sinza jijini Dares Salaam.
 Meneja wa Vodacom Tanzania Grece Lyon  (kushoto ) na Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Uzuri Tandale ya jijini Dar es Salaam, (kulia)wakionyeshwa vitabu vya sayansi na wanafunzi wa shule hiyo baada ya kukabidhiwa na wafanyakazi wa Vodacom, Ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo huadhimishwa Mei 6 hadi 12 ,ambapo wafanyakazi wa vodacom waliambatana na mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani Tanzania,Mohamed Mpinga  (hayupo pichanini) kutoa elimu  kwa watoto wa shule za Uzuri na Mapambano zote za Sinza jijini Dares Salaam.

 Meneja Mawasiliano wa Vodacom Rukia Mtingwa akiwaongoza wanafunzi wa shule ya msingi ya Uzuri iliyopo Tandale jijini Dar es Salaam, kwenda kujifunza jinsi ya kutumia alama za barabarani ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Umoja wa Mataifa ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo huadhimishwa Mei 6 hadi 12 ,kila mwaka .Wafanyakazi wa Vodacom waliambatana na Mkuu wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Tanzania,Mohamed Mpinga   (hayupo pichanini)  Pia walitoa msaada wa vitu  mbalimbali ikiwemo vitabu vya Sayansi.

No comments:

Post a Comment