Wakali wa klabu ya Azam ambapo baadhi wa hawatakuwa kwenye kikosi cha msimu ujao akiwemo Gaucho (24)
KLABU ya soka ya Azama imeweka bayana kwamba haitaacha mchezaji iliyo na
mkataba naye na wala haitaongeza mchezaji mwingine katika kikosi
ilichonacho sasa.
Kwa mujibu wa taarifa yake, Azam imesema kama ilivyokuwa wakati wa
dirisha kubwa la usajili 2012/13 ambapo Azam ilimuongeza George
Odhiambo 'Blackberry' pekee, safari hii imepandisha twachezaji wawili wa
U20, Mudathir Yahaya na
golikipa Hamadi Juma Yahya Kadedi na kufunga zoezi la usajili.
Taarifa hiyo inanukuu ripoti toka kwa Kocha mkuu wa Azam Stewart
Hall, kuwa hakuna sababu ya klabu kwenda nje kusajili wachezaji ambao
viwango vyao havipishani na waliopo klabuni.
Mchezaji Abdulhalim Humoud amepata timu nchini Afrika ya Kusini, Abdi
Kassim 'Babi' mkataba wake umekwisha kama ilivyo kwa Deogratius
Munishi Dida huku Uhuru Selemani akirejeshwa Simba SC baada ya kumaliza
msimu wa mkopo na Azam FC.
Wachezaji wengine wote waliosalia
wanabaki klabuni na kocha mkuu amependekeza baadhi ya makinda wa Under
20 walioonesha viwango vya juu wapandishwe timu kubwa, wapewe mikataba
na kisha wapelekwe kwa mkopo ili wakapate nafasi ya kucheza. Wachezaji
hao ni Omary Mtaki na Kevin Friday.
Azam ambayo imemaliza
ligi ikishika nafasi ya pili kwa msimu wa pili mfululizo itaanza kambi
ya kujiandaa na msimu mpya hapo June 24 kwa mujibu wa ratiba ya mwalimu
na baada ya kumaliza kipindi cha pre season, kikosi cha Azam
kitasafiri nje ya nchi kucheza mechi za majaribio kama ilivyo kawaida
yake.
Wachezaji wanaounda kikosi cha Azam FC ni;
Magolikipa; Mwadili Ally, Aishi Salum na Hamad Juma Yahya
Mabeki; Himid Mao, Erasto Nyoni, Waziri Salum, Samih Nuhu, Luckson
Kakolaki, Aggrey Morris, Said Moradi, David Mwantika na Jockins Atudo
Viungo; Kipre Bolou, Salum Abubakar, Jabir Aziz, Ibrahim Mwaipopo, Humphrey Mieno na Mudathir Yahya
Washambuliaji; John Bocco, Gaudence Mwaikimba, Khamis Mcha, Kipre Tchetche, Brian Umony na Abdallah Seif Karihe
Wakali wa klabu ya Azam ambapo baadhi wa hawatakuwa kwenye kikosi cha msimu ujao akiwemo Gaucho (24) |

No comments:
Post a Comment