Monday, June 3, 2013

BASATA YAANZA KUYAFANYIA KAZI MAOMBI YA WASANII


Na Elizabeth John

BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kushirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari za Sanaa na Utamaduni (CAJAtz), kesho wanatarajia kuzikutanisha taasisi mbalimbali zinazohusika na urasimishaji ili kutoa elimu kwa wasanii, wadau na wakuzaji wa sanaa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Kaimu katibu mkuu mtendaji wa BASATA, Godfrey  Mngereza, alisema kuwa taasisi hizo zitakutana katika ukumbi wa BASATA ulioko Ilala Sharif Shamba.
 
Mngereza alizitaja taasisi hizo ambazo zitakutana kuwa ni Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza, Chama cha Hakimiliki na Hakishiriki Tanzania (COSOTA), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).
 
  Alisema katika kuelekea urasimishaji wa sekta ya filamu na muziki ambao ulianza rasmi Januari mosi na ifikapo Julai mosi mwaka huu hakuna kazi yoyote ya filamu na muziki itakayoingia sokoni bila kuwa na stampu ya TRA.
 
  Pia aliwataka wadau wa sekta ya sanaa kupeleka michango na hoja zao ili kuleta mustakabali utakaojenga sekta ya sanaa.

No comments:

Post a Comment