Tuesday, June 18, 2013

Epiq Open Mic kumekucha Dar


Vijana waliojitokeza wakiwa kwenye foleni. 
 Jopo la washauri likongozwa na Marco Chali (wa pili toka kulia), akifuatiwa na Dknob, Walter na mwisho kulia ni Godzila
 Mmoja wa vijana akiimba mbele ya washauri.
Mmoja wa wasichana akionyesha uwezo wake.

Vijana waliojitokeza wakijiandikisha.


NaMwandishi wetu


Baada ya kuzinduliwa kwa mafanikio wiki mbili zilizopita katika viwanja vya Mwembe Yanga, mamia ya vijana wamejitokeza mwishoni mwa wiki hili katika viwanja ya ofisi za Zantel kuhudhuria usaili wa Epiq Open Mic.
Huku ikiwa imebaki wiki kadhaa kabla ya kuanza kwa msimu mya wa Epiq BSS, Zantel kwa kushirikana na Marco Chali Foundation, wamezindua Epiq Open Mic ili kuwapa vijana nafasi ya kuonyesha vipaji vyao.
Fursa hii, ya Epiq Open Mic, inawapa nafasi vijana wenye vipaji vya muziki fursa ya kusikilizwa na mtayarishaji wa muziki maarufu nchini, Marco Chali pamoja na jopo la wanamuziki kama Godzila na Dknob, ambao wanawashauri mambo kadhaa kuhusiana na muziki wao, na huku wale wenye vipaji zaidi wakipewa nafasi ya kurekodi na Marco Chali.
Akizungumzia Epiq Open Mic, Marco Chali anasema hii ni fursa ya vijana kujifunza misingi ya muziki, lakini pia kuweza kurekodiwa muziki wao.
‘Lengo la Epiq Open Mic ni kuwahamasisha vijana kushiriki katika kukuza vipaji vyao, kuongeza uelewa wa mambo ya muziki pamoja na kuchangamkia fursa zilizopo katika muziki’ alisema Chali.
Marco Chali ambaye pia ni mtunzi na mwimbaji, ametayarisha nyimbo nyngi ambazo zimeshinda tuzo ndani na nje ya nchi za wasanii kama Ms. Trinity kutokea Jamaica, A.Y wa Tanzania, Prezzo wa Kenya, J Martins kutoka Nigeria na wengine wengi.
Kwa upande wake, Afsa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan alisema kampuni ya Zantel inaaminini katika kuwawezesha vijana kufikia ndoto zao.
‘Muziki ni ajira kwa vijana wengi, na kuamini hilo ndio maana kampuni ya Zantel imeamua kuwafikia vijana wote wenye vipaji na kuwapa nafasi ya kuonekana’ alisema Khan.

No comments:

Post a Comment