By. Pascal Mayalla           
Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania, MKURABITA,  unaendelea na  utekelezaji kwa vitendo, wa awamu ya kwanza ya kuwapatia  “Maisha Bora kwa Kila Mtanzania” kwa kuendelea  kugawa
hati miliki za kimila  kwa wanavijini mbali mbali, ili kwanza kuwamilikisha rasilimali, kasha ndipo kuwaelimisha jinsi ya kuzitumia rasilimali hizo kujiletea maendeleo ambayo ndiyo yatakayo leta maisha bora kwa kila Mtanzania.
Hayo yamebainishwa na Mratibu 
wa  Mkurabita, Bibi. Seraphia Mgembe, wakati akitoa tathmini ya zoezi la
 kuwakabidhi hati miliki za kimila, kwa wakulima wa zao la chai wa 
wilaya ya Mbinga, Mufindi na Njombe, lililohotimishwa hivi karibuni.
Bibi Mgembe amesema, maisha 
bora kwa kila Mtanzania, haya patikana kwa wananchi kubweteka na 
kuisubiria serikali ndio ifanye kila kitu, bali ni kwa serikali kujenga 
mazingira ya uzalishaji mali, ikiwemo kuwamilikisha wananchi rasilimali 
zao, na maendeleo ya kweli, yatapatikana kwa wananchi kuelimishwa na 
kujibiidisha katika kutumia
rasilimali hizo kama dhamana za kupatia mitaji ya kujiletea maendeleo.
Bibi Mgembe amesema,  huku 
zoezi la kuwamilikisha wananchi rasilimali zao likiendelea, MKURABITA 
inayapitia tena yale maeneo ambayo tayari wananchi wake wameisha 
kabidhiwa hati miliki, ili kuwajengea uwezo wananchi hao, jinsi ya 
kuzitumia hati miliki hizo kama dhamana na kukopa katika mabenki ili 
kutumia  fedha za mkopo kujiletea maendeleo.
Bibi Mgembe amesisitiza, 
maendeleo ya kweli na endelevu, ni yale yanayotokana na  matumizi ya 
rasilimali zilizowazungunguka wananchi husika,  nan i kwa kulitambua 
hilo, ndio maana MKURABITA imekuwa ikizishirikisha taasisi za kifedha, 
ili kuwaelimisha wananchi fursa mbalimbali za mikopo ya kibiashara na 
kimaendeleo zinazoweza
kupatikana kwa kutumia dhamana za hati miliki zao.
Kwa upande wao, Wakuu wa 
wilaya za  Njombe, Bi. Sarah Dumba na Mkuu wa Mufindi, Bi. Evarista 
Kalalu, waliipongeza MKURABITA kwa juhudi zake za kuhakikisha wakulima 
wa chai sasa wanayamiliki rasmi mashamba yao ya chai, ambapo  mwanzo 
walikuwa na utajiri ambao hauwafaidii chochote zaidi ya kulima na kuuza 
mazao yao, lakini sasa, sio tuu ni wamiliki wa mashamba hayo, bali 
wanaweza kuzitumia hati miliki zao, kukopo mikopo mikubwa ya 
kimaendeleo.
Jumla ya hati miliki za kimila zaidi ya 2000 zilikabidhiwa kwa wakulima wa chai.
 Wananchi wa Njombe, wakifurahia kukabidhiwa hati miliki za kimila, kulikofanywa na MKURABITA hivi karibuni.
 Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Sarah Dumba, akimkabidhi hati miliki ya kimila, Mwanakijiji wa kijiji cha Matembwe, Bw. Solomon Matunasa wakati wa hafla fupi ya MKURABITA kukabidhi hati miliki za kimila kwa wakulima wa chai wa Rungwe, Mfindi na Njombe hivi karibuni. Katikati ni Mratibu wa MKURABITA, Bibi Seraphia Mgembe.
Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Sarah Dumba, akimkabidhi hati miliki ya kimila, Mwanakijiji wa kijiji cha Iwafi, Bw. Eneas Paruasi wakati wa hafla fupi ya MKURABITA kukabidhi hati miliki za kimila kwa wakulima wa chai wa Rungwe, Mfindi na Njombe hivi karibuni. Katikati ni Mratibu wa MKURABITA, Bibi Seraphia Mgembe.
No comments:
Post a Comment