MRISHO MPOTO NA BENDI YA MJOMBA BAND KUFANYA KAMPENI YA USAFI WA MAZINGIRA
Msanii
wa ngoma za asili na Mkurugenzi wa bendi ya Mjomba Band Mrisho Mpoto
akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kinondoni Mkwajuni
wakati alipotangaza kuhusu kundi lake kuanza kampeni kubwa ya
kuhamasisha wananchi kuhusu usafi wa mazingira mijini na vijijini kwa
kunawa mikono na sabuni, kujenga na kutumia vyoo bora na kuboresha
mzingira kwa ujumla ili kuhakikisha elimu hiyo inawafikia walengwa kwa
kubadili tabia na njia mbadala za mawasiliano kuhusu elimu hiyo,
Upatikanaji wa maji safi na salama na usafi wa mazingira bado ni tatizo
kubwa kwa watanzania walio wengi, mwaka 2010 aslimia 9 tu ya wananchi
waishio vijijini na asilimia 22 ya wananchi waishio mijini waliweza
kupata huduma bora za usafi wa mazingira. kati ya sababu zingine , ni
watu kutozingatia faida za usafi wa mazingira Katika k kampeni hiyo
Mrisho Mpoto na kundi lake la mjomba Bandi wanashirikiana kwa pamoja na
Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, kushoto ni Mariam Mahamudu Afisa
Afya, Mazingira Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii , Kampeni hiyo itaanza
na mikoa ya Dodoma, Mara, Njombe, Rukwa na Tanga kabla ya kuendelea
mikoa mingine Mariam
Mahamudu Afisa Afya, Mazingira Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii
akizungumza katika mkutano huo kuzungumzia kuhusu kampeni hiyo, kulia ni
Mrisho Mpoto Mkurugenzi wa Mjomba Band.
No comments:
Post a Comment