Huyu
mama alikaa juu ya paa kwa siku tano tangu jumamosi kupinga nyumba yao
kuchukuliwa na bank.Anasema mumewe alimdhamini mtu ambaye alichukua mkopo
bank miaka mingi iliyopita na kushindwa kulipa mkopo huo.
Kwa mujibu wa maelezo yake , kesi yao bado ipo mahakamani kwani tayari yule mdaiwa kuna mali zake zilizotaifishwa.
Mdaiwa
alikopa ml 240, wameuza nyumba zake 2 na mabasi mawili.Wadaiwa
wanaomba kujua kiasi kilichobaki katika hilo deni ili watoe na kuuza nyumba yao.
Nyumba
ipo mbezi Tangi bovu na inaeneo kubwa sana .Mama anasema hata akiuza si
chini ya ml 500 iweje atolewe kwa ml 240 wakati mdaiwa nyumba zake mbili
zimeshachukuliwa na mabasi mawili yale makubwa ya safari za
mikoani yamechukuliwa .Hiyo ml 240 haijatimia tu?na kama bado kiasi gani kimebaki?
Ndani ya nyumba vitu walishachukua hao watu wa auction mart, ndani kweupe.Na wakati haya yakiendelea hakukuwa na amri yoyote iliyotoka mahakamani wala hawakuwa na kibali cha mahakama.
Gea alimfuata huko huko juu kumsikiliza...
Chumba cha habari cha clouds fm kinafuatilia hapo bank ya Tanzania Investment bank(TIB) kujua chanzo cha tatizo maana
wakati haya yakiendelea hiyo jana inasemekana hii nyumba
ilikuwa imeshauzwa.
Jana hiyohiyo, mume wa huyu mama
alikuwa mahakamani maana ilikuwa siku ya kesi kuendelea kusikilizwa.
Taarifa zinadai kuwa Mumewe alirudi na oda maalum kutoka mahakamani kuwa nyumba hiyo isiguswe na vitu vyao virudishwe.
Dinamarios Blog
No comments:
Post a Comment