Monday, June 3, 2013

TAMASHA LA COKE ZERO LAFANA ARUSHA


Mmwanamuziki wa kundi la muziki wa  Hip Hop la G-White Juma Abdallah akitumbuiza mamia ya wapenzi wa muziki  wakati wa tamasha la Coke Zero lililofanyika Jijini Arusha mwishoni mwa wiki.

Mmwanamuziki wa kundi la Hip Hop la G-White Paul Mushi akitumbuiza mamia ya wapenzi wa muziki  wakati wa tamasha la Coke Zero lililofanyika Jijini Arusha mwishoni mwa wiki.

Wakazi wa Jiji la Arusha na vitongoji vyake walijitokeza kwa wingi katika viwanja wa Soweto Jumamosi Juni Mosi kushuhudia miondoko ya wasanii wa muziki wakiongozwa na mkali wa Hip Hop nchini Joe makini pamoja na kikundi cha G-White.
Tamasha hili lilikuwa maalum kwa ajili wa uzinduzi wa kinywaji kipya cha Coca-cola Zero kanda ya kaskazini iliyo chini ya kampuni ya kutengeneza na kusambaza vinywaji baridi jamii ya Coca-Cola ya Bonite Bottlers yenye makao yake mjini Moshi.
Burudani hiyo ya aina yake ilianza saa nane kwa vijana waendesha piki piki wakionyesha umahiri wao wa kutawala chombo hicho cha moto kabla ya kikundu cha Hip Hop kcha Paul Mushi na Juma Adballah kupanda jukwaani na kupokelewa kwa shangwe na maelfu ya wapenzi wa muziki waliojitokeza kushuhudia tamasha hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari katika tukio hilo, Mkurungenzi Mkuu wa Mauzo wa kampuni ya Bonite Bottlers Bw. Christopher Loiruk alisema kampuni yake inayo furaha kwa kuandaa tamasha hilo kuitambulisha Coke Zero  na kuburudika pamoja na wateja wao. 
‘Bonite Bottlers tumekuwa mstari wa mbele kudhamini michezo pamoja na kuendeleza vipaji vya vijana na leo tumeona kikundi kipya kabisa cha muziki wa Hip Hop kikipata nafasi ya kuonyesha umahiri. Wapenzi wa muziki watakubaliana name kuwa wakiendelea kupewa fursa na kuwezeshwa wataweza kuwa moja ya wasanii wanzuri sana hapa nchini.’ Anasema Bw. Loiruk.
Naye Meneja Bidhaa Coca-Cola Tanzania Maurice Njolowa alisema nia ya kampuni yake ni kuweka kinywaji kipya cha kampuni hiyo cha Coke Zero karibu na vijana na kwa kuandaa tamasha la bure kama hivi ndio njia nzuri ya kuwa karibu.
Tamasha hilo ni muendelezo wa tamasha la Coke Zero lililofanyika Coco Beach jijini Dar es Salaam wakati kinywaji hicho kisicho na sukari kilipozinduliwa jijini Dar es Salaam mwezi wa Machi mwaka huu. Tamasha lingine la Coke Zero litafanyika jijini Mwanza hivi karibuni

No comments:

Post a Comment