Tuesday, June 25, 2013

ZANTEL YAZINDUA HUDUMA YA DAKTARI KWENYE SIMU YA MKONONI


Mkuu wa Kitengo cha Rasirimali Watu cha Zantel, Francis Kiaga akifafanua jambo wakati wa ushirikiano na Kampuni ya BR Solution na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ili kuwawezesha watanzania kupata huduma ya ‘Daktari kwa njia ya simu’ ikiwa na lengo la kupata ushauri kwa masaa 24 mahali popote nchini. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa BR Solutions, Richard Toba na Ofisa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan. (Picha na Habari Mseto Blog)
Mkurugenzi Mkuu wa BR Solutions, Richard Toba (kulia) akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
 Ofisa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan.
Dk. Aidan Njau akifafanua jambo, Sajid Khan. 

DAR ES SALAAM, Tanzania

KAMPUNI ya Simu za Mkononi ya Zantel imezindua ushirikiano na Kampuni ya BR Solution na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ili kuwawezesha watanzania kupata huduma ya ‘Daktari kwa njia ya simu’ ikiwa ni kupata ushauri kwa masaa 24 mahali popote nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya Zantel jijini Dar es Salaam leo, Mkuu wa Kitengo cha Rasirimali watu cha Zantel Francis Kiaga alisema, wameamua kuingia ubia na Wizara pamoja na BR ili kuwasaidia watumiaji wa Zantel kuongea moja kwa moja na madaktari endapo watakuwa na tatizo linalowasumbua ambalo wanahitaji ushauri.

“Huduma hii ya ‘Daktari kwa njia ya simu’ sisi kama Zantel tunaimani itawanufahisha watanzania kupata ushahuri kwa bei laisi juu ya matatizo yanayowasumbua na ndio maana tumeamua kubolesha maisha ya wateja wetu kwa teknolojia ya simu za mikononi kwa kuwa tunatambua Watanzania wengi wanatumia simu,”alisema Kiaga.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa BR Solution Francis Njau alisema, huduma hiyo itashughulikia magonjwa kama, Ukimbi, Cancer, Moyo, Malaria, Afya ya Uzazi na huduma ya kwanza ambayo bado wanajipanga zaidi jinsi ya kuwafahamisha watanzania jinsi ya kufanya tofauti na kumwelekeza mgonjwa kwenda duka la madawa bila ya kwenda hospitalini kwanza.

“Tukumbuke Zantel walishawahi kushinda tuzo za ubunifu katika kutumia teknolojia katika kubolesha afya na huduma kupitia huduma yake ya Mobile Baby katika tuzo la kongamano la Makampuni ya simu mwaka jana,”alisema.

Kwa upande wa Daktari Aidan Njau wa Aghakan Hospitali alisema, wamejipanga kuhakikisha wanawapa ushauri mzuri watanzania ambao watapiga simu au kutuma meseji ambayo itatangazwa hapo badae na kudai kuwa huduma hiyo itakuwa sio kumpata dawa mgonjwa kwa kuwa fani yao hairuhusu kumpa mgonjwa dawa bila ya kumpima.

“Katika kipengele cha huduma ya kwanza kuna ushahuri ambao tutamwambia mgonjwa atakapopiga simu, ila kumwambia tumie dawa ni ngumu kwa kuwa mtu anaweza kupiga simu anasema anaumwa kichwa ukamwambia tumie Diklofenak alafu kumbe ana vidonda vya tumbo ambapo ni hatari zaidi,”alisemaTumaini.

No comments:

Post a Comment