Baadhi ya vijana wanaofanya shughuli zao kando kando ya barabara ya Uhuru Dar es salaam eneo la Malapa wakicheza mchezo wa bao mchezo huo uliopata umaarufu mkubwa miaka ya nyuma ulikuwa ukuchezwa na wazee pekee rakini kwa sasa vijana wamekuwa wakiufatilia na kuucheza kwa ustad mkubwa kushoto ni Jagani Ndizi na Omari Kijungujiko PICHA NA BLOG YA SUPER D |
Wednesday, July 31, 2013
VIJANA WACHANGAMKIA MCHEZO WA BAO
Aibu! Njemba lafungwa miaka 30 kwa kumlawiti, kumzalisha bintie
Yusufu Amani (39) aliyembaka mwanaye wa kumzaa kisha kumzalisha baada ya kutengana na mkewe Afungwa miaka 30 |
Hapa akijifunika sipigwe picha baada ya hukumu |
Mabondia wa Tanzania huuza mechi zao Ulaya?
Rashid Matumla 'Snake Man' |
Benson Mwakyembe |
Karama Nyilawila aliyetwaa ubingwa wa WBF Ulaya |
MABONDIA Mada Maugo na Benson Mwakyembe Jumamosi walipokea vipigo nchini Russia katika mapambano yao ya kimataifa, huku kukiwa na tuhuma kwamba mabondia wengi wa Kitanzania wanaoenda kupigana nje ya nchi 'huuza' mechi zao.
Maugo alipokea kichapo cha TKO ya raundi ya 5 katika pambano la raundi 8 dhidi ya bondia asiye na uzoefu Movsur Yusupov aliyecheza mapambano manne tu kulinganisha na Mtanzania huyo aliyepigana michezo 25.
Mtanzania mwingine, Mwakyembe alidundwa kwa KO ya raundi ya 7 ya pambano lake la raundi 8 dhidi ya bondia mwingine asiye na uzoefu Apti Ustarkhanov, ambaye hilo lilikuwa ni pambano lake la tatu na la pili kushinda tangu aingie kwenye ngumi za kulipwa.
Kina Maugo walipambana dhidi ya wenyeji wao katika mapambano ya uzito wa Super Middle ya raundi nane yaliyofanyika katika ukumbi wa Trade & Entertainment Centre 'Moskva', Kaspiysk chini ya wakala Mkenya Thomas Mutua.
Vipigo vya mabondia hao vimekuja wakati wadau wa ngumi za kulipwa wakihoji sababu zinazofanya mabondia wa Kitanzania kushindwa kutamba kila waendapo nje huku ripoti mbalimbali zikiwatuhumu mabondia wa majuu kuwatumia mabondia kutoka Afrika kupandisha chati zao katika viwango vya ubora kwa kuwanunua wawaachie washinde.
Ripoti za kuuzwa mechi au kuwapo kwa mchezo mchafu ziliwahi kutolewa na baadhi ya mabondia akiwamo Pascal Ndomba na Francis Cheka aliyepokea kichapo cha kushangaza mapema mwaka huu nchini Ujerumani.
Ndomba anayepigana uzito wa juu wa (Cruiserweight), alisema baadhi ya mawakala wa nje hutaka mabondia dhaifu wa kwenda kupigana na mabondia wao ili kupata ushindi kirahisi na kuboresha rekodi zao.
"Hili ndilo linalofanyika, bondia mkali mara chache sana kupelekwa nje na hata akienda basi atahujumiwa ili apoteze mchezo kwa manufaa ya mabondia wanaoenda kupigana nao," Ndomba alisema hivi karibuni.
Naye Cheka alitoa maelezo ya kufanyiwa 'hila' katika pambano lake dhidi ya Uensal Arik aliloongoza kwa raundi sita za mwanzo kabla ya kurushiwa kitaulo katika raundi ya saba na kupoteza mchezo kwa TKO.
Pascal Ndomba |
Cheka alisema kambi ya mpinzani wake walimfuata hadi hotelini alipofikia kuelekea pambano lao kumshawishi awaachie pambano hilo kwa ahadi ya pesa lakini alipokataa ndipo alipokuja kuhujumiwa ulingoni kwa mtu aliyekuwa upande wa kona yake kurusha taulo ulingoni ilhali alikuwa akiongoza kwa pointi.
Bondia huyo anayeaminika kuwa bora zaidi nchini kwa sasa katika uzito wake, alisema hakuambatana na kocha wake wakati akienda katika pambano hilo hivyo hata kwenye kona yake walikuwa wenyeji wake na ndiyo waliorusha taulo ulingoni.
Hata hivyo, wapo waliomtuhumu kwamba huenda Cheka alicheza 'dili' na wakala wa pambano hilo ili kutotibua rekodi ya mpinzani wake ambaye alikuwa amepoteza pambano moja tu ya 18 aliyokuwa amecheza.
NIPASHE ilizungumza na Marais wa Mashirikisho ya Ngumi za Kulipwa Tanzania, Emmanuel Mlundwa wa PST na Yasin Abdallah 'Ustaadh' wa TPBO kutaka kujua ukweli kuhusu tuhuma hizo, ambapo walikuwa na maoni tofauti .
Mlundwa alisema kinachowaponza mabondia wa Tanzania siyo hujuma wala nini ila maandalizi duni wanayofanya kabla ya mapambano yao pia kuwa na viwango duni kulinganisha na wapinzani wao wanaoenda kucheza nao.
"Ngumi za kulipwa ni biashara, mabondia wa ngumi hizo wanapotafutiwa mechi wanapaswa kujiandaa, lakini hilo halifanyiki na hivyo kwenda kulitia aibu taifa na kujiharibia soko wao wenyewe bila kujua," alisema Mlundwa.
Nyota huyo wa zamani wa kimataifa wa ngumi, alisema siyo kweli kama kuna rushwa zinazofanyika bali Watanzania wanaopewa nafasi kulingana na rekodi zao nchini huenda kupigana kichovu kwa kukosa maandalizi mazuri.
Ustaadh yeye alisema
Francis Cheka |
"Mabondia wengi hawafanyi mazoezi mpaka wakati wa pambano, hapo unatarajia afanye vizuri? Pia hawaishi kwa kuzingatia miiko ya ngumi na hivyo wanapoenda nje ni rahisi kupigwa na kuhisiwa labda wanauza," anasema.
Alisema ni vyema mabondia wakafanya kazi chini ya mameneja kama ilivyokuwa kwa Rashid Matumla kwani itafanya ajikite kwenye mazoezi tu na mambo mengine kuwaachia meneja zao.
Ustaadh alisema majukumu wanayobeba mabondia ya kufanya kila kitu wakati mwingine huwafanya washindwe kujikita kwenye mazoezi na hivyo kujikuta muda wa pambano ukifika hawajajiandaa vizuri.
Rais huyo wa TPBO-Limited, alisema pia mabondia wengi hutoa visingizio kila wanapopigwa nje ya nchi bila kuangalia kama sheria za ngumi zinasemaje wanapokuwa kwenye ulingo na kutolea mfano pigano la Cheka na Arik.
"Cheka alipolalamika nilimuuliza vipi katika pambano lake na Arik, hakutupa ngumi yoyote katika raundi ya 7 na kupigwa makonde mfululizo na kunieleza mkono wa kulia ulimzingua, sheria zinasema bondia asipojibu mapigo kwa zaidi ya ngumi 10 alizorushiwa refa anaweza kuvunja pambano au wasaidizi wa bondia kuingilia kati kwa kurusha kitaulo na ndivyo ilivyotokea," alisema.
Mada Maugo |
JACK WOLPER AMJIBU MBAYA WAKE ALIYETANGAZA KUWA YEYE NI KAHABA
Msanii nyota wa filamu bongo, Jacqueline Wolper amewataka wasanii wa bongo movie kuacha tabia ya kupigana majungu ya kinafiki ambayo huchangia kujenga bifu za kijinga....
Akiongea na mpekuzi wetu, wolper alidai kuwa kuna mipaka ya watu kuishi lakini kuna baadhi ya wasanii wanaamini kwamba majungu ndo mshahara wao kiasi kwamba wasipomsengenya mtu basi hawawezi kuishi...
Wolper anadai kuwa yeye ni miongoni mwa wasanii wanaosemwa sana kwa mabaya hasa kuhusu maisha yake ya kila siku.Hali hiyo inatokana na umaarufu alionao ambao huwafanya wasanii wenzake wamchukie hasa wasanii wa kike...
Hii ni kauli ya Wolper alipoongea na ripota wetu:
"Wasanii tungekuwa na ushirikiano kama nisha tungefika mbali sana.
"Mimi simuogopi mtu katika maisha yangu, lakini ninachohitaji katika maisha yangu ni Heshima.
"Ukiona nimekukwaza, basi njoo nyumbani au nambie nikufuate ili tuyamalize kibinadamu na si kudhalilishana mitandaoni...
"Kuna msanii mmoja wa kike amekuwa akinichafua sana mitandaoni kwa kuniita kahaba, najuza na matusi mengine kibao.
"Huyo ni mtu anayetafuta pakutokea, anatafuta kujulikana kupitia Wolper na pengine kafulia na sasa anatafuta mtaji.
"Tangu anitukane sikuona haja ya kumjibu kutokana na heshima niliyo nayo katika kazi yangu na heshima yangu kwa wazazi , ndugu na jamaa.
"Niliamua kumwachia mungu.Kama ni kahaba au najiuza, mungu anajua.Alisema Wolper
KESI YA LADY JAYDEE YAPIGWA KALENDA
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kinondoni, leo imeiaharisha kesi inayomkabili msanii wa kizazi kipya nchini, Judith Wambura 'Lady Jaydee' a.k.a Annaconda dhidi ya uongozi wa Clouds Media Group hadi Agosti 2, mwaka huu.
Kesi hiyo ya madai iliyopo mbele ya Hakimu Athumani Nyamlani, leo ililetwa kwa ajili ya kusikilizwa lakini ilishindikana kutokana na wakili anayemtetea, Jaydee kutotokea mahakamani hapo na kumtuma mwakilishi wake.
Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa wakili huyo wa Jaydee, amekwenda katika Mahakama Kuu kuhudhuria kesi nyingine na hivyo kushindwa kufika mahakamani hapo kuendelea na kesi hiyo na hivyo kuahirishwa hadi Agosti 2, mwaka huu.
Kesi hiyo ya madai ilipelekwa mahakamani hapo na Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa Kampuni ya Clouds Media kwa madai ya kuukashifu uongozi huo.
Kwa mujibu wa mdai huyo, ambaye ni uongozi wa Clouds Media ulidai kuwa mdaiwa huyo ambaye ni Lady Jaydee aliandika maneno ya kuukashifu uongozi huo kupitia mitandao ya kijamii.
Tuesday, July 30, 2013
SUPER D SUPER COACH ALIPO JUMUHIKA NA NDUGU NA JAMAA ZAKE WA KARIBU KUFUTURU NYUMBANI KWAKE
SUPER D AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA NDUGU ZAKE NA MARAFIKI
Super D akipata futari na Ibrahimu Kamwe
Super D akipata futari na Ibrahimu Kamwe |
Super D akipata futari na Ibrahimu Kamwe |
SUPER D |
SUPER D KATIKA POZI
DAR ES SALAAM KUWA MWENYEJI WA MAONYESHO YA VODACOM ELIMU EXPO 2013 VIWANJA VYA CHUO CHA POSTA KIJITONYAMA AGOSTI 30
Naibu
Waziri wa Elimu, Phillip Mulugo, akizungumza na waandishi wa habari,
kwenye Ukumbi wa Kivukoni, Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo,
wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa maonyesho ya siku tatu ya Vodacom
Elimu Expo, yanayotarajia kuanza Agosti 30, mwaka huu katika Viwanja vya
Michezo vya Chuo cha Posta, Kijitonyama jijini. Kulia ni Mkurugenzi
Mkuu wa Elimu Expo, Joel Njama (kushoto) ni Mkuu wa Idara ya Masoko na
Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa.
Naibu
Waziri wa Elimu, Phillip Mulugo (katikati) Mkurugenzi Mkuu wa Elimu
Expo, Joel Njama (kulia) na Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa
Vodacom, Kelvin Twissa, wakigonganisha glasi, kama ishara ya uzinduzi wa
maonyesho hayo, wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika
Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo.
Mkurugenzi
Mkuu wa Elimu Expo, Joel Njama (kulia) akizungumza na waandishi wa
habari wakati wa mkutano huo leo, Katikati ni Naibu Waziri wa Elimu,
Phillip Mulugo, na Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom,
Kelvin Twissa.
Mkuu
wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa,
akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano huo leo, Katikati
ni Naibu Waziri wa Elimu, Phillip Mulugo, na Mkurugenzi Mkuu wa Elimu
Expo, Joel Njama. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPO CHINI
Sehemu ya waandishi wa habari, waliohudhuria mkutano huo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa makini kumsikiliza Naibu Waziri wa Elimu.
Naibu Waziri, wakati akizungumza na wanahabari hao leo.
Picha ya pamoja kwa kumbukumbu.
**********************************************************
Mji wa Dar es salaam umeandaliwa kuwa mwenyeji wa maonyesho ya elimu ya kwanza ya aina yake mwaka huu, katika uwanja utakaoruhusu muingiliano na majadiliano kati yawatengenezaji wa sera, wapenda maendeleo, watunzi mbalimbali, wazazi, wanafunzi, na jamii kwa ujumla.
Maonyesho hayo yaliyopewa jina la Vodacom Elimu Expo, yanalenga kuwahusisha wadau wote wa elimu katika kuangalia mianya iliyopo, kugundua changamoto na kutafutia suluhisho ili kupelekea elimu bora kwa Watanzania kwa ujumla.
Ni tukio litakalochukua siku tatu kuanzia tarehe 30 mwezi wa nane mwaka 2013 na litafanyikia viwanja vya michezo vya Posta Kijitonyama, Dar es salaam.
Wasemaji mbalimbali kutoka mashirika na viwanda tofauti wataongelea kuhusu viwanda vyao na vilevile kukutana na watu ambao wanapenda makampuni yao na bidhaa zao.
“Maonyesho haya ya kujivunia yamepewa maudhui yasemayo ‘Elimu Bora ndio Tegemeo la Watoto wetu, Tuijenge kwa Pamoja.’ Tunawasihi wadau wa elimu kujitokeza kwa wingi katika maonyesho haya.
Elimu ndiyo ufunguo wa maendeleo katika taifa hili kubwa, na kusaidia elimu katika nyanja tofauti ndio kubwa tunaloweza kufanya”, alisema Njama, Mkurugenzi Mkuu wa maonyesho haya.
Pia aliongezea kuwa wageni zaidi ya 150,000 wanatarajiwa kuhudhuria katika maonyesho haya, wakiwepo pia wasanii na waburudishaji mbalimbali katika umati huo wa watu.
Akiongea wakati akitangaza udhamini wa maonyesho hayo Dar es salaam, Kelvin Twissa, Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa Vodacom, alielezea matumaini yake kuwa Vodacom Elimu Expo itasaidia kusuluhisha changamoto mbalimbali zinazokabili sekta ya elimu hapa nchini.
Moja ya changamoto hizo kubwa ni ile ya kulipa ada ya shule, ambalo limeonekana ni jambo la kuchosha sana na kupoteza muda katika mistari mirefu ya benki.
“Ni jambo la kusikitisha kabisa kuchelewa kulipa ada ya shule kwa sababu ya foleni zilizopo katika benki zetu.
Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom imekuja na njia ya kuitatua changamoto hii. Sasa hivi kuna uwezekano wa kulipa ada ya shule kupitia M-Pesa. Tunawasihi wadau wa elimu wanaomiliki shule kuanza kutumia huduma hii,” alisema Twissa.
Maneno hayo pia yalisisitizwa na Mheshimiwa Philip Mulugo, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, ambaye pia alisema serikali ina jukumu la kuhakikishia elimu bora wananchi wake na katika hali ambayo kila mtu anaweza kugharamia.
“Hii ni fursa kwa wale wote ambao wanajadili na kuja na suluhisho ambalo litapelekea elimu Tanzania kuendelea katika njia iliyo bora. Serikali itatoa kila kinachohitajika ili kufanikisha
jambo hili,” alisema Mulugo.
Vodacom Elimu Expo, tukio lililoandaliwa na Masoko Agencies Tanzania Limited, ni tukio linalokusudia kushawishi ubora na mabadilishano ya habari na majadiliano ya kielimu ambayo yanalenga katika uboreshaji wa ngazi za kielimu Tanzania.
Baadhi ya wadhamini wa maonyesho haya ni, Clouds FM, DTV, Entertainment Masters, Mwananchi Communications Ltd, Times FM, Primebiz Solutions Ltd, na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
*************************************
Kuhusu Vodacom Tanzania
Vodacom Tanzania ni kampuni inayoongoza kwa mawasiliano ikiwapa ubunifu wa mawasiliano ya GSM nchini kote.
Kampuni
ya Vodacom Tanzania ni ni kampuni shiriki ya Vodacom (Pty) ltd. South
Africa ambayo pia ni kampuni shiriki ya Vodafone Group UK. Vodacom Group
( Pty) wanamiliki hisa asilimia 65, na zingine 35 zikimilikiwa na
Mirambo Ltd.
Vodacom Tanzania imepewa heshima ya kuwa kampuni bora kuliko zote katika miaka iliyofuatana kuanzia 2009 -2012.
Vodacom Tanzania ina matawi makuu 6 Dar es salaam na maduka tegemezi 66 nchini kote.
Vodacom Tanzania Limited ni kampuni ya wananchi na ipo kusaidia jamii kwa kupitia Vodacom foundation.
Vodacom
foundation ina nguzo kuu tatu ambazo ni, afya, elimu na mambo ya jamii.
Mfuko wa Vodacom foundation umesaidia zaidi ya miradi 120 ndani ya nchi
na imeshinda tuzo za kitaifa na kimataifa kwenye tuzo za usaidiaji wa
jamii ambazo ni East African CSR Awards na Diversion na Inclusion Awards
ambayo hutolewa na Vodafone group iliyopo Milan.
Wasiliana na: Georgia Mutagahywa, Mkuu: Idara ya Mawasiliano, 0754 711 215
Kuhusu
Muandaaji Vodacom Elimu Expo, tukio lililoandaliwa na Masoko Agencies
Tanzania Limited, ni tukio linalokusudia kuwashawishi ubora wa
mabadilishano ya habari na majadiliano ya kielimu ambayo yanalenga
katika uboreshaji wa ngazi za kielimu Tanzania.
Kuunganisha
malighafi za kielimu zilizopo nchini na ukuaji wa teknologia ilikuwa
chanzo kikubwa cha waandaaji kwa kuwa walitarajia kutumia nyenzo
zillizopo katika huduma za mawasiliano katika kukuza jamii yenye uelewa
wa mambo.
Masoko
Agencies Tanzania Limited wanalenga katika kuwafi kishia watu elimu na
kuwafanya watu wajishirikishe katika nyanja za elimu.
Tunalenga
katika kuendeleza ajenda ambazo watunzi mbali mbali na wasomaji,
wawekezaji na wadhamini, pia wazazi na watengeneza sera mbalimbali
watakaa pamoja na
kujenga jamii yenye uelewa.
Kufanya
kazi na taasisi zote za elimu zikiwepo shule, vyuo, na vyuo vikuu
Tanzania, tunalenga kukuza ufaulu kwa kuzijua changamoto wanazokumbana
nazo na pia kikubwa zaidi kuziletea suluhisho changamoto hizo.
MSTAHIKI MEYA JERRY SILAA KUPITIA MDAU AKABIDHI VIFAA KWA AL - MADRASSATUL MUNAUWARATUL ISLAMIYA CHA MSASANI BONDE LA MPUNGA.
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akizungumza na uongozi wa Al
Madrassatul Munauwaratul Islamiya iliyopo Msasani Bonde la Mpunga
Ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla fupi ya kukabidhi
Spika mbili, Vipaza sauti viwili (Microphones) pamoja na Amplifaya
ambavyo vitatumika kuendeshea shughuli mbalimbali za kueneza mafunzo ya
dini kwa jamii na watoto wanaosoma chuoni hapo. Vifaa hivyo vimetolewa
na mdau mpenda maendeleo kupitia kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala
Jerry Silaa.
Pichani
juu na chini ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa pamoja
na Bw. Abdulmalik Ibrahim (kulia) aliyemwakilishi mdau aliyetoa vifaa
hivyo (jina kapuni) wakikabidhi Spika tatu, vipaza sauti viwili na Mixer
kwa Katibu wa Madrasa hiyo Bw. Salim Amri (wa pili kushoto)
aliyeambatana na Ustaadh Nurdin Nassor Abdallah (katikati). Kushoto ni
mmoja wa walimu wa madrassatul Munauwaratul Islamiya kilichopo Msasani
Bonde la Mpunga Ustaadh Mohamed Kassim.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akikagua moja vifaa hivyo alivyokabidhi leo ofisini kwake .
Ustaadh
Nurdin Nassor Abdallah wa Al Madrassatul Munauwaratul Islamiya ya
Msasani Bonde la Mpunga akitoa shukrani kwa Mstahiki Meya Jerry Silaa
pamoja na mdau alijitolea baada ya kupokea vifaa hivyo ambavyo amesema
vitawasaidia katika kazi zao za kueneza neno la Mungu hasa kipindi hichi
cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ikiwemo kuhubiri Amani nchini.
Uongozi
wa Al Madrassatul Munauwaratul Islamiya kilichopo Msasani Bonde la
Mpunga wakiomba dua za baraka kwa msaada waliopokea leo ofisini kwa
Mstahiki Meya Jerry Silaa.
MPAMBANO MWINGINE WA MASUMBWI KUFANYIKA IDI MOSI
kocha kwame mkuluma kulia akimwelekeza Bondia Iddy Kipandu 'Iddy Bonge' jinsi ya kutupa makonde mazito mazito Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Na SUPER D
Bondia Iddy Kipandu 'Iddy Bonge' yupo kambini kwa ajili ya kupambana na bondia Bahati Mwafyela
mpambano utakaofanyika siku ya sikukuu ya Idi Mosi jijini Dar es salaam katika ukumbi wa friends Corner Manzese
akizungumzia
maandalizi ya mpambano huo mtaalishaji Waziri Rosta amesema mpambano huo
wa uzito wa juu umekuwa gumzo katika jiji la Dar es salaam na vitongoji
vyake kwani mabondia hawo wanatafutana kwa mda mrefu sana na sasa
wamekutana kwa ajili ya mchezo huo
Mpambano huo wa
raundi 8 siwakukosa kwani ndio mpambano pekee kwa mwaka huu kukutanisha
uzito wa juu kwani mabondia wa uzito huu wanaotamba viwango vyao ni
vidogo ukizingatia kuwa wapo wachache nchini
aliongeza kuwa mbali na mpambano huo kutakuwa na mapambano mengine ya mabondia chipkizi na wanaotamba hapa nchini
Na kwa upande wa kocha anaemnoa bondia Iddy
Kipandu 'Iddy Bonge' amesema kuwa bondia wake alikuwa na manyama nyama
mengi lakini kwa sasa akuna kutokana na mazoezi anayompatia kwani kwa
sasa dozi yake ni kutwa mara tatu na mpaka siku ya mchezo naisi mambo
yatakuwa safi
Mpambano huo utakao sindikizwa na
mabondia Hassani Mandula atakae pambana na Twalib Mchanjo na Fadhili
Majia atakae menyana na Ally Mahiyo na Mustapha Doto atapambana na
Hashimu Mjeshi mapambano yote ya utangulizi itakuwa ni ya raundi sita
Siku hiyo kutakuwa na uhuzwaji wa DVD
mpya kwa ajili ya mafunzo ya mchezo wa masumbwi zitakazokuwa zikisabazwa
na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila
'Super D'
DVD hizo mpya ni kati ya
mike tyson vs evander holyfield na felix trinidad vs roy jones jr
Felix 'Tito' Trinidad vs Pernell Whitaker
ambapo dvd hizo zilizo rekodiwa kwa ubora wa hali ya juu kwa ajili ya kutoa mafunzo ya mchezo wa masumbwi nchin
Rajabu Mhamila 'Super D'
Photojournalist at Majira, Business Times
Mob;+255787 406938
Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania
Airtel yakabidhi milioni 14 kwa washindi wa promosheni ya Airtel yatosha.
Arusha.
Meneja wa airte Mauzo wa kanda ya kaskazini Stephen Akyooo akikabidhi shilingi milioni 1 kwa Bw, Robert Justine wa jijini Arusha fedha alizojishindia katika promosheni ya Airtel Yatosha inayoendeshwa na Airtel maalum kwa wateja wake wote wanaotumia huduma ya Airtel Yatosha kwa wiki, siku au mwezi mbapo pia mteja anaweza kujishindia moja kati ya Nyumba 3 za kisasa zilizopo dar es salaam.
Meneja wa airtel kanda ya kaskazini Stephen Akyoo akiwa na washindi wawili wa shilingi milion moja wa shindano la airtel yatosha kutoka mkoani Arusha bw, Robert Justine and Balistus Mambo. Washindi wote walikabidhiwa shilingi milioni moja kila mmoja walizojishindia katika promosheni ya Airtel yatosha na kuzitoa kwa Airtel Money.
======= ======= =====
Airtel yakabidhi milioni 14 kwa washindi wa promosheni ya Airtel yatosha.
• Ni washindi wa shilingi milioni moja wa wiki ya kwanza na ya
pili ya promosheni
• Ni washindi wa shilingi milioni moja wa wiki ya kwanza na ya
pili ya promosheni
Jumapili 28 julai 2013, kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetangaa na kuwazawadia washindi 14 wa kila siku wa promosheni ya Airtel yatosha shinda nyumba kila mmoja shilingi milioni moja pesa taslimu kupitia huduma ya Airtel Money.
Washindi hawa wamepatikana kupitia droo ya wiki ya kwanza na ya wiki ya pili ambapo jumla ya washindi 14 kutoka katika mikoa mbalimbali ya nchi walipatikana na hatimaye kukabithiwa pesa zao
Akiongea wakati wa kukabithi zawadi kwa washindi hao Meneja Mauzo wa
Kanda Mkoani Arusha bwana Stephen Akyoo alisema” leo tunayofuraha
kupata washindi wa promosheni ya Airtel yatosha na kuwakabithi zawadi zao. Washindi hawa wamepatikana kutoka katika mikoa mbalimbali na kujishindia kila mmoja shilingi milioni moja pesa taslimu kwa kutumia
huduma za Airtel yatosha na kujiunga na vifurushi vyetu mbalimbali. nae Meneja Uhusiano wa Airtel Akitangaza majina ya washindi hao bwana
Jackson Mmbando alisema "washindi wetu wa wiki ya kwanza na ya pili ni
pamoja na Hawa Said Mkazi wa Mtwara, John Masawe mkazi wa singida,
Joseph Emmanuel Nchimbi Songea, Rosemary Michael na John Masanja kutoka Tabora , Zuhura Sabuni kutoka Lindi, Balistus mambo kutoka Moshi, Robert Faustine kutoka Arusha , Frank Ladislaus na Paulina Michael kutoka Sengerema Mwanza, Flavian Adamson Malilo kutoka Katavi,
Jacob Muhole kutoka Dodoma, Singodi Severin kutoka Kagera na Ephrasia Thadeo kutoka Ngara.
Ili kushiriki mteja anatakiwa kupiga kupiga *149*99# na kununua kifurushi cha huduma ya Airtel yatosha cha siku, wiki au mwezi na kuunganishwa mojakwamoja kushiriki kwenye promosheni na kupata nafasi ya kushinda nyumba au pesa taslimu shilingi milioni moja kila siku.
Akiongea mara baada ya kukabithiwa zawadi hiyo Bwana Robert Justine moja kati ya washindi anayetokea mkoani Arusha alisema” nimefurahi
sana kuwa mshindi wa promosheni na ntaendelea kutumia huduma ya Airtel
yatosha ili kuendelea kufaidika na huduma hii na kupata nafasi ya
kushinda nyumba. Natoa wito kwa watanzania kutumia huduma hii na
kuhakikishia hata wao wananafasi ya kushinda kama mimi nilivyoweza
leo kukabithiwa shilingi milioni moja kwa kutumia tu huduma ya Airtel
yatosha. Promosheni ya Airtel yatosha bado inaendelea kwa mienzi mitatu hadi hapo mwishoni mwa mwenzi wa tisa ambapo mbali na zawadi za pesa taslimu wateja pia wanapata nafasi ya kujishindia nyumba 3 zilizopo kigamboni jijini Dar es saalam
DR. ALI MOHAMED SHEIN ALA FURATI NA WANANCHINI WA MKOA WA KUSINI UNGUJA
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed
Shein,(katikati) pamoja na Viongozi na wananchi na waumini wa Dini ya
Kiislamu wa Mkoa wa Kusini Unguja, wakijumuika katika chakula cha futari
aliyoiandaa katika viwanja vya Jengo la Ofisi ya Uhamiaji Tunguu jana. Baadhi
ya Wananchi na waumini wa Dini ya Kiislamu wakifurahi katika Viwanja
vya Ofisi ya Uhamiaji Tunguu,katika mualiko wa Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein, kwa
Wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja jana. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(kulia) akipeana mkono wa shukurani na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Alhaj Dk.Mohamed Gharib Bilal,baada ya futari aliyomualika jana huko katika viwanja vya Ofisi ya Uhamiaji Tunguu,Mkoa wa Kusini Unguja.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.
LHRC YATOA TAARIFA YA NUSU MWAKA YA MATUKIO MBALIMBALI NCHINI KUANZIA JANUARY-JUNE 2013
Mtafiti
wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Pasience Mlowe
(kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam jana Julai 29, 2013, wakati akitoa taarifa ya nusu mwaka ya
kuanzia Januari hadi Juni 2013 ya kituo hicho kuhusu mambo mbalimbali
yaliyotokea nchini. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uwezeshaji na Uwajibikaji wa Kituo hicho Imelda Urio.
Mkurugenzi wa Uwezeshaji na Uwajibikaji wa Kituo hicho Imelda Urio, akizungumza katika mkutano huo.
Mtafiti wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Pasience Mlowe (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana. Wengine ni watafiti wa kituo hicho
Mtafiti wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Pasience Mlowe (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana. Wengine ni watafiti wa kituo hicho
Sunday, July 28, 2013
MADA MAUGO NA BENSON MWAKYEMBE WACHEZEA VICHAPO TOKA KWA WARUSSIA
MAUGO |
BONDIA mada maugo mwishoni mwa wiki iliyopita alichezea kichapo kutoka kwa
Movsur
Yusupov
wa Russia katika mpambano uliopagwa kupigwa kwa raundi nane hata hivyo Maugo alipigwa kwa TKO ya raundi ya tano
ambapo Maugo alisalim amri kwa kupoteza mchezo huo ulifanyika katika viwanja vya Trade And Entertainment Centre "Moskva", Kaspiysk, Russia mwishoni mwa wiki iliyopita
Baada ya kupoteza mchezo uho August 30 atapanda tena uringoni
kukabiliana na Thomasi Mashali mpambano wa ubingwa wa WBF Africa uzito
wa kati mpambano utakaokuwa wa raundi 12 ambapo Maugo alisalim amri kwa kupoteza mchezo huo ulifanyika katika viwanja vya Trade And Entertainment Centre "Moskva", Kaspiysk, Russia mwishoni mwa wiki iliyopita
mwakyembe |
Nae bondia benson mwakyembe alikuwa na kibarua kizito siku hiyo hiyo nae alikubali kichapo cha K,O ya raundi ya 7 katika mpambano wa raundi 8
Mabondia wote wawili walionesha kuwa na viwango vya kutosha ila walizidiwa ufundi na maarifa ya mchezo wa masumbwi uringoni
Hata hivyo kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amekuwa akitoa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi akitumia mabondia kutoka mataifa yanayofanya vizuri katika mchezo huo ili kujua mbinu mbalimbali wanazotumia