Tuesday, July 30, 2013

DAR ES SALAAM KUWA MWENYEJI WA MAONYESHO YA VODACOM ELIMU EXPO 2013 VIWANJA VYA CHUO CHA POSTA KIJITONYAMA AGOSTI 30




 Naibu Waziri wa Elimu, Phillip Mulugo, akizungumza na waandishi wa habari, kwenye Ukumbi wa Kivukoni, Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo, wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa maonyesho ya siku tatu ya Vodacom Elimu Expo, yanayotarajia kuanza Agosti 30, mwaka huu katika Viwanja vya Michezo vya Chuo cha Posta, Kijitonyama jijini. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Elimu Expo, Joel Njama (kushoto) ni Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa. 

 Naibu Waziri wa Elimu, Phillip Mulugo (katikati) Mkurugenzi Mkuu wa Elimu Expo, Joel Njama (kulia) na  Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa, wakigonganisha glasi, kama ishara ya uzinduzi wa maonyesho hayo, wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Elimu Expo, Joel Njama (kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano huo leo, Katikati ni   Naibu Waziri wa Elimu, Phillip Mulugo, na Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa.
Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano huo leo, Katikati ni   Naibu Waziri wa Elimu, Phillip Mulugo, na Mkurugenzi Mkuu wa Elimu Expo, Joel Njama. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPO CHINI

 Sehemu ya waandishi wa habari, waliohudhuria mkutano huo.
 Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa makini kumsikiliza Naibu Waziri wa Elimu.
 Naibu Waziri, wakati akizungumza na wanahabari hao leo.
Picha ya pamoja kwa kumbukumbu.
**********************************************************
Mji wa Dar es salaam umeandaliwa kuwa mwenyeji wa maonyesho ya elimu ya kwanza ya aina yake mwaka huu, katika uwanja utakaoruhusu muingiliano na majadiliano kati yawatengenezaji wa sera, wapenda maendeleo, watunzi mbalimbali, wazazi, wanafunzi, na jamii kwa ujumla.

Maonyesho hayo yaliyopewa jina la Vodacom Elimu Expo, yanalenga kuwahusisha wadau wote wa elimu katika kuangalia mianya iliyopo, kugundua changamoto na kutafutia suluhisho ili kupelekea elimu bora kwa Watanzania kwa ujumla.

Ni tukio litakalochukua siku tatu kuanzia tarehe 30 mwezi wa nane mwaka 2013 na litafanyikia viwanja vya michezo vya Posta Kijitonyama, Dar es salaam.

Wasemaji mbalimbali kutoka mashirika na viwanda tofauti wataongelea kuhusu viwanda vyao na vilevile kukutana na watu ambao wanapenda makampuni yao na bidhaa zao.

“Maonyesho haya ya kujivunia yamepewa maudhui yasemayo ‘Elimu Bora ndio Tegemeo la Watoto wetu, Tuijenge kwa Pamoja.’ Tunawasihi wadau wa elimu kujitokeza kwa wingi katika maonyesho haya. 

Elimu ndiyo ufunguo wa maendeleo katika taifa hili kubwa, na kusaidia elimu katika nyanja tofauti ndio kubwa tunaloweza kufanya”, alisema Njama, Mkurugenzi Mkuu wa maonyesho haya.

Pia aliongezea kuwa wageni zaidi ya 150,000 wanatarajiwa kuhudhuria katika maonyesho haya, wakiwepo pia wasanii na waburudishaji mbalimbali katika umati huo wa watu.

Akiongea wakati akitangaza udhamini wa maonyesho hayo Dar es salaam, Kelvin Twissa, Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa Vodacom, alielezea matumaini yake kuwa Vodacom Elimu Expo itasaidia kusuluhisha changamoto mbalimbali zinazokabili sekta ya elimu hapa nchini.

Moja ya changamoto hizo kubwa ni ile ya kulipa ada ya shule, ambalo limeonekana ni jambo la kuchosha sana na kupoteza muda katika mistari mirefu ya benki.

“Ni jambo la kusikitisha kabisa kuchelewa kulipa ada ya shule kwa sababu ya foleni zilizopo katika benki zetu. 

Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom imekuja na njia ya kuitatua changamoto hii. Sasa hivi kuna uwezekano wa kulipa ada ya shule kupitia M-Pesa. Tunawasihi wadau wa elimu wanaomiliki shule kuanza kutumia huduma hii,” alisema Twissa.

Maneno hayo pia yalisisitizwa na Mheshimiwa Philip Mulugo, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, ambaye pia alisema serikali ina jukumu la kuhakikishia elimu bora wananchi wake na katika hali ambayo kila mtu anaweza kugharamia. 

“Hii ni fursa kwa wale wote ambao wanajadili na kuja na suluhisho ambalo litapelekea elimu Tanzania kuendelea katika njia iliyo bora. Serikali itatoa kila kinachohitajika ili kufanikisha
jambo hili,” alisema Mulugo.

Vodacom Elimu Expo, tukio lililoandaliwa na Masoko Agencies Tanzania Limited, ni tukio linalokusudia kushawishi ubora na mabadilishano ya habari na majadiliano ya kielimu ambayo yanalenga katika uboreshaji wa ngazi za kielimu Tanzania.

Baadhi ya wadhamini wa maonyesho haya ni, Clouds FM, DTV, Entertainment Masters, Mwananchi Communications Ltd, Times FM, Primebiz Solutions Ltd, na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
*************************************
Kuhusu Vodacom Tanzania
Vodacom Tanzania ni kampuni inayoongoza kwa mawasiliano ikiwapa ubunifu wa mawasiliano ya GSM nchini kote.

Kampuni ya Vodacom Tanzania ni ni kampuni shiriki ya Vodacom (Pty) ltd. South Africa ambayo pia ni kampuni shiriki ya Vodafone Group UK. Vodacom Group ( Pty) wanamiliki hisa asilimia 65, na zingine 35 zikimilikiwa na Mirambo Ltd. 

Vodacom Tanzania imepewa heshima ya kuwa kampuni bora kuliko zote katika miaka iliyofuatana kuanzia 2009 -2012.

Vodacom Tanzania ina matawi makuu 6 Dar es salaam na maduka tegemezi 66 nchini kote.

Vodacom Tanzania Limited ni kampuni ya wananchi na ipo kusaidia jamii kwa kupitia Vodacom foundation.

Vodacom foundation ina nguzo kuu tatu ambazo ni, afya, elimu na mambo ya jamii. Mfuko wa Vodacom foundation umesaidia zaidi ya miradi 120 ndani ya nchi na imeshinda tuzo za kitaifa na kimataifa kwenye tuzo za usaidiaji wa jamii ambazo ni East African CSR Awards na Diversion na Inclusion Awards ambayo hutolewa na Vodafone group iliyopo Milan.

Wasiliana na: Georgia Mutagahywa, Mkuu: Idara ya Mawasiliano, 0754 711 215
Kuhusu Muandaaji Vodacom Elimu Expo, tukio lililoandaliwa na Masoko Agencies Tanzania Limited, ni tukio linalokusudia kuwashawishi ubora wa mabadilishano ya habari na majadiliano ya kielimu ambayo yanalenga katika uboreshaji wa ngazi za kielimu Tanzania.

Kuunganisha malighafi za kielimu zilizopo nchini na ukuaji wa teknologia ilikuwa chanzo kikubwa cha waandaaji kwa kuwa walitarajia kutumia nyenzo zillizopo katika huduma za mawasiliano katika kukuza jamii yenye uelewa wa mambo.

Masoko Agencies Tanzania Limited wanalenga katika kuwafi kishia watu elimu na kuwafanya watu wajishirikishe katika nyanja za elimu. 

Tunalenga katika kuendeleza ajenda ambazo watunzi mbali mbali na wasomaji, wawekezaji na wadhamini, pia wazazi na watengeneza sera mbalimbali watakaa pamoja na
kujenga jamii yenye uelewa.

Kufanya kazi na taasisi zote za elimu zikiwepo shule, vyuo, na vyuo vikuu Tanzania, tunalenga kukuza ufaulu kwa kuzijua changamoto wanazokumbana nazo na pia kikubwa zaidi kuziletea suluhisho changamoto hizo.

No comments:

Post a Comment