Na Elizabeth John
MSANII
nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Dully Sykes amewashauri wasanii
wenzake kuitafuta zaidi elimu ya darasani ili iweze kuwasaidia katika
suala zima la wizi wa kazi zao.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam, Dully alisema wasanii wengi wa bongo fleva wanabebwa na vipaji walivyo navyo, si elimu.
“Kunawasanii
hapa Tanzania wanaibiwa kazi zao kila siku kwa sababu hawajasoma na
hawaelewi mikataba na mambo mengi tu, wanabaki kudhulumiwa na mameneja
wao,” alisema Dully.
Alisema jasho la wasanii huibiwa kila siku hususani mauzo ya albamu na miito ya simu sababu ni kukosa elimu.
Nyota
huyo ambaye anamiliki studio mbili za kurekodi muziki, Dhahabu record
na 4.12 record alisema wasanii wa bongo wanatakiwa wasome ili muziki
wetu ufike mbali na sio kuishia hapa.
Alisema
kutokana na kuufahamu umuhimu wa elimu anatamani apate mwalimu wa
kumfundisha nyumbani kutokana na kukosa nafasi ya kwenda darasani.
No comments:
Post a Comment