Wednesday, July 10, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AFUNGUA MKUTANO WA MABUNGE WA KUJADILI SERA ZA MISITU BARANI AFRIKA


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Mkutano wa Mabunge wa kujadili Sera za Misitu Barani Afrika, uliofanyika jana jioni Julai 9, 2013 kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam.Picha na OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mkurugenzi wa Baraza la Dunia ya baadaye wa Dunia, 'World Future Council' Alexandra Wandel, wakati alipowasili kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, jana jioni Julai 9, 2013 kwa ajili ya kufungua Mkutano wa Mabunge wa kujadili Sera za Misitu Barani Afrika, uliohudhuriwa na wabunge mbalimbali kutoka Bara la Afrika.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wabunge waliohudhuria Mkutano Mabunge wa kujadili Sera na changamoto za Misitu Barani Afrika.
  Mkurugenzi wa Baraza la Dunia ya baadaye wa Dunia, 'World Future Council' Alexandra Wandel,akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.
 Baadhi ya Wabunge wakiwa katika chumba cha mkutano huo, kutoka (kushoto) ni Mbunge wa Kahama James Lembeli, Mbunge wa Mafia, Abdulkarim Shah, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, wakiwa katika mkutano huo 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (katikati) akiwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, (wa pili kulia) Mkurugenzi wa Baraza la Dunia ya baadaye wa Dunia, 'World Future Council' Alexandra Wandel (wa pili kushoto) na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Getrude Mongela (kulia) wakifuatilia moja ya mada zilizokuwa zikitolewa ukumbini hapo kupitia Screen kwa njia ya TV. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (katikati) na Getrude Mongela, baada ya kufungua rasmi mkutano huo jana Julai 9, 2013 jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment