Saturday, July 20, 2013

MBASPO YANYAKUA UBINGWA WA KOMBE LA MUUNGANO MUFINDI 2013 YAITOA MBEYA CITY KWA MATUTA 5-4


Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Angetile Osiah  akikabidhi kombe la  ubingwa  kwa  timu ya  Mbaspo  kutoka Mbeya  baada ya  kufanikiwa  kushindwa  kwa  mikwaju ya penati 5-4 dhidi ya  wahasimu  wao Mbeya City katika faili ya kombe la Muungano Mufindi 2013 na kunyakua kombe na pesa kiasi cha Tsh milioni 3
 Mwenyekiti  wa chama cha  soka mkoa  wa Mbeya kushoto akiwa na mmoja kati ya  wachezaji wa  timu ya Mbaspo wakionyesha  kombe la ubingwa  leo katika  uwanja  wa  shule ya Msingi  Wambi mjini Mafinga
 Mabingwa  wa mashindano ya  kombe la Muungano Mufindi mwaka 2013 timu ya Mbaspo ya Mbeya  katika  picha ya pamoja na mashabiki wageni  rasmi na  wadhamini   jioni ya leo katika  uwanja  wa Wambi mjini Mafinga
Timu ya  Mbaspo kutoka mkoani  Mbeya  leo  imeibuka bingwa  wa mashindano ya kombe la Muungano  2013  baada ya  kuigagadua  kwa  jumla ya mikwaju ya  paneta  5-4 timu ya Mbeya  City  katika  mchezo  wa fainali  uliochezwa katika  uwanja wa  Shule ya  Msingi  Wambi mjini Mafinga  mchezo  ulioshuhudiwa na mgeni  rasmi Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Angetile Osiah.
Katika  mchezo  huo   timu  zote mbili ziliweza  kuonyesha soka kali  lililofanya  mashabiki kujigawa  katika  kuzishangilia  timu hizo ambazo zote mbili  zilikuawa katika uwanja  wa ugenini.
Mbali ya  timu ya  Mbeya  City kujipatia mashabiki  wengi  kipindi cha kwanza  wa  kuishangilia ila hali  iligeuka na mashabiki robo  tatu ya  uwanja  kuamua  kuelekeza ushabiki  wao kwa  timu ya Mbaspo kutokana na  viungo  wake  nambali 4 na 14  mgongoni  kuuteka  uwanja  huo kwa  soka  safi.
Hadi  timu  zote  mbili  zinakwenda mapumziko kipindi cha kwanza  hakuna  timu  iliyobahatika kuchungulia  lango la mwenzake .
Kasi ya mchezo  ilionekana  kubadilika kipindi cha  pili kwa  timu  zote kukamiana  bila mafanikio  hadi mwamuzi wa mchezo  huo alipopuliza filimbi ya mwisho  kuhitimisha  mchezo huo bila bingwa  kupatikana .
Ili  kuwa kazi ngumu katika upigaji mikwaju ya penati ambapo  timu ya Mbeya  City  ilijikuta  akipoteza  nafasi  moja na  kutoa nafasi kwa  timu ya Mbaspo ambao walijipanga  vema na kufanikiwa  kuingiza nyavuni mikwaju yote  mitano na  hivyo  kufanikiwa  kuibuka  bingwa kwa kuingiza nyavuni mikwaju 5-4 na kufan ikiwa  kutangazwa mabingwa katika michuano  hiyo.
Katika mashindano  hayo mshindi  wa kwanza  timu ya  Mbaspo imekabidhiwa  pesa kiasi cha  Tsh milioni 3  Mendani na  kombe ,mshindi wa  pili Mbeya City  akinyakua mendani na Tsh milioni 1.5 wakati  mwamuzi  bora na mchezaji  bora  kila mmoja  akinyakua Tsh 400,000

Mratibu  wa mashindano  hayo Daud Yassin Amewapongeza  wadhamini  wa mashindano  hayo ikiwemo kampuni ASAS LTd ya  Iringa,kampuni ya Mwananchi Communication,NSSF,Pareto,Ibrahim Khamis, PPF,MUcoba Benk na  Chai Bora kwa  kufanikisha  mashindano  hayo.

No comments:

Post a Comment