Monday, July 1, 2013

REDD’S MISS MOROGORO 2013 AONGEZA CHEO BAADA YA KUTWAA NA TAJI LA KANDA MASHARIKI.


 Redd’s Miss Kanda ya Mashariki 2013, Mwanafunzi  wa mwaka wa kwanza wa  Shahada ya Ulinzi wa Jamii  kutoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha ( IFM) ambaye pia ni Malikia wa Taji la Mkoa wa Morogoro  Diana Laizer (21) ( kati kati) akiwa na wenzake mshindi wa pili  , Sabra Islam (19) ( Kushoto) pia kutoka Mkoa wa Morogoro pamoja na mshindi wa tatu Janeth Awet ( 19) kutokaMkoa wa Lindi  mara baada ya kutagazwa washindi katika shindano lao lililofanyika Juni 29, mwaka huu.

 Madensa wa Kundi la Msanii wa kizazi kipya Tundaman, wakishambulia jukwaa.
 Baadhi ya washiriki wa Redd's Miss Kanda ya Mashariki 2013, wakiwa katika vazi la jioni.
Mshindi wa nne , Redd's Miss Kanda ya Mashariki 2013, Elizabeth Perty kutoka mkoa wa Pwani akipita jukwaani na vazi la ubunifu.
********************************************
Na Mwandishi Wetu, Morogoror
MWANAFUNZI wa mwaka wa kwanza wa Shahada ya Ulinzi wa Jamii kutoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha ( IFM), Diana Laizer (21) amefanikiwa kunyakua taji la Redd’s Miss Kanda ya Mashariki baada ya kuwashinda wenzake 12 walioshiriki kuwani taji hilo mwaka 2013. 
 Mshindi huyo ambaye pia ni malkia wa taji la Redd’s Miss Morogoro 2013 akiwa amevalia namba sita ya ushiriki ,amefanikiwa kuchukua mikoba ya mtangulizi wake Rose walifanikiwa kunyakua taji hilo juzi usiku katika ukimbi wa Nashera Hoteli wa Mjini hapa baada ya kutangazwa na majaji wa shindano hilo. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPO CHINI
 Jaji Mkuu , Albert Makoye ambaye ni Mkuu wa Itifaki wa Miss Tanzania, mbali na kumtangaza malkia wa Kanda ya Mashariki , alimtangaza pia mshiriki kutoka mkoa wa Morogoro Sabra Islam (19) kushika nafasi ya pili katika kinyang’anyiro hicho. 
 Sabra aliingia kwenye shindano hilo baada ya kushika nafasi ya pili katika shindano ya Redd’s Miss Morogoro 2013 ambaye pia ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe. Kwa mujibu wa Jaji Mkuu huyo, mshindi wa tatu wa Redd’s Miss Kanda ya Mashairiki ilitwaliwa na mrembo Janeth Awet ( 19) kutoka Mkoa wa Lindi na nafasi ya nne ilinyakuliwa na mrembo Elizabeth Perty (22) kutoka Mkoa wa Pwani. Makoye alisema kutokana na washiriki wa kinyang’anyiro hizo Kanda ya Mshariki kuwa na warembo karibu wote wenye sifa na vigezo, 
Kamati ya Miss Tanzania imeamua kuwachukua washiriki wanne kuingia katika kambi ya shindano ya Miss Tanzania mwaka huu. Hata hivyo alimtaja mwingine aliyeingia tano bora ni Ivon Stephen (22) kutoka Mkoa wa Mtwara , ambapo wengi walioshiriki na mikoa yao katika mabano ni Zulfa Semboja (19) ( Mtwara) na Pulkeriah Ndovi (21) ( Mtwara). 
 Wengine ni Sophia Maganga (21), Lindi, Zainabu Shaaban (23) (Lindi), Lilian Joseph (21) ,(Pwani ) Easther Albert (20) ( Pwani), Muzne Abduly ( 19) na Ummy Mohamed (21) wote ni kutoka Mkoa wa Morogoro. Naye Mratibu wa Shindano hilo, Alex Nikitas, aliwakabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza sh: 600,000, Mshindi wa pili sh: 400,000 na mshindi wa tatu sh: 300,000 , ambapo mshindi wanne na watano walipatiwa sh: 200,000 kila mmoja na wengine waliobakia kusawadiwa sh: 100,000 kila moja.
 Katika shindano hilo, Mgeni rasmi alikuwa ni Mbunge wa Jimbo la Kilosa , Mustafa Mkulo na pia kuhudhuriwa na viongozi kadhaa akiwemo na Mbunge wa Jimbo la Gairo , Ahmed Sabiby pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali , Jaji Frederick Werema ambapo pia mwanamuziki wa kizazi kipya Tunda Man walitumbuiza likiwemo na kundi la sanaa la Wanne Star.
MC katika shindano la kumpata malkia wa Taji la Redd's Miss Kanda ya Mashariki Kaka Aidan Ricco ambaye ni Afisa Habari wa Kamati ya Miss Tanzania  akielezea utaratibu wa kuwapata washindi watano.
 Mshiriki Zulfa Semboja kutoka mkoa wa Mtwara akionesha vazi la ubunifu mbele ya watazamaji
Washindi wanne wa Redd's Miss Kanda ya Mashariki 2013 wakisubiri Jaji Mkuu kutaja majina yao katika nafasi ya ushindi kuanzia kwanza, pili , tatu na ya nne.
 Mwanamuziki wa Kike wa kizazi kipya, Keisha ( wa kwanza kulia) akipiga makofi kufurahiamchuano wa warembo wa Redd's Miss Kanda Mashariki , Juni 29, mwaka huu
 Redd's Miss Kanda ya Mashariki 2013 yenye taji kishwani akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wenzake waliokuwa wameingia tano bora.
 Redd's Miss Kanda ya Mashariki 2013, Diana Laizer akifurahia kitita cha fedha alichokabidhiwa na Mbunge wa Jimbo la Kilosa, Mustafa Mkulo baada kutangazwa mshindi.

No comments:

Post a Comment