Tuesday, July 23, 2013

SOBER HOUSE YAENDELEA KUTOA MBINU MBALIMBALI JUU YA KUACHA MADAWA YA KULEVYA KWA VIJANA WANAOUTUMIA MADAWA YA KULEVYA


Vijana wa walioacha kutumia dawa za kulevya wakiomba dua kabla ya kuzungumza  na mwandishi wa habari hizi Dotto Kahindi wa kwanza kulia
Idadi kubwa ya vijana wanaojiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya inaweza kupungua ama kuisha kabisa endapo waathirika wa utumiaji wa dawa hizo watatumika kutoa elimu kwa vijana wenzao ambao bado
hawajaingia katika janga hilo ambalo ni hatari sana kwa nguvu kazi ya taifa.
 

Tone Media kupitia TANGA YETU imefika katika kituo cha watumiaji wa dawa za kulevya (Rehab, SOBER HOUSE) jijini Tanga ambao wanatoa mbinu na elimu ya kutorudia kutumia dawa hizo ambazo zinaathiri na kugharimu maisha ya vijana wengi.

 Mwenyekiti wa SOBER HOUSE, Ibrahim Daga akifafanua jambo kwa mwandishi wa habari (hayupo pichani)

Vijana wadogo ambao pengine
sasa wangekuwa wakilitumikia taifa katika mambo mbalimbali walijikuta katika janga
hili la dawa za kulevya kutokana na sababu mbalimbali wengine wakirubuniwa na
marafiki, tamaa, kwenda na wakati, unywaji pombe na uvutaji bangi ambao
uliwapeleka moja kwa moja katika matumizi ya dawa hizo.
Ibrahimu Daga ambaye ni
Mwenyekiti wa Rehab SOBER HOUSE jijini Tanga anasema kituo hicho hulea watu 35
na kuwapatia elimu ya namna ya kuishi bila kurudia matumiazi ya dawa hizo,
mafunzo ambayo hudumu kwa miezi minne.
Anasema kuwa kituo hicho hakijapata
msaada wowote kutoka serikalini hasa mamlaka zinazohusika na dawa za kulevya na
kwamba kinajiendesha kwa michango ya wazazi wa waathirika.
“Tunahitaji sana kuungwa mkono
na serikali hasa katika upande wa kupata chakula kwa hawa vijana tulionao,
lakini katika mipango ya muda mrefu tunahitaji eneo kubwa kwajili ya kujenga
Rehab itakayochukua watu wengi zaidi” anaeleza Ibrahim


Meneja wa Rehab hiyo Salum
Amour anasema mahitaji makubwa katika rehab hiyo ni kupata elimu ya
ujasiliamali, biashara, kilimo na ufugaji kwa waathirika hao ili baada ya
kumaliza muda wa Rehab wawe na uwezo wa kuendesha maisha yao hata baada ya
kurejea katika hali zao za kawaida.


Miongoni mwa shughuli wanazojifunza ni usafi na kupika

 Vijana hawa wanatoa ujumbe
mzito kwa vijana wenzao, wakisema USIJARIBU KUFIKIRIA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA
NI HATARI.
Meneja wa Rehab hiyo Salum Amour (mwenye t-sheirt nyekundu) akizungumza na mwandishi wa habari

Nyumba inayotumika kuhifadhia vijana hao
Viongozi wa serikali kuanzia
ngazi ya Wilaya, Mkoa na Kitaifa ni jukumu lenu sasa kuhakikisha kuwa mnaunga
mkono jitihada za Rehab hii kwa kusaidia kuboresha hudumu ikiwemo chakula ili
malengo ya kumaliza tatizo la mateja mitaani yafanikiwe, PESA ZA DAWA ZA
KULEVYA NA UKWIMWI ZINAKWENDA WAPI??? Walengwa ndio hawa hamuwaoni?


Picha Zote na Tanga Yetu

No comments:

Post a Comment