Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, July 10, 2013

SONGAMBELE: NILINUSURIKA KUFUNGWA KWA KUMCHEKESHA RAIS


DAR ES SALAAM, Tanzania

Muasisi wa TANU Mustafa Mohammed Songambele (Pichani), amesema aliwahi kunusrika kufungwa kwa sababu ya kumchesha rais, Mwalimu Julius Nyerere.

Akizungumza na baadhi ya wafanyakazi katika Idara ya Itikadi na Uenezi, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo, Songamebele (88), alisema, mwaka 1970, wakati huo akiwa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam na pia Katibu wa TANU wa mkoa huo, alienda nyumbani kwa Mwenyekiti wa Chama, Mwalimu Nyerere, kwa ajili ya mazungumzo maalum.

Alisema, wakiwa katika mazungumzo alitamka maneno ambayo yalimfanya Mwalimu Nyerere kucheka hadi kudondoka sakafuni huku akibubujiwa machozi kwa kicheko.

Mzee Songambele alisema, baada ya rais kuondoka kwenda ofisini kwake, maofisa usalama walimsogelea na kumhoji kwa nini umemchekesha rais mpoaka amedondoka chini? Yaani ulitaka Rais afe halafu tupate tatizo la kutoa maelezo kwamba wewe umemchekesha hadi kufa? inabidi tukukamate uwekwe ndani.

Alisema, baada ya Walizni kusema, hayo alilazimika kujitetea akisema "Mimi nilizungumza tu, sikuwa najua kwamba Mwalimu atacheka sana kiasi kile, sasa hili siyo kosa langu naomba mnisamehe".

"Nilipoona wanatafakari kidogo nipanda ngazi hadio ofisini kwa rais, nikamkuta, akasema, 'bwana nimeshacheka sana inatosha basi", nikamwambia Mwalimu mimi sikuja kukuchekesha tena, lakini tazama hawa walinzi wanataka kuniweka ndani kwa sababu wewe umefurahi ukacheka, sasa nimefanya kosa gani?", aliseleza Mzee Songambele.

Alisema, baada ya Mwalimu kusikia malalamiko hayo, aliwaita walinzi na kuwaamuru wamwache huru ndiyo ikawa salama yake, akaondoka.

Akizungumza na wafanyakazi hao, Songambele alikitabiria Chama Cha Mapinduzi kuendelea kutawala kwa muda mrefu licha ya kuwepo kwa vyama vingi, akisema uhakika huo unatokana na CCM kuwa na historia ambayo kufutika kwake si rahisi.

Songambele aliwataka CCM kujiimarisha zaidi ili kuendeleza misingi hiyo ya Chama kwa ajili ya kuhakikisha hakiyumbi wala kuyumbishwa kwa namna yoyote na wimbi la upinzani na kwamba kujenga misingi hiyo, vijana wana nafasi kubwa zaidi. Chanzo: CCM Blog

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...