Tuesday, July 2, 2013

TANZANIA YAJITOA KLABU BINGWA AFRIKA MASHARIKI



Na Elizabeth John
TIMU za Tanzania zimejitoa kushiriki mashindano ya klabu bingwa ya Afrika Mashariki katika mchezo wa Netiboli.
Timu hizo ni ambazo zilitakiwa kushiriki mashindano hayo ni Filbert Bayi, JKT Mbweni na Jeshi Stars.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA), Annie Kibira alisema kila timu imejitoa kushiriki mashindano hayo kwa sababu mbalimbali.
“Kila timu imejitoa kwa sababu yake, ni vigumu kuelezea sababu, hivyo hatutashiriki mashindano hayo kwasasa tunajiandaa na mashindano ya klabu bingwa ya taifa,” alisema Kibira.
Alisema klabu zote ambazo zinatarajia kushiriki mashindano ya klabu bingwa ya taifa, zinatakiwa kujiandaa na mashindano hayo ambayo yanatarajia kuanza kutimua vumbi Agosti 24 jijini Mbeya.
“Klabu 20 zinatarajia kushiriki mashindano hayo, timu zinatakiwa zianze maandalizi mapema ili kuweka mashindano hayo kuwa ya kishindani zaidi,” alisema.

No comments:

Post a Comment