Saturday, July 20, 2013

WASANII BONGO WASHAURIWA KUHESHIMU VIDEO ZAO



Na Elizabeth John


WASANII wa Tanzania wameshauriwa kufuata maadili ya nchi katika video za nyimbo zao ili wasipoteze sifa ya nchi katika vizazi vijavyo.
Baadhi ya wasanii wamekua wanawatumia wakinadada mbalimbali kwaajili ya kupendezesha video hizo huku wakivaa nguo za ajabu ambazo kiukweli kiutamaduni haipendezi.
Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaaam hivi karibuni na msanii anayeibukia katika fani ya muziki wa hip hop nchini, Emmanuel Peter Sahani ‘Plate’ ambapo alisema baadhi ya video za  Tanzania zinaidhalilisha nchi yetu.
“Kiukweli haipendezi hata kidogo video zingine huwezi kuangalia mbele za wazazi wako maana mambo yanayooneshwa humo yanatisha, tunawaharibu watoto ambao kila wakati hupenda kuangalia video za wasanii wa bongo, kazi ya msanii ni kuelimisha jamii na sio kupotosha,” alisema.
Alisema utandawazi ndio unaharibu maisha ya vijana wa Tanzania, maana kila kijaan ambaye ataangalia jinsi nchi za wenzetu wanavyovaa nae atataka ajaribu yeye atatokaje.
“Wnawadharirisha sana dada zetu, video ya wimbo sio lazima avae nguo za ajabu ambazo lazima mtu ajiulize atakapomuona mbona wanapovaa nnguo za maadili zinapendeza, jamani Watanzania tubadilike tunaaribu kizazi kijacho,”alisema

No comments:

Post a Comment