Sunday, July 28, 2013

WAZIRI WASIRA AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO-MAGU


Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Magu, Aileen Geofrey akimwonyesha kwa kuandika ubaoni, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu Stephen Wasira kwamba anajua kusoma na kuandika, baada ya Waziri Wasira kumuuliza kama anajua mambo hayo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Magu, Jacqueline Liana    Waziri Wasira alikuwa wilayani Magu, mkoani Mwanza juzi (24.7.2013) kwa ziara ya siku moja kukagua miradi ya maendeleo.
Mwenyekiti wa kikundi cha wanawake wajasiriamali cha Tujikomboe wilayani Magu, Maria Mwita akimweleza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu Stephen Wasira,shughuli mbalimbali zinazofanywa na kikundi hicho, Waziri Wasira alikuwa katika ziara ya siku moja wilayani Magu, mkoani Mwanza 
 WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu, Stephen Wasira,akimpongeza baada ya kumkabidhi hati ya kukamilisha mradi wa jamii Mwenyekiti wa Mtaa wa Ibidanja Ponsian Garimo,baada ya kukagua madarasa matano ya Shule ya Msingi Magu ambayo yalijengwa na TASAF kwa kushirikiana na wananchi. Waziri Wasira alikuwa wilayani Magu, mkoani Mwanza juzi (24.7.2013) kwa ziara ya siku moja kukagua miradi ya maendeleo
WACHEZAJI wa kikundi cha utamaduni cha Mwanalyaku Cultural Troupe cha wilayani Magu, mkoani Mwanza, wakitoa burudani wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu, Stephen Wasira alipotembelea juzi (24.7.2013) kijiji cha Kitongosima kilichopo katika wilaya ya Magu, mkoani Mwanza, kukagua shughuli za maendeleo.

No comments:

Post a Comment