Jeraha la Sheikh Ponda linavyoonekana kwa karibu |
Sheikh Ponda akiwa hospitalini |
Sheika Ponda akiwa wodini Muhimbili |
BAADA ya danadana ya Polisi kukwepa ukweli juu ya tukio la kupigwa risasi na kujeruhiwa kwa Sheikh Ponda Issa Ponda, ukweli sasa upo hadharani baada ya kiongozi huyo wa Umma wa Kiislam kuonesha jeraha hilo hadharani akiwa kalazwa Muhimbili.
Awali
Polisi mkoa wa Morogoro kupitia Kamanda wake Faustin Shilogile lilikuwa
likidai halijui lolote kuhusu tukio hilo, licha ya kukiri kwamba
ilitaka kumkamata kiongozi huyo kipenzi wa waislam walio wengi.
Tangu
jana vyombo vya habari vikitumia vyanzo vyake vya habari kutoka mjini
humo ikiwemo MICHARAZO viliripoti juu ya tukio hilo ambalo lilitokea
jioni mara baada ya Sheikh huyo kuhutubia kwenye Kongamano la Kiislam,
lakini Polisi ikawa inavunga kuwa haujui lolote.
Hatimaye
sheikh huyo alitua jijini mchana kwa matibabu katika hospitali ya
Muhimbili na 'kuwaumbua' wale waliokuwa wakikanusha taarifa hizo kwamba
hakuna kilichotokea juu ya kujeruhiwa kwake.
Mwenyekiti
wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amezungumza jijini Dar leo na kumtaka
Rais Jakaya Kikwete na IGP Saida Mwema kuangalia namna ya kuthibiti
jeshi la Polisi juu ya matumizi ya risasi za moto kwa raia wasio na
silaha yoyote.
Matukio
ya polisi kuwatwanga risasi raia kwa sasa imekuwa kama fasheni, kitu
ambacho kinawatia hofu raia juu ya umakini wa askari wa jeshi hilo
ambalo ni la usalama wa raia na mali zao.
No comments:
Post a Comment