Tuesday, August 20, 2013

MAVETERANI WAANDAA TAMASHA LA KUADHIMISHA MIAKA 15

Na Mwandishi Wetu
TIMU ya soka za maveterani na klabu za Jogging za mkoa wa Dar es Salaam zinatarajiwa kuchuana na kupamba tamasha maalum la kuadhimisha Miaka 15 ya Kituo cha Mazoezi cha  Home Gym litakalofanyika wiki ijayo jijini Dar es Salaam.
Tamasha hilo litakalohusisha michezo mingine kama ya kutunisha misuli, kunyanyua vitu vizito, kukimbiza wanyama kama Kuku, Kanga na Sungura litafanyika Agosti 31 kwenye kiwanja cha Mwenge, Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Home Gym, Andrew Mwangomango aliliambia gazeti hili jana kituo chao kimeandaa tamasha hilo kuadhimisha mafanikio yao tangu kilipoanzishwa rasmi mwaka 1998.
Mwangomango alisema tamasha hilo litaenda sambamba na burudani na michezo mbalimbali ikishirikisha klabu za maveterani na jogging na kutaja baadhi yake kuwa ni Mwenge Shooting, Mabenzi, Survey, Meeda, Mapambano, 501 Veterani, Home Gym wenyewe, Coca Cola Veterani, NMB Veterani, Magenge 20 Jogging Team, Kingungi Jogging na nyingine.
Mwangomango alisema kwa upande wa soka mshindi atazawadiwa Mbuzi aina ya Beberu huku upande wa watunisha misuli na kunyanyua vitu vizito na michezo mingine zawadi zao zitakuwa tofauti na hiyo, japo hakuweka bayana.
"Kwa sasa tunafanya mipango kwa ajili ya mgeni rasmi atakayeshiriki pamoja nasi katika tamasha hilo ambalo mbali na kusherehekea miaka 15 ya kituo chetu, lakini lina lengo la kujenga umoja, urafiki na kufahamiana miongoni mwa wanamichezo wa jijini Dar es Salaam," alisema.
Aliongeza kuwa kwa upande wa burudani wanatarajiwa tamasha lao kupambwa na bendi ya Victoria Sound baada ya bendi waliyoikusudia awali ya Extra Bongo siku hiyo ya Agosti 31 kuwa na majukumu mengine

No comments:

Post a Comment