Tuesday, August 13, 2013

TAASISI ZA KIFEDHA ZATAKIWA KUWA RAFIKI NA WAKULIMA


 
Na Esther macha wa matukiodaima.com ,Mbeya
TAASISI za kifedha zimetakiwa kuwa rafiki wa mkulima kwa karibu katika kuwapatia mikopo wakulima na kwamba mkulima anapofika kwenye taasisi hizo kwa ajili kuomba kupatiwa mkopo hupata shida kupatiwa mkopo huo tofauti na wafanyabiashara wakubwa.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bw.Said Mwambungu wakati alipotembelea mabanda ya wakulima katika John Mwakangale Jijini Mbeya.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa baadhi ya taasisi za kifedha zimekuwa na kasumba mbaya kwa wakulima ambapo zimekuwa zikiwabagua wakulima hao pindi wanapofika kuomba msaada wa kukopeshwa.
Aidha Bw. Mwambungu alisema kuwa wafanyakazi wa mabenki na taasisi zingine za kifedha wanatakiwa kuwa karibu na wakulima hao pia watumie zaidi taaluma na uzoefu wao  wa namna ya kuwasiadia wakulima hao ili waweze kujiinua kiuchumi.
Alisema kuwa mabenki na taasisi za kifedha zinatakiwa kuondokana na kasumba kwamba kwa vile ni mkulima hivyo hana uwezo wa kurejesha mkopo na kuwathamini sana wafanyabiashara pekee wakati mkulima akipewa elimu juu ya matumizi sahihi ya fedha anazokupeshwa anakuwa na uwezo mzuri tu wa  kurejesha mkopo huo.
  
“Mkulima huyu apewe elimu na taasisi hizo juu ya ureshaji wa fedha hizo, hapo atakuwa na urejeshaji mzuri katika fedha hizo”alisema Bw. mwambungu.

Alisema kuwa Mkulima bila ya kusaidiwa kwa vitendea kazi ataendelea kupiga hatua moja mbele na kurudi hatua tatu  nyuma badala ya kusonga mbele na kwamba hata maonyehso hayo ya wakulima hayata kuwa na  maana kama hawatapewa msaada wowote hususani taasifi za kifedha kuwapatia mawazo ya kuwawezesha kupiga mbele zaidi kiuchumi.

No comments:

Post a Comment