Monday, September 30, 2013

TAMASHA LA TUPO WANGAPI LILIVYO LINDIMA LEO



Ras Aluta Christopher Warioba akiongea na waandishi wa habari kwenye kongamano la wasanii wa Reggea lililofanyika leo kwenye viwanja vya BASATA
Ras Inocent akiongea neno kwenye kongamano la wasanii wa Reggea lililofanyika leo kwenye viwanja vya BASATA
Ras Ton akizungumza na vyombo vya habari wakati wa kongamano la Reggea lililofanyika leo  kwenye viwanja vya BASATA
 Ras Baraka akiwa kwenye stage akifanya maandalizi ya kuonesha burudani kwa wapenzi wa Reggea
Ras Inocent akitoa burudani kwenye kongamano  hilo.
Hata wakina mama nao walikuwepo
Hapa ni kuruka wa burudani
Mama huyu alishindwa kuvumilia music wa Reggea akaanza kucheza kwenye mvua
 Dabo akitoa burudani wakati mvua inanyesha yaani mzuka kulikuwa hakuna kusitisha furaha kwa wapenzi wa Reggea wwaliokuwa kwenye tamasha ilo
Ni burudani tu hakuna kusubilia mvua ikatike
  Ras Ikabonnga Katondo akiwa na Ras Anord Kalikawe kwenye kongamano lililofanyika leo  kwenye viwanja vya BASATA

2013/9/8 Geofrey Adroph CODE
Wafanyakazi wa Tulizana wakiwaamasisha wananchi waliofika kwenye viwanja vya Leaders Clubs kupima Virus vya Ukimwi na pia kutoa elimu ya maambukizi ya Virus hivyo
Mmoja wa wafanyakazi akimweleza jambo kwa umakini kijana aliyekuja  kupima ili aweze kutoka kwenye mtandao wa ngono kwenye viwanja vya Leaders Club
Mmoja wa wananchi waliochangia damu kwenye tamasha la "Tuko wangapi? Tulizana" kwenye viwanja vya Leades Clubs jana mchana
Mfanyakazi wa Tulizana akitoa elimu kuhusu matumiza ya Kondom aina ya Dume  kwa vijana waliofika kwenye Tamasha la "Tuko wangapi? Tulizana"
Baadhi ya wafanyakazi wakiwa wamepumzika baada ya kazi ngumu ya kuelimisha jamii juu ya kuachana na mtandao wa mapenzi  ambao unaweza kusababisha maambukizi ya vurus vya UKUMWI wakati wa Tamasha la "Tuko wangapi? Tulizana" lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club
Mfanyakazi wa Tulizana akitoa elimu kuhusu matumiza ya Kondom aina ya Salama  kwa vijana waliofika kwenye Tamasha la "Tuko wangapi? Tulizana" lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club
Upimaji wa Afya ukiendelea

Msiba Tena! Mac 2 B afariki, Watuguru naye katangulia


TASNIA ya sanaa nchini imeendelea kupata pigo baada ya mcharaza gitaa Joseph Watuguru na Mac Maliki Simba 'Mac 2 B wamefariki dunia siku ya leo.


Watuguru alifariki  katika hospitali ya Amana wakati Mac 2 B aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya, mtayarishaji wa muziki huo na Reggae kufariki leo asubuhi nyumbani kwao Yombo kwa Abiola.

Mac 2B aliyekuwa membaz wa kundi la Wateule alikuwa akisumbuliwa na miguu mpaka mauti yalipompata nyumbani kwao Yombo na anatarajiwa kuzikwa kesho asubuhi.

Naye Watuguru aliyewahi kutamba na bendi mbalimbali ikiwemo African Revolution 'Tamtam' na Mchinga Sound alifariki kutokana na kuugua muda mrefu na inaelezwa kuwa huenda naye akazikwa kesho.

MICHARAZO inatoa pole kwa wanafamilia, ndugu, jamaa na wadau wa sanaa kwa ujumla kwa misiba hiyo ambayo imekuja wakati tasnia hiyo ikiendelea kuomboleza vifo vya wasanii wengine waliotangulia mbele ya haki tangu mwaka jana.

PICHA ZA FAINALI YA KIGOLI 2013 JANA TRAVERTINE


PICHA ZA FAINALI YA KIGOLI 2013 JANA TRAVERTINE

 Washiriki wa shindano la Kigoli 2013 wakishambulia jukwaa mmoja mmoja katika fainali hizo zilizofanyika jana katika Hoteli ya Travertine jana usiku





 Mwaandaji wa shindano la Kigoli 2013 na Jaji Mkuu wa shindano hilo, Maimatha wa Jesse akicheza wimbo wa My No One wa Diamond katika fainali hizo

 Msanii wa kizazi kipya, Dyna alikuwepo kutumbuiza katika fainali hizo, hapa akiimba sambamba na shabiki wake

FRANSIC MIYEYUSHO AMTWANGA SADIK MOMBA KWA POINT


Bondia Sadiki Momba kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Fransic Miyeyusho wakati wa mpambano wao usiokuwa wa ubingwa uliofanyika siku ya jumapili katika ukumbi wa  Friends Coner  Manzese Dar es salaam Miyeyusho alishinda kwa pointi picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Sadiki Momba kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Fransic Miyeyusho wakati wa mpambano wao usiokuwa wa ubingwa uliofanyika siku ya jumapili katika ukumbi wa  Friends Coner  Manzese Dar es salaam Miyeyusho alishinda kwa pointi picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
refarii Sako Mtlya akimnyoosha mkono juu bondia  Fransic Miyeyusho baada ya kumgalagaza Bondia Sadiki Momba wakati wa mpambano wao picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Mussa Sunga kushoto akipambana na Fahiri Awadhi wakati wa mpambano wao uliofganyika jumapili Awadhi alishinda kwa Point picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi Nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akitoa maelezo ya DVD zake zenye mabambano ya ngumi makali kwa ajili ya kuangalia na kujifunza ngumi nzito zenye msisimko zinazofanyika duniani kote kocha huyo wa mchezo wa masumbwi alikuwa akionesha DVD za Lenox Lewis,Manny Paquaio,Mohamedi Ali,Floyd Mayweather, na wengine kibao picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi Nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akitoa maelezo ya DVD zake zenye mabambano ya ngumi makali kwa ajili ya kuangalia na kujifunza ngumi nzito zenye msisimko zinazofanyika duniani kote kocha huyo wa mchezo wa masumbwi alikuwa akionesha DVD za Lenox Lewis,Manny Paquaio,Mohamedi Ali,Floyd Mayweather, na wengine kibao picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Baadhi ya raia wa kigeni kutoka china waliokuja kumsapoti bondia mussa sunga wakiwa katika picha ya pamoja na bondia huyo
DVD KALI ZA MCHEZO WA NGUMI ZINAZOSAMBAZWA NA KOCHA SUPER D
Mashabiki wa mchezo wa masumbwi

TAMKO LA KUFANYIKA KWA TAMASHA LA UTAMADUNI HANDENI


NDUGU ZANGU WATANZANIA
NDUGU ZANGU WANA HANDENI
NDUGU MDAU WA UTAMADUNI, MABIBI NA MABWANA
SALAAM!
Mkuu wa Wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu, pichani.
Kwa heshima kubwa kwako naomba niwasilishe ombi kwenu kwa mdau yoyote wa utamaduni na Mtanzania kwa ujumla juu ya kuandaa Tamasha la Utamaduni wilaya ya Handeni, mkoani Tanga, ifikapo Desemba 14 mwaka huu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya Handeni, Dr Khalfany Haule, pichani.
Tamasha hilo tunakusudia kufanya katika Uwanja wa Azimio. Hata hivyo, Uwanja huu wa Azimio upo kwenye matengenezo, hivyo tunaweza kuendelea na tamasha letu kwa upande usiokuwa kwenye ukarabati.
Mbunge wa Handeni, Dr Abdallah Omari Kigoda, pichani.
Ndugu mdau na serikali kwa ujumla; kwa muda mrefu sasa kumekuwa kukifanyika matamasha ya kila aina katika mikoa mbalimbali ya Tanzania. Kabla ya yote, napenda kuwapongeza waandaaji wote wanaoandaa matamasha hayo yenye kujenga jamii inayoheshimu utamaduni wao
Kambi Mbwana, mratibu wa Tamasha la Utamaduni wilayani Handeni, mkoani Tanga, litakalofanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Yapo matamasha mengi yanayofanyika katika mikoa hiyo na nisingependa kuorodhesha yote zaidi ya kuwashukuru na kutambua mchango wao katika sekta ya Utamaduni hapa Tanzania.

Kwa kuandaa matamasha hayo na kufanyika kwa mafanikio licha ya kuwa na changamoto za kiubinadamu, imesababisha kujenga usawa kwa wadau wa utamaduni na wananchi kwa ujumla.

Leo hii pamoja namambo mengine, lakini mtu anajiona yupo mtupu, pindi anapodharau utamaduni wao na kukimbilia tamaduni za watu wan je, hususan waliokuwa kweny Mataifa makubwa.

Ndugu zangu wadau wa Handeni Kwetu, wilaya ya Handeni ni kati ya zile zinazokabiriwa na changamoto nyingi mno. Wilaya hii iliyopakana na wilaya Korogwe, imekuwa kwenye joto kubwa la kupokea wageni mbalimbali, huku kila mmoja akiwa na utamaduni wake.

Katika tamaduni hizo, wapo wale wanaoeneza mambo mazuri na wale wanaoeneza sumu, yani tamaduni zisizokuwa nzuri nao pia hawakosekani katika utitiri huo.

Kwa wale wanaofahamu mwingiliano wa watu katika wilaya ya Handeni, watakubaliana na mimi kuwa kuna kubadilishana kwa tamaduni kutoka upande mmoja kwenda mwingine.

Kwakuwa lengo ni kuongeza ufanisi katika kujieletea maendeleo yao; hakuna tatizo katika hilo. Hata hivyo, kwa kulijua hilo, ndipo tulipokaa na kubuni wazo la kuanzisha Tamasha la Utamaduni la Handeni Kwetu.

Wazo na jina la Tamasha hili kwa kiasi kikubwa linatokana na kuwapo kwa Mtandao blog yenye jina la Handeni Kwetu. Blog hii licha ya kupewa jina hilo, lakini inachanganya habari zote bila kubagua.

Ndio Gazeti tando lililojipatia umaarufu kwa kiasi kikubwa na kwa haraka mno. Mbali na blog hiyo, pia kuna forum yenye jina la Handeni Kwetu. Group hili lilianzishwa maalum kwa ajili ya kupeana mawazo na changamoto za kimaisha miongoni mwa jamii.

Group hili lilikuwa na dhamira pia ya kukusanya mawazo mapya na kuunganisha nguvu kwa ajili ya harakati za kimaisha. Tunashukuru kwa wale waliotuelewa na kushirikiana na sisi.

Kwa wale wanaofuatilia group hili, watakubaliana na mimi kuwa kwa sasa tumefikia hatua nzuri zaidi kwakuwa wengi wao wamekubali kushirikiana mawazo yao kwa ajili ya jambo la kimaendeleo.

Ndugu zangu wadau wa Handeni Kwetu; Tamasha la Handeni Kwetu linaandaliwa chini ya Kampuni inayojulikana kama Raha Company And Entertainment, yenye maskani yake jijini Dar es Salaam.

Kwa kupitia Kampuni hii; tunaamini kwa pamoja tutaweza kufanikisha kwa tamasha hili katika ardhi ya wilaya ya Handeni, mkoani Tanga. Sisi tunaamini kuwa changamoto nyingi zinaweza kujitokeza, ila tutakabiriana nazo kwa ajili ya kufungua historia mpya.

Tangu nchi hii ilipopata uhuru wake, katika wilaya ya Handeni na Tanga kama mkoa hakujakuwa na fursa kama hizo. Vijana wengi wana vipaji au wanapenda kushiriki kwenye mambo ya utamaduni, ila wanakosa sehemu ya kuonyesha kwa vjtendo.

Mbali na hilo, kwa wale wanaotamani kujiingiza kwenye mambo ya utamaduni na sanaa kwa ujumla, wanakosa sehemu ya kuongeza chachu yao kutokana na uhaba wa matasha ya aina hii.

Watu wanajiuliza, hata kama kuna kikundi au mtu anapenda mambo ya utamaduni, ila wapi aende kuonyesha? Swali jingine ni namna gani anaweza kuishi wakati wote anapokuwa kwenye harakati hizo?

Maswali haya na mengine yote yanaongeza ugumu katika kupambana na changamoto za kimaisha na sekta nzima ya Utamaduni. Pamoja na hayo; ndipo tulipoamua kuanzisha wazo hili.

Ndugu wadau wa Handeni Kwetu; Wazo aina hii halijakuja tu kiholela bali liliandaliwa na kupangiwa mtitiriko wote. Hata kuanzishwa kwa blog au group la Handeni Kwetu kulikwenda sambamba.

Ni kwa kupitia blog na group letu, tumeweza kujiingiza katika mtandao mpana wa kuweza kuuza mawazo yetu. Kuwaonyesha watu kile tunachokijua na kukithamini mbele ya jamii inayotuzunguuka.

Watu wanaoishi ndani ya Tanzania na nje ya nchi wamepata sehemu ya kuijua vyema wilaya ya Handeni. Sisi tunaamini kuwa hata kama sio leo au kesho, ila wapo wafanyabiashara, wawekezaji wanaweza kuguswa katika kuitembelea wilaya yetu na kuweka makazi.

Ndugu zangu wadau wa Handeni Kwetu; kwakuwa tayari tumeamua kuanzisha wazo kama hili, ni wakati wako wewe unayeguswa na mambo ya utamaduni kushirikiana na sisi.

Tunakuomba sana, kwa nafasi yako, uweze kushirikiana na sisi katika kufanikisha tamasha hili la Utamaduni la wilaya ya Handeni. Sisi tunaamini ushirikiano ndio unaoweza kufanikisha yote hayo.

Msaada wowote unaoona unafaa tupo tayari kuupokea. Kama unaona una taasisi yako, Kampuni yako au shirika na kuna uwezekano wa kudhamini, basi unakaribishwa, ambapo pia ni nafasi ya kujitangaza kwa wilaya hii.

Nashukuru kwa wale waliokubali kukaa pamoja na kulijadili suala hili hadi kutamani kudhamini katika Tamasha hili litakalofanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Maandalizi ya tamasha hili yanaendelea. Mazungumzo mengi yameshafanyika. Hadi kufikisha wazo hili kwenu, tulikaa chini na kujitafakari kwa kina juu ya kufanikisha kwa vitendo suala hili.

Ndugu zangu wadau wa Handeni Kwetu; sisi tunaamini serikali pekee haiwezi kuleta maendeleo ya mtu mmoja mmoja bila hata kushirikiana. Kwa kufanyika kwa tamasha hili, tunajua tutafungua fursa nyingine za kimaendeleo wakati wowote kuanzia sasa.

Tutaweza pia kukutana kwa pamoja watu wote katika tamasha hilo na kuweza kujadiliana juu ya mustakabari wa maisha yetu. Tutaweza kuitangaza vyema wilaya yetu.

Watu wenye nafasi zao, uwezo wao watakapoona juhudi hizo, wanaweza kuingia kwa miguu yote katika uwekezaji wa wilaya hii. Wote tunajua jinsi changamoto za uhaba wa maji na umeme unavyosumbua.

Kwa kufanyika kwa tamasha hili, kuna uwezekano mkubwa makampuni yanayotoa huduma wa umeme wa jua, uchimbaji wa visima na mengineyo kuguswa na kuwahudumia wananchi wote.

Pia tunaamini kuwa kwa kufikia hatua ya kuitangaza kama tulivyofanya kwa kuanzisha blog na forum, basi wageni wenye dhamira wanaweza kutembelea katika wilaya hii hivyo kukuza pato la Handeni na Tanzania kwa ujumla.

HITIMISHO

Tunajua wapo wanaoweza kujiuliza kwanini Handeni? Najua pia wapo watakaojiuliza maana ya Tamasha hili. Najua pia watu hao wanaweza kuingiza fikra nyingine, hasa za kisiasa.

Lakini watu hao wanapaswa kujua kuwa hakuna njia ya mkato inayofanywa katika kufanyika kwa tamasha hili. Ni kutokana na mapenzi ya dhati kwa wilaya hii, mkoa wa Tanga na Tanzania kwa ujumla.

Haya na mengine yote, yamesukuma hamu ya kuanzisha kwa tamasha hili ambalo tunaamini ni la kwanza kuwahi kufanyika kwa historia ya wilaya ya Handeni, mkoani Tanga, hivyo tutafurahi kama kila mmoja ataona faida ya kushirikiana na sisi ili tufanikishe maendeleo.

Katika hilo, tunaomba serikali kwa kupitia Mkuu wa Wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu, Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya, Mbunge wa Jimbo la Handeni, Ofisa Utamaduni wa wilaya na viongozi watuunge mkono bila kinyongo chochote kwa faida ya Handeni na watu wake.

Kadri ya mambo yatakavyosonga mbele, tutaendelea kujulishana kwa kupitia njia mbalimbali na kuwapa watu fursa ya kufuatilia mwelekeo wa Tamasha la Handeni Kwetu.

Pamoja ni Ushindi.
Tunathubutu, tutaweza na tutasonga mbele.
Mungu ibariki Handeni
Mungu ibariki Tanzania na watu wake wote.
Kambi Mbwana, Mratibu.

KAMATI ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) WAKUTANA

Amir Mhando

 
KAMATI ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) ilikutana Dar es Salaam Ijumaa Septemba 27, 2013 kujadili masuala mbalimbali chini ya Mwenyekiti wa chama hicho, Juma Pinto.
 
(A) MKUTANO WA KATIBA/UCHAGUZI MKUU
 
Kikao kilikubaliana sekretarieti ya TASWA ishirikiane na Kamati ya Katiba ya TASWA inayoongozwa na Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mwanaspoti, Frank Sanga kuhakikisha mchakato wa Rasimu ya Katiba mpya ya chama hicho unaenda vizuri.
 
Kamati  hiyo ya katiba itasimamia mchakato huo na ihakikishe kabla ya Desemba 15 mwaka huu, rasimu hiyo iwe tayari na ikabidhiwe kwa Kamati ya Utendaji ya TASWA, ambayo itaiwasilisha kwenye Mkutano Mkuu wa Katiba wa chama utakaofanyika Desemba 21 mwaka huu, mahali patakapotangazwa.
 
Hata hivyo Kamati ya Utendaji imeiagiza sekretarieti ya TASWA kujipanga vizuri ili kuhakikisha mkutano wa kujadili Katiba unafanyika nje ya Dar es Salaam kuwezesha wajumbe wawe watulivu zaidi na kufanya uamuzi sahihi kuhusiana na katiba yao.
 
Pia kikao hicho kimepanga Uchaguzi Mkuu wa TASWA ufanyike Januari 18 mwakani jijini Dar es Salaam. Utaratibu zaidi kuhusiana na uchaguzi huo utatangazwa, lakini si dhambi wala si nongwa kwa wanaotaka kuingia madarakani wakianza kutangaza nia mapema. Pia wanachama wametakiwa kulipia ada zao kabla ya Novemba 30 mwaka huu.
 
(B)  TUZO ZA WANAMICHEZO BORA
Chama chetu kila mwaka kimekuwa kikiendesha tuzo za Wanamichezo Bora, lakini mwaka huu tumechelewa kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo baadhi ya wadhamini waliokubali awali kutusaidia kushindwa kutekeleza ahadi zao.
 
Hata hivyo suala hilo sasa  limepatiwa ufumbuzi na Jumatano Oktoba 2, 2013, Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto atafanya mkutano na waandishi wa habari kwenye mgahawa wa City Sports Lounge, Dar es Salaam saa tano asubuhi kuzungumzia suala la tuzo pamoja na kutangaza tarehe ya kufanyika kwake. Atakuwepo pia Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo, Haji Manara.
 
(C)  MAFUNZO
Kama mnavyofahamu TASWA na Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (SJMC) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wameingia ushirikiano ya kuendesha mafunzo kwa waandishi wa habari za michezo nchini.

Kuna muelekeo mzuri kuhusiana na jambo hilo, ambapo vyombo hivyo vinaendelea na mazungumzo na wadhamini zaidi kwa nia ya kuyafanya mafunzo hayo yawe bora na tayari wapo waliojitolea kutusaidia ingawa ingawa si kwa bajeti yote.
 
(D)      Uchaguzi Mkuu wa TFF
Kikao kilijadili kwa kina suala la uchaguzi wa TFF na kuweka jambo hilo kiporo kwanza na kufanyia kazi baadhi ya changamoto, hadi Jumanne Oktoba 1 mwaka huu, ambapo kikao kingine cha Kamati ya Utendaji kitafanyika.
 
(E)       UANACHAM WA AIPS
TASWA ni mwanachama hai wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Duniani (AIPS) chenye makao yake makuu Lausanne, Uswisi na kila mwaka tumekuwa tukishiriki kwenye mikutano, lakini wanachama wetu asilimia kubwa hawana kadi za AIPS kwa vile si wanachama.

Faida za kadi hizo unaweza kutumia viwanja vya michezo mbalimbali duniani ambako kuna vyama vya waandishi wa habari za michezo.

Naomba kuwajulisha kuwa utaratibu wa kupata kadi za AIPS kwa mwaka 2014 tayari umeanza, hivyo kila mmoja kwa nafasi yake aombe kwa njia ya mtandao huu:http://www.aipsmedia.com/index.php?page=getcard.

Ukishakubaliwa fomu yako utaelekezwa uwasiliane na TASWA, ambapo utapewa utaratibu wa malipo ambayo ni dola za Marekani kumi (10) tu, ambapo gharama za utumaji wa ada hizo kwa fedha za kigeni kabla ya Novemba mosi mwaka huu chama kitaingia.

Lakini baada ya muda huo kupita, wale ambao watachelewa kujaza fomu bado watakuwa nayo nafasi ya kupata kadi hizo, ila watalazimika kuingia gharama za kutuma fedha za kigeni nje, ambazo chama hakitabeba tena jukumu hilo.
 
Nawasilisha.
 
Amir Mhando
 
Katibu Mkuu TASWA
29/09/2013

MISS UTALII TANZANIA, KUITANGAZIA DUNIA KUPATIKANA KWA NYATI WA AJABU NA PEKEE DUNIANI KATIKA HIFADHI NGORONGORO.


Miss Utalii Tanzania 2013, Hadija Said Mswaga, amesema kuwa kupatikana kwa nyati mweupe wa ajabu na pekee duniani katika hifadhi ya Ngorongoro, imekuwa ni chachu na kichocheo cha pekee kwake katika mpango mkakati wake wa kuitangaza Hifadhi ya Ngorongoro kitaifa na kimataifa, ambapo kwa kuanzia ameamua kuanza kampeni hiyo kupitia mashindano ya dunia anayokwenda kushiriki ya Miss Tourism World 2013, ambayo mwaka huu yanafanyikia nchini Equatorial Guinea Octoba 12, 2013.

Kupatikana kwa Nyati huyo wa ajabu Mweupe, ambaye hapatikani sehemu nyingine yoyote Duniani, wakati huu ambao anakwenda katika mashindano hayo ya Dunia, imekuwa ni fulsa ya pekee kwa Tanzania, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na kwake , kuithibitishia dunia kuwa Ngorongoro Cater ni Ajabu la Asili la Dunia Barani Afrika. Ambapo sasa Ngorongoro Crater  pamoja na maajabu ya bonde lenyewe la kreta ya Ngorongoro, pia kuna maajabu ya Nyati Mweupe, Unyayo wa Binadamu wa kale zaidi Duniani, Mchanga wa ajabu unao hama kila mwaka kwa umbo la Nusu mwezi, Mlima wenye Volkano Hai wa Oldonyo Lengai, lakini pia ushirikiano wa kuishi bila kudhuriana wa binadamu na Wanyama katika hifadhi hiyo na upatikanaji wa jamii karibu zote za Wanyama wakubwa (BIG FIVE) na adimu duniani wakiwemo Faru Weusi,Duma,Mbwa Mwitu, Kaka kuona n.k.
 
Ngorongoro Crater na Hifadhi nzima ya Ngorongoro ni tunu ya Taifa la Tanzania, nahazina ya Dunia ambayo tunapaswa kuienzi na kuitangaza kwa nguvu zetu zote, ili iweze kuingiza pato na kuchangia zaidi uchumi na pato la Taifa, lakini pia kukuza na kuendeleza huduma za jamii ,ikiwemo elimu na afya. Naupongeza uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kwa jitihada zao za kukuza utalii na kupambana na majangili , nawaomba kuimarisha na kuongeza mapambano na vita dhidi ya ujangili na majangili, ili kuhakikisha kuwa majangili hao hawamdhuru nyati huyo wa ajabu na Wanyama wengine katika hifadhi hiyo. Lakini pia naiomba mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kumlinda nyati huyo dhidi ya Wanyama wengine wala nyama kama samba n.k.

Wafanyakazi wa hifadhi hiyo Ijumaa ya tarehe 27-9-2013 asubuhi wakiwa katika basi la mamlaka wakienda kazini walimshudia Nyati huyo akiwa na kundi la nyati wengine kandokando ya barabara ndani ya hifadhi hiyo. Jambo ambalo liliwavutia na dereva wa basi hilo kulazimika kusimamisha basi kutoa fulsa kwa wafanyakazi hao kumshudia nyati huyo na baadhi yao kupiga picha kwa simu zao na kamera walizokuwa nazo.

Hadija ameushukuru uongozi wa Ngorongoro , kwa kumpatia DVD zaidi ya 100 ya hifadhi hiyo,ambazo atakwenda kuzigawa kwa washiriki wote 126 na vituo vya Televisheni vya nchi zao wanaoshiriki katika mashindano hayo ya Dunia ya Miss Tourism World 2013 mwaka huu. Baada ya kurudi nitazunguka nchi nzima na dunia nzima kuitangaza Ngorongoro kwa kushirikiana na Uongozi wa Miss Tourism Tanzania Organisation na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro

MAGAZETI YA MWANANCHI NA MTANZANIA YAFUNGIWA


SERIKALI imeyafungia  kutochapishwa Magazeti ya MWANANCHI na MTANZANIA kuanzia 27 Septemba,2013  kutokana na mwenendo wa magazeti hayo kuandika habari na makala  za uchochezi na uhasama kwa nia ya kusababisha wananchi wakose imani kwa vyombo vya dola hivyo kuhatarisha amani na mshikamano ulipo nchini.

Gazeti la MWANANCHI limefungiwa kutochapishwa kwa siku kumi na nne(14) kuanzia 27 Septemba,2013.Adhabu hii imetangazwa kwa Tangazo la Serikali(Government Notice )Namba 333 la tarehe 27 septemba,2013.

Gazeti la MWANANCHI limepewa adhabu hiyo kutokana na hivi karibuni kuchapisha habari zenye mwelekeo wa uchochezi na uvunjifu wa amani,mfano tarehe 17 Julai,2013 katika toleo Namba 4774 ilichapisha habari isemayo “MISHAHARA MIPYA SERIKALINI 2013”  kwa kuchapisha waraka uliozuiliwa kwa matumizi ya vyombo vya habari waraka huo ulikuwa wa Siri  haukupaswa kuchapishwa Magazetini.

Aidha, katika toleo la Jumamosi,tarehe 17 Agosti,2013 lilichapisha habari yenye kichwa kisemacho “WAISLAM WASALI CHINI YA ULINZI MKALI”  habari hiyo ilikolezwa na picha ya mbwa  mkali mwenye hasira.Habari na picha hiyo ilitoa tafsiri ya kuwa Jeshi la Polisi lilipeleka Mbwa katika maeneo ya ibada ya waumini wa dini ya kiislam.Jambo ambalo halikuwa la  ukweli.

Jeshi la Polisi katika doria siku hiyo halikupeleka mbwa katika maeneo ya Misikiti.Serikali na jeshi la Polisi linaheshimu na kuzingatia maadili ya dini ya Kiislamu na kwa hiyo Jeshi lake haliwezi kupitisha au kuingiza mbwa katika maeneo ya ibada.

Hivyo basi,kwa gazeti hili kuchapisha habari iliyokolezwa na picha ya mbwa ni uchochezi wa kulichonganisha Jeshi la Polisi na waumini wa dini ya kiislam  mbwa ni najisi hapaswi kuingia  katika maeneo ya ibada.

Gazeti la MTANZANIA limefungiwa kutochapishwa kwa siku tisini(90) kuanzia tarehe 27 Septemba,2013 kwa kuchapisha habari zenye uchochezi.Gazeti hili limeonywa mara nyingi  lirekebishe mtindo wake wa uandishi wa  kichochezi na lizingatie maadili na Sheria na Kanuni za  fani ya Habari.

Pamoja na kuonywa gazeti hili halikuonyesha kuzingatia maelekezo ya Msajili wa Magazeti, mfano ;katika toleo na 7262 la 20 Machi,2013 liliandika habari yenye kichwa kisemacho “URAIS WA DAMU”,tarehe 12 Juni,2013,toleo Namba 7344 lilichapisha makala isemayo “MAPINDUZI HAYAEPUKIKI”.

Aidha, siku ya Jumatano,tarehe 18 Septemba,2013 katika toleo Namba 73414 ukurasa wa mbele lilichapisha Kichwa cha habari kisemacho “SERIKALI YANUKA DAMU” taarifa hiyo ilikolezwa na picha zilizo unganishwa kwa ustadi mkubwa kwa kutumia kompyuta  kutapakaza rangi nyekundu mithili ya damu nyingi kumwagika .Katika habari hiyo gazeti hilo limedai bila uthibitisho kuwa Jeshi la Polisi linahusika  na wahanga waliomizwa na watu wasiojulikana kwa kumwagiwa tindikali na  waliyovamiwa na kujeruhiwa vibaya.

Vile vile gazeti hilo limeishtumu serikali kuwa goigoi katika kushughulikia matukio yenye sura ya kigaidi.

Kwa ujumla wake habari hiyo ni ya kichochezi ina lengo la kuwafanya wananchi wavichukie vyombo vya ulinzi na usalama  wavione kuwa haviwasaidii.

Kutokana na makosa yalitajwa hapo juu serikali imelifungia gazeti la Mtanzania  kutochapishwa kwa muda wa siku tisini(90) kwa Tangazo la Serikali Namba 332(Government Notice No.332) la tarehe 27 septemba,2013,.
Serikali inawataka wamiliki,wahariri na wanahabari kwa ujumla kuwa makini,kuzingatia weledi,miiko na madili yataaluma uandishi wa habari.

Serikali inawataka wamiliki na hasa wahariri kuhakisha kuwa habari wanazoziandika na vipindi wanavyoviandaa vinazingatia taaluma,kuweka mbele maslahi ya taifa letu kwa kuwa na uzalendo wa hali ya juu.

Serikali inavionya vyombo vya habari vinavyoutumia uhuru wa habari bila wajibu kuwa haitasita kuvichukulia hatua kali ikiwemo ya kuvifungia .Serikali haitakubali kuona vyombo vya habari kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani  nchini.
Imetolewa na
MKURUGENZI IDARA YA HABARI
WIZARA YA HABARI,VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
28 SEPTEMBA,2013