Miss
Utalii Tanzania 2013, Hadija Said Mswaga, amesema kuwa kupatikana kwa nyati mweupe
wa ajabu na pekee duniani katika hifadhi ya Ngorongoro, imekuwa ni chachu na
kichocheo cha pekee kwake katika mpango mkakati wake wa kuitangaza Hifadhi ya
Ngorongoro kitaifa na kimataifa, ambapo kwa kuanzia ameamua kuanza kampeni hiyo
kupitia mashindano ya dunia anayokwenda kushiriki ya Miss Tourism World 2013,
ambayo mwaka huu yanafanyikia nchini Equatorial Guinea Octoba 12, 2013.
Kupatikana
kwa Nyati huyo wa ajabu Mweupe, ambaye hapatikani sehemu nyingine yoyote
Duniani, wakati huu ambao anakwenda katika mashindano hayo ya Dunia, imekuwa ni
fulsa ya pekee kwa Tanzania, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na kwake ,
kuithibitishia dunia kuwa Ngorongoro Cater ni Ajabu la Asili la Dunia Barani
Afrika. Ambapo sasa Ngorongoro Crater
pamoja na maajabu ya bonde lenyewe la kreta ya Ngorongoro, pia kuna
maajabu ya Nyati Mweupe, Unyayo wa Binadamu wa kale zaidi Duniani, Mchanga wa
ajabu unao hama kila mwaka kwa umbo la Nusu mwezi, Mlima wenye Volkano Hai wa
Oldonyo Lengai, lakini pia ushirikiano wa kuishi bila kudhuriana wa binadamu na
Wanyama katika hifadhi hiyo na upatikanaji wa jamii karibu zote za Wanyama wakubwa
(BIG FIVE) na adimu duniani wakiwemo Faru Weusi,Duma,Mbwa Mwitu, Kaka kuona
n.k.
Ngorongoro
Crater na Hifadhi nzima ya Ngorongoro ni tunu ya Taifa la Tanzania, nahazina ya
Dunia ambayo tunapaswa kuienzi na kuitangaza kwa nguvu zetu zote, ili iweze
kuingiza pato na kuchangia zaidi uchumi na pato la Taifa, lakini pia kukuza na
kuendeleza huduma za jamii ,ikiwemo elimu na afya. Naupongeza uongozi wa
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kwa jitihada zao za kukuza utalii na
kupambana na majangili , nawaomba kuimarisha na kuongeza mapambano na vita dhidi
ya ujangili na majangili, ili kuhakikisha kuwa majangili hao hawamdhuru nyati
huyo wa ajabu na Wanyama wengine katika hifadhi hiyo. Lakini pia naiomba
mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kumlinda nyati huyo dhidi ya Wanyama wengine
wala nyama kama samba n.k.
Wafanyakazi
wa hifadhi hiyo Ijumaa ya tarehe 27-9-2013 asubuhi wakiwa katika basi la
mamlaka wakienda kazini walimshudia Nyati huyo akiwa na kundi la nyati wengine kandokando
ya barabara ndani ya hifadhi hiyo. Jambo ambalo liliwavutia na dereva wa basi
hilo kulazimika kusimamisha basi kutoa fulsa kwa wafanyakazi hao kumshudia
nyati huyo na baadhi yao kupiga picha kwa simu zao na kamera walizokuwa nazo.
No comments:
Post a Comment