Mhariri wa Championi Ijumaa, John Joseph
akimkabidhi glovu mbili, bondia mkongwe nchini Rashid Matumla. Vifaa hivyo
vimetolewa na gazeti la Championi ukiwa ni msaada kwa Matumla kwa ajili ya
kusaidia ndoto yake ya kuanzisha shule ya ngumi.
Wengine katika picha hiyo ni Mhariri
Kiongozi wa Championi, Saleh Ally (wa pili kulia) aliyeratibu zoezi hilo. Wanaoshuhudia ni waandishi wa gazeti hilo,
Wilbert Molandi na Martha Mboma.
Matumla amekuwa na ndoto ya kuanzisha
shule ya ngumi lakini hana mtaji, hata Championi halijatoa vifaa vya kutosha,
lakini uongozi wa gazeti hili umekuwa ukisisitiza wadau wajitokeze zaidi
kumsaidia Matumla kutimiza ndoto yake.
Bingwa huyo wa zamani wa dunia mara
mbili, amekuwa akiandamwa na ugonjwa wa ganzi na maumivu makali kwenye uti wa
mgongo na daktari amemshauri kutoendelea kupigana ili kuokoa maisha yake.
Matumla amesema anaweza kuendeleza
maisha yake kwa kufungua shule ambayo anaamini itazalisha wachezaji wengi nyota
wa mchezo wa ngumi.
Championi limeamua kumsaidia katika hilo
na kuendelea kuhimiza wadau kujitokeza zaidi kumsaidia ili atimize ndoto hiyo
kwa kupata vifaa na kulipa pango angalau la mwaka, angalau aanzishe Matumla
Boxing School.
PICHA NA KHATIM NAHEKA
No comments:
Post a Comment