Na Mwandishi Wetu
VIDEO
Queen wa Bongo, Agnes Gerald Waya ‘Masogange’ na shosti yake, Melissa
Edward wapo huru kufuatia kesi iliyokuwa ikisikilizwa nchini Afrika
Kusini ya kukamatwa na madawa ya kulevya aina ya Crystal Methamphetamine
ya Sh. bilioni 6.8, lakini baadhi ya wadau nchini wanasema kuna mchezo
umechezwa, Imebainika mambo ya kushangaza nyuma ya pazia.
Masogange
na Melissa walikamatwa Julai 5, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Oliver Tambo uliopo Kempton Park jijini Johannesburg nchini
humo. Wawili hao wameishi mahabusu kwa saa 1824.
MMOJA HURU, MMOJA AHUKUMIWA.
MMOJA HURU, MMOJA AHUKUMIWA.
Melissa Edward. |
Uhuru
wa Masogange ni baada ya Mahakama ya Kempton jijini Johannesburg kumtia
hatiani kwa kuingiza kemikali hatari nchini humo, akatakiwa kulipa
faini ya randi 30,000 (Sh. milioni 4.8 za Bongo) au kifungo cha miaka 2
jela.
Kwa
upande wake Melissa yeye hakukutwa na hatia kwa vile ilibainika mizigo
aliyokutwa nayo aliombwa na Masogange amsaidie kubeba baada ya kukutana
ndani ya ndege ya Shirika la South Africa Airlines.
KUMBE SI CRYSTAL MATHAMPHETAMINE
Habari
kutoka nchini humo zinasema mdhamini wa Masogange (jina halijapatikana)
alipigana kuhakikisha staa huyo na nduguye ambaye amezaliwa naye kwa
mama mkubwa wanakuwa huru na kurejea Bongo.
Katika
kupigana huko, mdhamini huyo alifurahia matokeo ya uchunguzi wa mkemia
mkuu wa serikali ya nchi hiyo kuyaona madawa hayo kuwa si Crystal
Methamphetamine bali ni Ephedrine ambayo si unga ila ni kemikali hatari
ambayo ikichanganywa na dawa nyingine hupatikana unga halisi.
Kwa
Bongo madawa hayohayo ni unga na tayari watu wengi wapo korokoroni kwa
kukamatwa nayo akiwemo aliyekuwa rafiki wa marehemu Steven Kanumba,
Saada Ally.
Mangunga |
Katika
hilo, mtu anayekamatwa na madawa hayo nchini humo hushtakiwa kwa kosa
la kuingiza kemikali hatari. Serikali ya Afrika Kusini ilipiga marufuku
kuingizwa nchini humo kwa madawa hayo na adhabu yake iko wazi.
“Yule
mdhamini alipojua mkemia mkuu amesema yale si Crystal Methamphetamine
bali ni Ephedrine aliitumia nafasi hiyo kucheza na mwanasheria ambapo
kifungo chake kinajulikana,” alisema mtoa habari wetu mmoja.
MSEMAJI WA ‘TRA’ YA SAUZ AINGIA SHAKA.
Habari
zinasema kuwa, kufuatia taarifa za mahakama kwamba mzigo huo si Crystal
Methamphetamine bali ni Ephedrine Msemaji wa Mamlaka ya Mapato ya
Afrika Kusini (SARS), Marika Muller alisema kuwa timu yake ina uhakika
wa asilimia mia moja kwamba, mzigo wote wa Masogange na Melissa
walioukamatwa nao ni madawa ya kulevya aina ya Crystal Meth.
Muller
akatoa la moyoni akisema kwamba, kama mahakama imekubaliana na matokeo
ya uchunguzi wa mkemia mkuu wa nchi hiyo, yeye hana la kusema kwa kuwa
uamuzi wa korti ni wa mwisho.
KAMANDA NZOWA ANYOOSHA MIKONO.
Ijumaa
Wikienda lilimtafuta Kamanda wa Kikosi cha Kudhibiti na Kupambana na
Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa ambapo alipoulizwa juzi kama
serikali ina mpango wa kumkamata Masogange atakaporejea nchini ili
awataje waliomtuma, alisema:
“Sasa
kama wameachiwa kule, sisi tutawakamataje? Hatuna sababu ya kufanya
hivyo, kesi ilisikilizwa kule mahakama ikafikia ilipofikia, basi tena!
Ila tutafuatilia chini kwa chini mtandao huo.”
MCHEZO UMECHEZWA:- Jijini
Dar es Salaam, baadhi ya wasomaji walipozungumza na gazeti hili juzi
walitilia shaka kuwepo kwa mazingira ya kuchakachuliwa kwa madawa hayo. Walisema
kuwa, ilikuwaje SARS iwakamate akina Masogange na kugundua walibeba
Crystal Meth (unga) halafu mahakama iseme ni Ephedrine (kemikali
hatari)?
“Hivi
jamani, hiki sasa ni kiini macho. Tuliambiwa lakini watatoka tu.
Mamlaka ya mapato kule Sauzi waliona ni madawa ya kulevya, mahakama
ikaona ni kemikali hatari, mnadhani nani mkweli hapo?” alihoji msomaji
aliyejitambulisha kwa jina la Aunt Elizabeth, mkazi wa Mbezi Beach, Dar.
Wengine walitupia kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook, Instagram na Twitter wakidai hivyohivyo kwamba kuna mchezo umechezwa.
“Kwanza wamekamatwa Julai 5, mwaka huu. Kesi imeisha katikati ya wiki iliyopita, hata miezi mitatu haikufika. Hapa Bongo, yule mama Leila (Mwanaidi Mfundo) na wenzake walikamatwa 2011 kwa unga huohuo, kesi yao bado ipo Mahakama Kuu, Dar hadi leo,” alisema Samuel Msalanda wa Ilala, Dar.
Wengi
walionesha kutilia shaka hukumu hiyo kutokana na mitazamo yao lakini
Mahakama ya Kempton jijini Johannesburg, Afrika Kusini ndivyo
ilivyoamua.
MASWALI TATA:- Ukiachana
na mitazamo na ukweli ulivyo, bado kuna maswali tata ambayo utatuzi
wake unakuwa mgumu kulingana na kesi yenyewe kuanzia kutajwa,
kusikilizwa hadi hukumu ilikuwa nje ya Tanzania.
Je, mwenyewe Masogange alipokuwa akisafirisha dawa hizo alijua ni kemikali hatari ambayo ni mali ghafi ya madawa ya kulevya?
Iwe ni kemikali au la! Alitoa wapi mali ghafi hiyo na alikuwa akimpelekea nani kule Afrika Kusini?
Ni kigogo au mtu gani aliyeratibu safari hiyo mpaka Masogange akafanikiwa kupita kwenda Afrika Kusini?
Nani alimpeleka Masogange hadi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)?
Kituo cha kwanza cha Masogange kuondokea kwenda JNIA kilikuwa wapi?
Inawezekana ni nyumbani kwake ambapo alilala na mizigo yote ile?
Kama
mahakama imebaini Masogange hakuingia Afrika Kusini na unga, vipi
kuhusu wale wafanyakazi wa JNIA walioachishwa kazi na Waziri wa
Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe kwa kuzembea Masogange akapita na ule
mzigo?
Yupo wapi Nassoro Mangunga aliyetajwa na Dk. Mwakyembe kuwa alifanikiwa kutoroka na mabegi matatu ya unga kule Sauzi?
Habari kwa hisani ya Global Publishers
No comments:
Post a Comment