Tuesday, September 3, 2013
NHIF YAZINDUA HUDUMA ZA BIMA YA AFYA YA JAMII (CHF)MJINI KILWA 1
Adoh
Mapunda Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilwa akipokea vifaa maalum vya
kuhifadhia fedha na nyaraka mbalimbali kutoka kwa Balozi Ali Mchumo
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
(NHIF) wakati wa uzinduzi wa Huduma za Bimaya Afya (CHF)katika
halmashauri hiyo uliofanyika jana kwenye viwanja vya Mkapa Garden Mjini
Kilwa, wa pili kulia anayeshuhudia tukio hilo ni Kaimu Mkurugenzi wa
(NHIF) Khamis Mdee na kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), Athuman Rehani
na Fortunata Raymond Msimamizi wa NHIF mkoani Lindi.wananchi
mbalimbali wakiwemo wazee walijitokeza katika zoezi la upimaji wa afya
yakiwemo magonjwa ya Kisukari, Shinikizo la Damu ikiwani pamoja na
kupima Uzito Urefu. Ado
Mapunda Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilwa akikata utepe kuashiria uzinduzi
rasmi wa huduma za Bima ya Afya katika Halmashauri ya wilaya ya Kilwa
jana kulia ni Bw. Khamis Mdee Kaimu Mkurugenzi NHIF na kushoto ni Dr.
Hilda Mwakipesile kutoka NHIF Baadhi ya wazee wakisubiri kupata huduma ya upimaji wa afya zao katika viwanja vya Mkapa Garden mjini Kilwa jana Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Mfuko wa taifa wa Bima ya Afya NHIF Balozi Ali Mchumo akipata huduma ya vipimo kutoka kwa mmoja wa madaktari wa NHIF jana anayeshuhudia ni mama Fatma Said Ali Mke wa Balozi Ali Mchumo
No comments:
Post a Comment