Sheikh Ponda Akishuka kwenye
basi la Magereza tayari kuingia Mahakamani Kusikiliza kesi yake inayomkabili
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoani Morogoro.
Sheikh Ponda anashtikiwa
katika Mahakama hiyo akikabiliwa na Mashtaka Matatu ambayo inadaiwa aliyatenda
Mkoani Morogoro katika Mkutano hadhara mwezi uliopita.
Kiongozi
huyo wa umma wa Kiislam Tanzania amenyimwa dhamana na hivyo kurejeshwa
tena rumande mpaka kesi yake itakaposomwa tena Oktoba Mosi.
Sheikh Ponda akiwa
Chini ya Ulinzi Mkali wakati akiingia Mahakamani kusikiliza kesi yake
inayomkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoani Morogoro.
Wafusi wa Sheikh Ponda
wakiwa wakiwa mahakamani leo kusikiliza kesi ya Kiongozi wao iliyokuwa imetajwa
mahama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro.
Ulinzi mkali ukiwa
umeimarishwa mahakamani leo wakati kesi hiyo ikiendelea mjini Morogoro.
No comments:
Post a Comment