Mkurugenzi mkuu wa Airtel Nigeria Segun Ognsanya Katikati akiwakabithi captain wa timu ya wasichana Tanzania
Wachezaji wa timu ya wasichana ya Tanzania ya Airtel Rising stars wakishangilia ushindi
Mwakilishi wa
Airtel Tanzania bi Lilian Kibiriti akifurahia ushindi na Wachezaji wa
timu ya wasichana ya Tanzania ya Airtel Rising stars mara baada ya
kuibuka mabigwa wa michuano ya Airtel Rising stars ya Afrika
Mkurugenzi
mkuu wa Airtel Nigeria Segun Ognsanya Katikati akiwakabithi captain wa
timu ya wasichana Tanzania na kocha wa timu ya wasichana Rogacian
Kaijage zawadi za ushindi mara baada ya kuibuka mabigwa wa michuano ya
Airtel Rising stars ya Afrika.
----------------------------------------
Timu
ya wasichana ya Tanzania imeibuka mabigwa katika michuano ya vijana
chini ya umri wa miaka 17 ya kimataifa ya Airtel Rising Stars yaliyokuwa
yanafanyika mwaka huu nchi Nigeria.
Tanzania
ilipata ubigwa huo baada ya kuchuana vikali na timu ya Kenya katika
mechi ya Fainali na kuifunga Kenya goli moja bila na kuibuka mabingwa .
Donisia Daniel ndio alipeleka furaha kwa upande wa Tanzania.
Tanzania
ilikua kundi moja na Sierra-Leone , Malawi , na Uganda. Walishinda
mechi moja dhidi ya Sierra-Leone 2-1 , wakapoteza mchezo dhidi ya Uganda
na kutoka sare na Malawi 1-1
Wakashinda
4-2 katika mikwaju ya penati dhidi ya DRC katika robo fainali mechi
zilizopigwa katika uwanja wa NIS Sports. Na wakawatoa Uganda kwa mvua ya
magoli 8-1
Mbali
na ushindi huo wa wasichana watanzania walijishindia zawadi mbalimbali
ikiwemo , Mchezaji bora kwa upande wa wasichana Tatu Iddi, Mfungaji bora
wa mashindano kwa upande wa wavulana Athanas Mdam na Mfungaji bora kwa
upande wa wasichana Shelda Boniface.
Kwa
upande wa wavulana Timu ya Niger wametetea tena ubingwa baada ya
kuifunga Zambia kwa mikwaju ya penati 7-6 katika mechi ya fainali ya
Airtel Rising Stars ilifanyika kweny uwanja wa Agege nchini Nigeria.
Niger
wamefanya vizuri kuanzia hatua ya makundi baada ya kushinda michezo
yote katika makundi na kufikisha magoli 12 na kuruhusu magili matatu tu
katika mechi sita . Jumla ya mechi 58 zimechezwa katika mashinda Aidha timu ya wavulana ya Tanzania imeshikilia nafasi ya nne kati ya timu zaidi ya 16 zilizoshiriki michuano hiyo
Michuano
ya kimataifa ya Airtel Rising Stars kwa mwaka huu yamefanyika nchini
Nigeria katika viwanja vinne Agege, Township Stadium, Legacy Pitch,
National Institute for Sports Fiels na Main bowl .
Kulianza
na “ gala night” jumapili usiku ikafatia sherehe za ufunguzi , na
mechi za ufunguzi za makudi katika uwanja wa AgegeTownship .
Mashindano
ya kiamataifa ya umri chini ya miaka 17 ya Airtel Rising Stars
yanafanyika kwa mara ya pili , mashindano haya yamekua bora kwa vijana
wadogo na kwakuzingatia jinsia.
No comments:
Post a Comment