Thursday, September 26, 2013

WAREMBO 15 KUPANDA JUKWAANI IJUMAA KUWANIA TAJI LA MISS UNIVERSE TANZANIA 2013


 Mkurugenzi wa Kampuni ya Compass Communications,  Maria Sarungi akizungumza katika uzinduzi wa mashindano ya mwaka huu ya Miss Universe Tanzania ambayo yamepangwa kufanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Ijumaa. Kushoto ni mratibu wa mashindano hayo, Mwanakombo Salim na kulia ni mwakilishi wa kampuni ya Fastjet, Gean Uku.
 Warembo 15 wanaowania taji la Miss Universe Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutambulishwa na waandaaji. Warembo hao watapambana Ijumaa kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Ijumaa.
Na  Mwandishi Wetu
MASHINDANO ya kumsaka mrembo wa Miss Universe Tanzania yatafanyika Ijumaa kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Posta kwa kushirikisha jumla ya warembo 15.

Warembo hao kwa sasa wapo kambini  kwenye hotel ya Urban Rose wakijifua kuwania tiketi ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa yaliyopangwa kufanyika mjini Moscow, Russion Novemba 9 mwaka huu.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Compass Commuications, Maria Sarungi aliwataja warembo hao kuwa ni  Aziza Victoria, Irene Nsiima, Betty Boniface, Kundi Mlingwa, Mariam Ngwangwa na Naomi Kisaka.

Wengine kwa mujibu wa Maria ni Glady Msemo, Salsha Lukiko, Upendo Dickson, Vestina Mhagama,  Angela Lutataza , Consolata Mosha, Clara Noor,  Agnes Thobias, Dinah David n Clara Noor.

Alisema kuwa warembo hao wamepata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania baada ya kupita katika mchujo wao walioendesha katika mikoa nane ya Tanzania Bara. Mikoa hiyo ni Mwanza, Arusha, Mtwara, Manyara, Mbeya, Dodoma, Kilimanjaro na wenyeji  Dar es Salaam.

Alifafanua kuwa lengo lao kubwa ni kupata mshindi ambaye atailetea sifa Tanzania kama ilivyokuwa kwa Flaviana Matata mwaka 2007 na kuingia katika hatua ya sita bora nchini Mexico. Mashindano hayo yamedhaminiwa na TANAPA, Fastjet, Mohamed Enterprises (MetL),  Coca-Cola, Missie Popular Blog, Healthy Beauty Clinic, Beauty Point, Sia Couture, Seif Kabelele Blog, AZH Photography.com na Adams Digicom.

Mrembo ambaye kwa sasa anashikilia taji ni Winfrida Dominique. Warembo wengine waliopita wa ambao hawakuweza kufurukuta katika mashindano ya kimataifa ni Amanda Ole Sulul (2008), Illuminata James (2009), Hellen Dausen (2010) na Nelly Alexandra Kamwelu (2011).

No comments:

Post a Comment